CCM na upotoshaji: Tanzania ni ya tisa duniani kutoa walinda amani sio ya tisa kwa amani duniani

Huu upoyoshaji wa makusudi au kutokujua kusoma ndio kikwako "kiingereza" wamekuja na propaganda kuwa UN yaitaja tanzania kama nchi ya 9 kwa amani duniani kitu ambacho sio kweli.

Tanzania ni ya 9 kutoa walinda amani ambao hata ivyo jeshi na serikali haijawai kusema ni wanajeshi kiasi gani wako nje ya nchi.

Na kibaya zaidi hata hao wanajeshi wakirudi hawalipwi stahiki zao kama inavyostahili na.mikataba yao ya amani hawaijui.


View attachment 789595
Wanajeshi hawalipwi!!! Be serious na careful mkuu,umeongelea idara nzito sana kwa ishu ya uongo.
 
Huu upoyoshaji wa makusudi au kutokujua kusoma ndio kikwako "kiingereza" wamekuja na propaganda kuwa UN yaitaja tanzania kama nchi ya 9 kwa amani duniani kitu ambacho sio kweli.

Tanzania ni ya 9 kutoa walinda amani ambao hata ivyo jeshi na serikali haijawai kusema ni wanajeshi kiasi gani wako nje ya nchi.

Na kibaya zaidi hata hao wanajeshi wakirudi hawalipwi stahiki zao kama inavyostahili na.mikataba yao ya amani hawaijui.


View attachment 789595
Chanzo chako Gazetini
Wakupuuzwa
 
Unalingnisha na nchi gani? Maana humu tunakwenda na data. Humu hapakufai kazungushe vidole juu na Madela huko ufipa
Ni kwanza duniani mkuu, maana kwingine kama Marekani Kusini taarifa za hayo mambo zinatolewa na dola. Ufipa ni wapi mimi nipo Arusha, Madela ya wale wasomali akina Kinana kwa kweli nayaona pale mjini kati lakini hayanihusu kabisa.
 
RIPOTI ya Tathmini ya Amani na Utengamano kwa mwaka 2017, imeitaja Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na amani; na iko kwenye 10 bora kwa kushika nafasi ya tisa katika nchi za Afrika zenye amani.

Ripoti hiyo, iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Masuala ya Uchumi na Amani duniani (IEP), iliitaja pia Tanzania kuwa ni nchi ya 54 kati ya nchi 163 kwa amani wakati nchi za Sudani Kusini, Libya, Somalia na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) zilitajwa kuwa miongoni mwa nchi 10 zenye hali mbaya ya amani duniani. Taasisi hiyo, imefanya uchunguzi wake wa hali ya amani na utengemano kwa nchi zote 163 duniani kwa kutumia vigezo 23 vinavyoangalia hali ya ubora na kiasi cha amani kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Mambo makubwa yaliyoangaliwa katika ripoti hiyo ni matatu ambayo ni hali ya ulinzi na usalama wa raia, kiwango cha migogoro ya ndani na ya kimataifa inayoendelea na hali ya jeshi la nchi husika. Kwa mujibu wa matokeo ya ripoti hiyo hali ya amani mwaka jana iliimarika kwa asilimia 0.28, ambapo nchi 93 ziliimarisha amani wakati nchi 60 amani ilishuka. Nchi ya Iceland imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuongoza kwa kuwa na amani duniani tangu mwaka 2008, ikifuatiwa na nchi za New Zealand na Ureno wakati nchi za Syria, Afghanistan, Yemen, Sudan Kusini na Somalia zimeendelea kuwa na hali mbaya ya amani. Aidha, kwa upande wa nchi za Afrika, Tanzania imeendelea kushika nafasi hiyo ya 54 kwa kuwa na amani kati ya nchi 163 duniani kwa miaka mitatu mfululizo.

Wakati Tanzania ikishika nafasi hiyo ya kwanza kwa amani kwa nchi za Afrika Mashariki na ya 54 duniani, nchi ya Uganda ilishika nafasi ya 105, Rwanda 113, Kenya 125 na Burundi 141 duniani. Nchi nyingine za Afrika zilizoingia kwenye 10 bora kwa amani ni pamoja na Sierra Leone iliyoshika namba 39, Ghana 43, Malawi 48, Namibia 50, Senegal 60, Equatorial Guinea 61, Togo 63, Guinea 69, Morocco 75 na Swaziland 77. Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo, chanzo kikubwa cha nchi zilizoshuka kwa hali ya amani, ni kushuka kwa ulinzi na usalama wa raia hasa kwenye nchi za Jangwa la Sahara kutokana na kuongezeka kwa matendo ya ugaidi na hali mbaya ya kisiasa.

Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa Ulaya inaongoza kwa kuwa na nchi tano zilizoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na amani, huku Mashariki ya Kati, Kaskazini mwa Afrika na Jangwa la Sahara zikiwa na nchi zilizoshuka kwa kuwa na amani. Kwa Jangwa la Sahara kati ya nchi 44, nchi 22 amani yake ilishuka zikiwemo nchi za Ethiopia, Burundi, Mali na Lesotho kutokana na matukio ya Ugaidi na hali mbaya ya kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, athari za matukio ya vita zinakadiriwa kusababisha hasara ya dola za Marekani trilioni 1.04 duniani, wakati matumizi ya kujenga amani yanakadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 10. Taasisi hiyo ya IEP, yenye makao yake makuu Sydney, New York na Brussels ni taasisi huru inayofanya kazi na washirika mbalimbali katika kufuatilia hali ya uchumi na amani duniani. Na hii ni ripoti yake ya 11 ya hali ya amani na utengemano duniani.
 
kalulukalunde
Hebu tuwekee hiyo ripoti tuione kwa macho yetu vinginevyo hayo mnayopika huko Lumumba ni upumbavu mtupu. Aidha baba yako hakuwamo kwenye orodha ya waliotekwa na kuuawa na wasiojulikana ndiyo maana unatuletea ungese huu
 
Tanzania is the Most Peaceful Nation in East Africa - Report

According to the recently released 2017 Global Peace Index Report Tanzania is most peaceful and calm nation in East Africa, it ranks number nine on the continent and number 54 in the global rankings. The report also reveals that Tanzania has less weapons imports, low levels of violent crime and a decline in external conflicts fought.

source:www.allafrica.com
usipende kulishwa matango pori
Kama lile ni tango pori nitaaminije hili lako si tango pori!?

Hivi kati ya gazeti la Majira ambalo tuko nalo hapahapa home for many yrs now na hiyo website ni ipi inaweza ikaungwa mkono na Watanzania wengi likitokea suala la kuaminiwa nchini!?

Shida yako ni kukurupukia website za kigeni ambazo hizohizo wakati mwingine zikitoa habari zisiyowapendeza mnaanza kupaniki ovyoovyo tu maana hauwezi hata kuzifungia.
 
Back
Top Bottom