Uchaguzi 2020 CCM na Serikali yake tulikosea. Kwa hili lazima Lissu atupige bao

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
Kati ya makosa yaliyofanywa na Serikali yangu ya CCM ni kushindwa kutoa ajira kwa vijana na kuacha wazagae mitaani bila kazi.

Ni kosa kubwa sana kwa sababu vijana hawa ni bomu tulojitegea wenyewe kutumaliza.

Maelfu ya vijana wanaojitokeza kwa wingi kwenye hadhara za bw. Tundu Antipas Lissu ni sababu yetu sisi.

Kwa miaka minne tumewatelekeza mitaani kama kuku wa videri; tumeua future zao; tumewaua kisaikolojia; tumewatoa kwenye reli hadi baadhi wamekata tamaa wameamua kuwa walevi wa gongo na wavuta bangi.

Uchaguzi umefika tutawaeleza nini hawa vijana watuelewe na watuchague?

Tutawashawishi vipi wazazi wao waliowasomesha kwa shida ili watuamini na watuchague?

Tutawambia tumenunua ndege?

Tutawambia tunajenga SGR?

Tutawambia tunajenga daraja la Busisi?

Tutawambia tumejenga flyover?

Wana CCM wenzangu; 'maendeleo ya vitu bila kuboresha maendeleo ya watu ni sawa na kazi bure'

Kwakuwa tumelikoroga kwa miaka minne sasa muda wa kulinywa umewadia.
 
Hakuna namna itabidi tuwaeleze ukweli tu kuwa tumewajengea fulaiova sijiara sitigilaji goji na pia tumewanunulia dilimulaina,kwa vyovyote vile watafurahi sana na kura zote kwa jiwe and company, hahaaa.
 
Sote tulitamani kuwa na flat screen zilipoingia. Na wengine sasa wana UHD Ultra slim. Lakini baada ya muda mchache tu wa kuwa nayo unaiona sio lolote si chochote.

Hata kwa wenye ndoto za kumiliki nyumba, baada ya kumiliki nyumba unajiona kama bado huja achieve kitu kikubwa na hata kama ukipata gari bado unaona kawaida tu. Baadhi ya wakaazi wa Dar wanaona maji ya bomba si lolote si chochote wakati wenzetu vijijini kila baafa ya miaka 5 ndio kilio chao kwenye kampeni.

Ninachojaribu kusema ni kuwa hizo ndege, flyovers na SGR mwisho wa siku tutaona ya kawaida sana tu. Hayo hayatofanya vijana wasidai ajira na wananchi uhuru wao wa kikatiba.

The same ukinunuwa gari mpya nyumbani, watoto hawasiti kukudai nguo za Xmass ama kwenda out siku za weekends. Anayofanya Magu are neither wonders nor miracles. Isiwe sababu ya kumuabudu. He is, in fact, far below.par!
 
Vijana walidekezwa sana..eti kila akimaliza chuo anasubiri post,ulikuwa upotevu mkubwa wa hela..vijana wakawa wanaishia maofisini tu,,nani akalime sasa?
Ukilima wewe inatosha. hatuwezi kuwa na nchi ya wakulima watupu; tunahitaji wataalamu wa kutosha katika utumishi kama madaktari wawepo wa kutosha kwenye mahospitali wakitoa huduma kwa raia; pawepo walimu wa kutosha wa kutufundishia watoto wetu shuleni
 
Madaktari wanatosha,,tiba za asili si zipo,,kwa mfano huku geita,hatuhusudu sana mambo ya hospitali,wakati waganga wapo wa kutosha,
Walimu nao wameshatosha,hakuna sababu ya kupoteza pesa kuajiri wengine,
Mafundi wa mabarabara,tutaweka kampuni za kichina au uturuki watafanya kazi
 
Unasubiriwa na fikra za kizamani Mungu akusaidie angalau upate akili kidogo uondokane na ujinga ulojaza kichwani
 
Kati ya makosa yaliyofanywa na Serikali yangu ya CCM ni kushindwa kutoa ajira kwa vijana na kuacha wazagae mitaani bila kazi.

Ni kosa kubwa sana kwa sababu vijana hawa ni bomu tulojitegea wenyewe kutumaliza.

Maelfu ya vijana wanaojitokeza kwa wingi kwenye hadhara za bw. Tundu Antipas Lissu ni sababu yetu sisi.

Kwa miaka minne tumewatelekeza mitaani kama kuku wa videri; tumeua future zao; tumewaua kisaikolojia; tumewatoa kwenye reli hadi baadhi wamekata tamaa wameamua kuwa walevi wa gongo na wavuta bangi.

Uchaguzi umefika tutawaeleza nini hawa vijana watuelewe na watuchague?

Tutawashawishi vipi wazazi wao waliowasomesha kwa shida ili watuamini na watuchague?

Tutawambia tumenunua ndege?

Tutawambia tunajenga SGR?

Tutawambia tunajenga daraja la Busisi?

Tutawambia tumejenga flyover?

Wana CCM wenzangu; 'maendeleo ya vitu bila kuboresha maendeleo ya watu ni sawa na kazi bure'

Kwakuwa tumelikoroga kwa miaka minne sasa muda wa kulinywa umewadia.
Hata Ulaya na USA ajira ni tatizo ndugu
Vijana wanaojielewa wamaejiajiri!
Na siyo wote kwenye mikusanyiko ya Lisu hawana ajira!
Na siyo wote waliokusanyika watampigia kura Lisu!
Subiri Oct ndiyo utaijua siasa
 
Back
Top Bottom