Ccm na serikali yenu kujisifia siyo kazi yenu bali ni ya wananchi wenyewe.


N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Messages
2,602
Likes
10
Points
0
N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2013
2,602 10 0
Nawashangaa kuwaona wanaccm,ccm na serikali yake wakitamba majukwaani kuwa wameleta maendeleo.Kutamba majukwaani/kujisifia sio kazi yenu wanaccm.Hii ni kazi ya wananchi wenyewe.Mfano,mtu anafanya biashara ya duka,anayetakiwa kusifia ni mnunuzi wa bidhaa au muuzaji wa bidhaa? Bila shaka ni mnunuzi kwa ndio mwenye kujua ubora na uzuri wa bidhaa hiyo,na sio muuzaji.Kwa hiyo mnunuzi ndiyo mwenye kusifia sio muuzaji.CCM mmpooooo!!
Mazuri mliyoyafanya sio kazi yenu kujisifia,wananchi ndio wahusika wakuu kama kazi yenu inakubalika watawasifia wao sio ninyi mjisifie.
Wananchi ndiyo wanapima maendeleo yenu kwani wao ndiyo walengwa wa maendeleo,kazi yenu ni kutekeleza wajibu.Halafu kujisifia wakati huo ni wajibu wenu kufanya hivyo,na mnalipwa mishahara mkitimiza majukumu yenu,hii haikubaliki.
Kikubwa tekelezeni wajibu wenu,wananchi ndiyo watawasifia.Pale mnapofanya ovyo wananchi watawapinga,watawakosoa na kuwaonya,lakini mtakapofanya vizuri wananchi watawapongeza,watawasifia na kuwapa moyo.Sifa mara nyingi huambatana na maovu,mbona mmekuwa wepesi kujisifia tu lakini hamuyasemi madhaifu yenu? Nyinyi ni binadamu kama binadamu wengine,lazima mapungufu na maovu yenu yapo.Kwa hiyo,kukaa tu na kujisifia wakati siyo kazi yenu hatuwaelewi!!
Pia,kujisifia kwenu hakuendani kiwango cha utekelezaji wa ilani yenu,kwamba ni kwa kiwango gani mmetekeleza ilani yenu,kama ni 0.0005% si mseme? Sio tu kukaa na kujisifia bila facts.
Maoni yangu.
 
Kasimba G

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
2,887
Likes
1,022
Points
280
Kasimba G

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
2,887 1,022 280
Wanafuata sera za utandawa, manaake sikuhizi unaweza kujitangaza mitandaoni kuwa wewe ni mzuri, mrefu, lakini reality kinakuwa kitu tofauti na kioja!
 
N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Messages
2,602
Likes
10
Points
0
N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2013
2,602 10 0
Wanafuata sera za utandawa, manaake sikuhizi unaweza kujitangaza mitandaoni kuwa wewe ni mzuri, mrefu, lakini reality kinakuwa kitu tofauti na kioja!
basi sioni tofauti na watu wanaojiuza mitaani.
 

Forum statistics

Threads 1,274,530
Members 490,721
Posts 30,515,416