CCM na serikali zake zote zilizopita wameliibia sana taifa

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,233
16,202
Kwanza wabunge wa ccm ni watu waliochanganyikiwa wao hawajui kutafuna bali kutafuniwa
Ndio maana katika marais wote wa chama chao waliopita kila walichokiamua ndani ya ikulu na kukileta bungeni wabunge wa ccm bila kusoma kuchambua ubaya na uzuri wa kitu kilicholetwa wao walipitisha hivyo hivyo kwa madai rais anaelewa kila kitu

Ni uwendawazimu kuamini eti mtu akishakuwa raisi anajua kila kitu wala haitaji kushauriwa
Mwalimu nyerere alisema tuyaache madini yetu ardhini mpaka hapo tutakapopata akili ya namna tunavyoweza kuyatumia kwa maslahi ya wananchi wote wa Tanzania

Lakini mjanja mmoja akiongozana na wabunge wote wa ccm walipitisha sera ya ubinafsishaji ambayo kiuhalisia walioipitisha ambao ni wabunge wa ccm hawakujali kabisa maslahi ya watanzania wala kutaka kujua ni madhara gani taifa litapata kwa kupitisha sera ile bila kuitafakari
Ikaja sheria ya mafuta na gesi nayo ikapitishwa kwa dharura na wabunge wa ccm tena kwa vifijo vya hali ya juu wala hawakujali ni madhara gani tutapata baadae

Leo tunaacha madini yetu yakiendelea kuchimbwa huku tukiibiwa ila wabunge wa ccm hawajaliona wameona mchanga tu tena kwa hisani ya mtu wanaeamini anajua kila kitu rais wao
Sheria walizipitisha wao wenyewe huku maslahi ya taifa yakiachwa na kutazama faida ya mmoja mmoja

Leo ccm wanaibuka tena kikondoo na kuunga mkono mtu wanaeamini ni mzalendo eti kisa ni rais huku wakijisahaulisha kila kitu walikipitisha wao

ACACIA wao wanaamini watamalizana na serikali kwa kuwa wanajua kisheria tena zile zilizopitishwa na wabunge wa ccm na kusainiwa na rais wao haziwezi kuwafanya lolote kwa kuwa zinawabeba

Tunachopata kwenye madini yenyewe achana na hoko kamchanga inasikitisha sana wakati wenyewe wakiondoka na madola bilions sisi hakuna chochote chenye maana tunachopata zaidi ya makombo tu

Waliotufikisha hapa ni wabunge wa ccm na marais wao waliopita leo kuna mtu ana kauchungu ka kinafiki amewaokoteza tena wabunge wale wa ccm kuwa kwenye mchanga tunaibiwa kuliko kwenye migodi yetu na wabunge hao wa ccm wamesimama tena kidete na rais wao wakijidai wakati wa kuibiwa umefika mwisho tena kwenye mchanga na siyo migodini

Wamejisahaulisha yote kwamba haya yote walisababisha wao na sheria walizipitisha wenyewe na inakutia zaidi hasira pale wabunge hao hao wa ccm wanapowaita wabunge wa upinzani ni wezi

Ngoja niishie hapa maana nazidi kupatwa na hasira
 
Watanzania kweli hatujui tatizo ni nini na kwa kukwepa hilo tunatupia lawama ccm,sasa tunalaumu viongozi wa serikali zilizopita wakati viongozi hao hao wa serikali zilizopita ndiyo tulitaka na bado tunataka kuwapa tena nchi baada ya kufanya waliyoyafanya huko ccm.
 
Mkuu sina hata la nyongeza maana kila ulichokisema ni cha maana. Lakini kama mmoja wao kaamua kuuona upupu waliuweka shimoni na sasa tunaukalia sioni ubaya wa kumuunga mkono.

Unafiki wa wabunge haupo CCM peke yake japo huko ndiko ulikotoka, wabunge wote wanatakiwa kualaumiwa pia. Kuna watu walisifiwa sana humu ndani wakati wa sakata la Richmond, EPA, ESCROW, kwanini katika haya masakata wabunge waliungana na kwanini kwasasa hawataki kuungana?

Kwanini waliomshikiniza Mheshimiwa Lowasa kujihuzuru lakini sasa wanamlamu rais kumpumzisha Muhongo?

Swali hilo juu ukilijibu ndiyo utakapoona hakuna wabunge wenye mapenzi ya hii nchi kama baadhi wanavyotaka kuwaamini.

