CCM na serikali ya Magufuli wanaiogopa CHADEMA kuliko Corona. Wana vyombo kulinda wanasiasa kuliko walipa kodi na afya zao

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,349
2,000
Ukiskia press ya polepole, press ya Magufuli, press ya Sabaya mikusanyiko wanayoikataza ni ya siasa pekeee na hasa ya Chadema.

Ndio maana Lema katumiwa askari zaidi ya 20, na bunduki za kutosha kama wanasaka jambazi sugu. lakini Lema ana simu, kwanini hawampigii?

Naona airport na mipaka na tuna gun za kupima joto pekee na sampuli lazima iende Dar, yaani tuna maabara moja nchi nzima ya kupima corona.

Serikali hii ina vyombo vya kisasa kulinda wanasiasa kuliko kulinda afya za walipa kodi.

Madukani hakuna mask na ukizipa box ya mask iliyokuwa ikiuzwa shs 7,000 kwa sasa inauzwa 150,000
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
1,927
2,000
Chama cha corona (chadema) mmechukia sana wananchi kutahadharishwa kuhusu hilo gonjwa, nia yenu sio njema kwa wananchi
 

infinix

JF-Expert Member
Sep 6, 2018
1,594
2,000
Huu ni ushahidi kwamba, waafrika tuko nyuma sana kifikra, kimtazamo na hata namna zetu za kufikiria.

Siku zote wanawaza namna ya kuzidi kuwa madarakani na hawafikiri juu ya majanga mabaya mfano corona, kwamba siyo tu maabara, lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia watu wasitoke nje ya nchi, na wale waliopo huko wabaki huko kwanza mpaka janga hili litakapokwisha.

Sasa janga limekwishaingja, sasa tufanyeje??

Hatuoni na wala hatusikii mpango mkakati wa kupambana na hili janga ili kusudi tusipokee tena wagonjwa wapya.

Lkn ukiuliza kuna mpango gani wa kupambana na chadema, utashangaa, kumbe wajinga hawa wana mpango mpaka wa miaka mitano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mr Big

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
478
1,000
Kila siku siasa hamna vitu vya msingi vya kuongea?
Kila mara mada za vyama hata cent tano hampokei kutoka kwao
Kaeni chini mfikilie mada za kusaidia jamii sio kupondana ovyo..
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Top Bottom