Ccm na serikali yake vimesimamaje machoni mwa raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm na serikali yake vimesimamaje machoni mwa raia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Byendangwero, Dec 25, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hili serikali iweze kuongoza vizuri inahitaji kuwa na wengi wa raia wake nyuma yake. Hivi sasa kila kona ya nchi hii kunasikika vilio vingi vikiilalamikia serikali iliyoko madarakani na chama kilichoiweka pale. Hali hiyo inajenga hisia kwamba, uenda umaarufu wa chama hicho tawala na serikali yake, umeporomoka kiasi cha kushindwa kuongoza nchi bila ya msaada wa vyombo vya dola gandamizi. Kutokana na unyeti wa suala hilo, pengine hivi sasa ni wakati muafaka kwa REDET na Synovate kulifanyia utafiti na kutoa ushauri unaostahili kwa serikali.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Synovate? REDET? Hawawezi kufanya utafiti huo hata siku moja, read my words! Watafanya utafiti wa serikali kupendwa na si vilio vya wananchi!
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kama kuna chama chenye nafasi ku-turn things around machoni mwa watanzania CCM ndio wana nafasi hiyo.
  Wao wanasema wameshika mpini kwa maneno ya Topical. Wao ndio wako kwenye sukani.
  Kinachowapasa ni kuifanya serikali kuwa functional sio kama ilivyo sasa.

  Kwa mfano, Hivi sasa serikali ina askari polisi wa kuvunja migomo, maandamano ya wanafunzi badala ya kutatua matatizo ya wanafunzi hao.
  Serikali ina polisi wengi wa kuzuia mikutano ya upinzani lakini hawana polisi wachache wa kulinda mikutano hiyo.

  Serikali inavunja mkataba ambao matokeo yake ni kuilipa kampuni waliyovunja nao mkataba mabilioni ya fedha, badala ya kutatua tatizo la Tanesco. Kuna mapendekezo ya kitaalamu yametolewa humu JF na Mtanganyika kwenye thread ya CHADEMA kuandamana kupinga kupanda bei ya umeme. Hii ni mifani michache tu.

  Hawawezi kuendelea kumuomba mlalahoi akaze mkanda wakati wao wanatanua tu.

  Sijui nani ni mshauri wa CCM na serikali yake lakini between now hadi 2015 wanaweza kuchapa kazi kama wako makini na 2015 wananchi watakipigia kura na kubakia madarakani bila ya kuchakachua. Wana ujasiri huo?

  Kuna mama mmoja alishasema kuwa katika CCM hakuna msafi, lakini watanzania hawahitaji malaika , wanachohitaji ni mzalendo mwenye uchungu na nchi na rasilimali zake kwa manufaa ya wote.

  Nini wafanye.?
  Washughulikie wala rushwa vigogo sio vidagaa tu.
  Wapige vita ufisadi kwa vitendo sio domo tupu majukwaani.
  Wapeleke huduma za jamii vijijini.
  Serikali iache matumizi ya anasa kama ununuzi wa VX
  Wakati huo huo walete Katiba mpya

  Rais Kikwete anaweza kuibuka "a hero" at the end of his term.

  Siku nyengine nitatoa ushauri wangu vipi wanaweza kupiga vita rushwa, vipi wanaweza kushughulikia fisadis hata kama viongozi ni miongoni mwao. I will suggest a very human way, isiyo ya kukomoa ,wala kulipa visasi and very practical.
  Ninaiandaa. Kwa hiyo CCM wasome JF wapate Ideas.

  Sisi wengine ni raia wema si washabiki wa chama chochote cha siasa na tunaitakia mema nchi yetu. Lakini right now tunaona kama nchi imepoteza muelekeo.
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukweli Unabaki Palepale. Fever ya Siasa Inatokana na Filings za Wananchi Kuanzia Hali ya Maisha Yao kwa Sasa na Matokeo ya Uchaguzi. Leo Hii Tukianza Kukusanya Maoni ya Wananchi Juu ya Nchi Yao Watakuambia Wamechoka na CCM na Hawana Matumaini na Uongozi wa JK Kutatua Matatizo ya Nchi. Kitu CCM Wanaendelea Kuharibu ni Denial of Truth Kwamba Wameshindwa Kutatua Matatizo ya Tanzania. Kitu cha Kufanya Sisi Wananchi ni Kuhakikisha Tunapata Katiba na Kutimua CCM Kabla ya 2015.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CCM katu haiwezi kujisafisha. Kikwete is so dirty kwamba kwake kuwa hero at the end of his term ni ndoto ya mchana. Jinsi CCM inavyodidimia ndivyo inavyodidimiza nchi. Njia pekee iliyobaki ni kuwatupa nje. Watanzania wameshaamka. Ndio maana Kikwete alipata kura halali asilimia 27% tu.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Suala la kujisafisha linakujaje, wakati kwa maoni ya wengi ccm hivi sasa imetekwa nyara na mafisadi papa, pamoja na waarifu wa aina zote; wauza unga, majambazi, wanyang'anyi, n.k ambao wamekigeuza chama hicho kuwa kichaka cha uarifu wa kila aina. Kwahiyo matumaini pekee kwa ccm kuweza kujisafishani kwa wanachama wa kawaida kuamka katika usingizi totolo waliomo, na kuwapiga buti katika uchaguzi mkuu ujao, wale wote walio sababisha chama hicho kipotea njia.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Watanzania walipawa tips za kanga, vitambaa vya kichwa, kapelo, tshirt na pesa kidogo za kununua shahada. Wasubiri miaka mingine minne wakiwa katika maumivu.
   
 8. m

  mzambia JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kawaida watz ni wasahaulifu kama alivyosema makamba mtasahau tu na tutapita kwa kishindo 2015
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona mtasahau tu kama mlivyosahau ishu ya epa maana mnakomaa na dowans na kuchakachua kura tu, bado meremeta, kagoda, tangold etc.
   
Loading...