Mnyika alimsema rais kwanini alimchagua Muhongo mwenye kashafa ya ESCROW kuwa waziri lakini anasahau kuwa Chama chake kilitaka kumweka mtu aliyefukuzwa kazi kwa shinikizo la bunge na 100% wa UKAWA kwa ufisadi na kumpendekeza kuwa mgombea wa urais.

Lissu naungana na wengine ni mwanasiasa mzuri lakini hakwepi lawama, yeye kama mwanasheria alitakiwa pia kukipatia chama chake ushauri wa maana badala tu ya kupendekeza watu waliotoka CCM na kutuweka hapa tulipo wawe viongozi wa upinzani.

Hakuna mwanasiasa wa kweli wa Tanzania ukimuondoa Mtikila, James Mapalala, Nyerere, Fundikira japo walikua na mapungufu lakini hawakua kama hawa tulio nao.
 
Na viongozi wengine wapo upinzani sijui na hao wanawasemaje.
 
Ni kweli lakini mambo ya ndani ya vyama tuyaache lakini linapokuja swala la Taifa bila kujali wingi wa watu wa vyama fulani tuweke maslahi ya watanzania maskini mbele nani wa kuwatoa hapa kuwapeleka mbele kama si hawa wanasiasa wetu?

Lakini unapomwona mwanasiasa anajali maslahi ya chama chake kuliko maslahi ya taifa ni wa kuangamizwa

Mikataba mibovu isiyojali maslahi ya wananchi maskini wa Tanzania ccm ndio tatizo kubwa sana kama wangekuwa makini na kujali maslahi ya taifa tungekuwa mbali mno kuliko hapa tulipo
Tatizo kubwa wanatumia wingi wao kufanya chochote wakitakacho
 
Na viongozi wengine wapo upinzani sijui na hao wanawasemaje.
Kwa nini hawashtakiwi washtakiwa kama kuna ushahidi wa kutosha
Ndio maana nasema wabunge wa ccm enzi za mkapa na Kikwete ni wanafiki wakubwa
Hawa wabunge wapya ambao hawana hata miaka 5 sina shida nao
 
kessy kesha sema wanyongwe wana ccm wote hasa wabunge waliopitisha mikataba fake
 
Wataendelea kuiba na kuiba na kuiba bila ya haya wala soni huku wakizidi kulitia taifa hasara na kuwaongezea raia lindi la umaskini
 
Ni kweli lakini mambo ya ndani ya vyama tuyaache lakini linapokuja swala la Taifa bila kujali wingi wa watu wa vyama fulani tuweke maslahi ya watanzania maskini mbele nani wa kuwatoa hapa kuwapeleka mbele kama si hawa wanasiasa wetu?

Lakini unapomwona mwanasiasa anajali maslahi ya chama chake kuliko maslahi ya taifa ni wa kuangamizwa

Mikataba mibovu isiyojali maslahi ya wananchi maskini wa Tanzania ccm ndio tatizo kubwa sana kama wangekuwa makini na kujali maslahi ya taifa tungekuwa mbali mno kuliko hapa tulipo
Tatizo kubwa wanatumia wingi wao kufanya chochote wakitakacho
Mkuu umesema kweli. Big up mleta mada.
Bwn yesu amasema Mafarisayo (MACCM) ni wanafiki wanachuja mbuu wanameza mgamia.
Wanashangilia kuzuia mchanga huku dhahabu yote inachuliwa bure kwa mikataba mibovu!!
Kina Nyika wakisema ukweli wanafurushwa nje ya Bunge!!
 
Hakuna kiongozi wa fisiem aliye upinzani
Jaribu kuamka kama upo kitandani. Upinzani mpaka waanzilishi wake wengi ni FISIEM kama una umri wa miaka 18 hujui lini upinzani ulianza. Mtei mkwe wa Mbowe alikua waziri wa Fedha, Lowasa alikua waziri mkuu, sumaye alikua waziri mkuu. Sasa kama unawasema CCM kwa makosa ya nyuma usisite kuwataja mpaka waliokimbilia upinzani.

Kwani jambazi akitoroka jela Kenya akija Tanzania anakua siyo jambazi????

Jaribuni kuacha upuuzi wa kupenda vyama mpaka mnauza utu na ufahamu wenu. ndiyo maana kuna kitu kinaitwa intelpol
 
Back
Top Bottom