CCM na staili ya kumpiga mwizi kimya kimya

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
693
1,199
Habari wadau,

Kwanza nianze na pole kwa ndugu zetu wa upinzani kwani kwani siasa ni sawa na mpira wa miguu yaani kuna kushinda na kufungwa.

Katika chaguzi hizi ndogo naimani kuwa vyama vya upinzani watakua wamepata somo ni njia gani sahihi ya kupambana na mpinzani wao CCM.

Kwenye chaguzi hizi vyama vya upinzani waliingia na sera ya kumponda MTU badala ya kuuza sera zao kwa wananchi.

Nimesikitishwa jamaa mmoja wa upinzani kutwa kucha alikua akimponda RAIS kana kwamba kulikua hamna Sera za maana za kunadi chama chake hivyo kusababisha chama chake kupata kura nane (8) jimbo zima hii ni aibu kubwa.

Nawaomba wapinzani mbadilike kwani wananchi wanahitaji maendeleo sio majungu ya kisiasa mnayo yatumia.

Nilifurahishwa na uzi mmoja ulisema UCHAGUZI MDOGO NDO KIPIMO KWA CCM. huenda aliyeandika uzi huu aliongozwa na itikadi za kichama zaidi kuliko uhalisia.

Imefika kipindi hata wapinzani wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani hii ni hatari na ni ngumu kuja kuiangusha CCM.

Siasa ni sera sio kelele zisizo za msingi.
 
Wanasema wanahitaji Tume huru ya Uchaguzi.
Wanasema Kama Refa na washika vibendera wapo upande wenu ni ngumu sana kushinda.
 
Wanasema wanahitaji Tume huru ya Uchaguzi.
Wanasema Kama Refa na washika vibendera wapo upande wenu ni ngumu sana kushinda.
 
Kuna mbunge mmoja wa upinzani alisema anayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili mara moja. Nafikiri ipo haja ya kuwapima hawa wapinzani akili na Huyu ndiye anayewamaliza
9a97e143182321e80f768a2c0e744f58.jpg
 
Bora mngesambaratisha hiki chama halafu muanzishe kingine nakisiwe na wale jamaa wakule mahala maana wao hubebana waokwawao kila uchaguzi niwalewaletu.
 
hawa bavicha sera zao ni kukariri tuuu kutwa kushinda kwenye mitandao ya jamii kulalamika na wakikutana huku wanajiaminisha kwamba wapo wengi na siku za kupiga kura hawaonekani. mtaisoma namba bavichaaaaa
Wakati wenzao wapo kwenye foleni wao wapo busy na keyboard kwenye viofisi vyao,siju hawa waheshimiwa hata kama wana kazi za kufanya kutwa wapo kwenye mitandao !
 
Kushangilia ushindi wa CCM ni sawa na kupiga punyeto







Kuna mbunge mmoja wa upinzani alisema anayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili mara moja. Nafikiri ipo haja ya kuwapima hawa wapinzani akili na Huyu ndiye anayewamaliza
9a97e143182321e80f768a2c0e744f58.jpg




Kweli nawapongeza wanaccm,ushindi ni wakishindo,ukawa umeaibika na kusambaratika,ni kama pigo la mbwa mwitu nilishuhudia jana wengine machozi yanawatoka .
 
Sio kweli ndg ccm hubebwa na nguvu ya dola.
Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mkoa, na majeshi. Hivyo sio kweli kuwa wanamfukuza mwizi kimyakimya wanapigiwa mayowe na hivyo vyombo
 
Kata moja tu hahahahaha!!!!!duuuh kipigo,siku zote mbwa hupigiwa eneo LA tukio!!!safi sana ccm mnachukiza lakini mnashinda!!!!
 
Wameshikishwa adabu. Pamoja na kelele zote, matusi na kejeli lakini wamefanya ovyo kabisa katika uchaguzi. HUO NDIO UBATIZO WA MOTO.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom