CCM na ujangili uliokithiri wizi na unafiki wa kutisha

Kazimzubwee

Member
Nov 7, 2016
51
57
Ndugu amani iwe nanyi, Ujangili unaotendeka nchi hii vinara wake wapo CCM,kila uchafu na wizi wa rasilinali za nchi hii vinara watoka CCM na mbaya zaidi wametufanya wtz wote hatuna akili.

Haiwezekani tembo wanaisha na faru wameshatoweka wakati kuna kikosi maalum cha kulinda hawa wanyama,pia kuna TANAPA. Haiingii akili hata kidogo serikali baada ichukue hatua nao wanalalamika wakati majangili wanawajua na wanakunywanao kahawa kila siku.

CCM na serikali yake nawasihi acheni unafiki mnaliangamiza Taifa,ufisadi nyinyi,ujangili nyinyi wizi nyinyi kila uchafu nchii hii waanzilishi ni nyinyi na mnajuana na kulindana.

CCM hii inadiriki kuhonga hadi wabunge ili kupindisha haki, mnalaana nyinyi na bado mnadanganya mtaleta mabadiliko ya kweli cjui mnayatoa wapi maana nchi hii mmeongoza na kutawala zaidi ya miaka hamsini na matokeo yake mmezalisha genge la wezi na wanyang'anyi na majangili naomba mungu awalani siku moja muumbuke.
 
Uchaguzi unaofata pigia kura vyama vya upinzani.

Ni hayo tu yanakusumbua? nahisi una mengine moyoni hujaandika ya kibinafsi kwa yaliyokukumba na CCM hii.
 
sema tu unachukia CCM kwa ushahidi upo wa waliokamatwa na kutungua ndege kesi yao ilisikilizwa simiyu wote wale ni wanamagezi.swala la wizi,ujambazi limelenga masirai ya mtu binafsi sio ya chama chochote
 
Msifanye kosa 2020 CCM SOTE TUSEME INATOSHA
Imetosha kufanyaje? Ungetudadavulia kutosha huko ni kupiga tembo kwa kasi, kuiba fedha za miradi na kuzihamishia ughaibuni au mafanikio yapo ccm au kutosha kivipi? Au yatosha kuitwa lofa nawe ukamchekea na kumpa kura ya ndiyo kama zawadi?
 
Back
Top Bottom