CCM na Serikali yake acheni kusifiana kwani wananchi hawaoni mnachofanya

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Yafuatayo ni mabaya yenu ambayo mmeitumbukiza NCHI kwenye Giza Nene

1. Mikataba mibovu kuanzia Mali asili mfano madini na vitalu vya uwindaji bila kusahau gesi ya mtwara

2. Wizi wa Mali za umma hakuna ubishi kuwa nyie wenyewe ndoo wezi kwani tangu tumepata uhuru nyie ndiyo mnaongoza NCHI kashifa mbalimbali zinatokana na uongozi wenu mbovu.

3. Sheria mbovu ambazo mmetunga wenyewe Kwa ajiri ya kuwalinda wenyewe ndiyo zimetufikisha hapa kwani hata kashifa Iptl Hadi Sasa tuliona waliokamatwa pamoja na kukamatwa wahusika wakuu waliachwa na kesi ikapigwa nolle'.

4. Kila kukicha mnabadili mitaala ya elimu hamjui mnadira Gani KATIKA NCHI. Mzee mungai alifuta SoMo la kilimo lakini ndoo kinatufanya tuishi ingawa Somo hilo halipo.

Kwa hayo machache mnafaa kuendelea kuongoza nchi? Au mnataka watu watumie njia mbadala kudai uhuru wao.

Aidha nasema hivo kwasababu CCM ni kikundi kidogo Cha watu kinakula fedha za umma bila kuwafanyia maendeleo Huku kundi hilo likipumbaza umma Tanzania ni masikini. Wakati madini tunayo gesi tunayo mito tunayo maziwa tunayo mbuga tunazo n.k.
 
Back
Top Bottom