Miongoni mwa mambo ambayo wanasiasa wanayatumia katika kujiweka karibu na watu, kwa kuamini katika falsafa ya siasa ni watu na mwanasiasa ni wafuasi, wanasiasa sehemu mbalimbali wamekuwa wakishughulika zaidi na matukio ya kijamii na yenye kuvuta hisia za wengi. Matukio kama ya misiba, michezo na mahafali n.k
Matukio ya kijamii ambayo yanaambatana na huzuni ama maafa yanawavuta wengi zaidi katika kufariji wahanga na waathirika, wanasiasa wengi na walio makini wanatumia zaidi matukio haya kujijenga na kujiimarisha kisiasa. Tukio kama la mafuriko ya jangwani, mabomu ya gongo la mboto, misiba ya wasanii wakubwa kama kanumba na wengineo yalitumika vyema hasa na wanasiasa kutoka upande wa chama tawala katika kufarijiana na kusaidiana na wahanga na waathirika.
Utaratibu huu ambao wanasiasa wa chama cha mapinduzi wamekuwa nao wa kujiweka karibu na wananchi hasa wakati wa shida zao unawaimarisha na kuwasaidia kujijenga kisiasa, jambo hili ni la msingi kisiasa kwa kuzingatia nature ya jamii yetu na tabia tuliyojijengea kama watanzania wenye itikadi ya ujamaa na kujaliana hasa wakati wa shida.
Nimemuona NAPE kwenye mazishi ya John Stephen Maganga, akiwa kama muwakilishi kutoka chama cha mapinduzi na akapewa platform ya kufikisha salamu za rambirambi kutoka kwa mwenyekiti wa chama chake. Lakini nikiri kuwa sijamuona prominent figure yeyote kutoka chadema kwenye mazishi hayo, na nategemea kuwaona tena viongozi wa CCM Tanga kwenye mazishi ya Msanii wa Filamu Shalo-Milionea na pia naweza nisiwaone viongozi wa chadema wakiwakilisha chama chao, ama CUF ama TLP.
Katika midani ya siasa za sasa na mvutano wa kipinzani baina ya vyama vya siasa, hakuna nguvu wanayoitegemea isipokuwa watu wao, wafuasi. Na wafuasi wanapatikana katika mambo kama haya, mitazamo ya watu wetu inaangalia zaidi ni nani yupo karibu yao hasa katika kipindi cha shida, " a friend in needy, is a friend indeed " waswahili wanasema "rafiki wa kweli ni yule anayekujali wakati wa shida".
"...WAPINZANI KUWENI MARAFIKI WA KWELI KWA WATANZANIA..."