CCM na Serikali wengi wanasikiliza, kusoma na kufuatilia akaunti za wapinzani na activists kuliko akaunti zao

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hakuna akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii inayomilikiwa na serikali, Wana CCM na Watumishi wa serikali ambayo ipo active kwenye mijadala na inayopata usomaji na uchanguaji wenye afya.

Wakati huo huo tunaambiwa wananchi wengi na watu wengi walioelimika na kuwa na uwezo wa kifedha wapo serikalini na kwenye chama Tawala. Upinzani na activists hawazidi elfu moja waliopo active mitandaoni.

Kama tunatafuta tatizo lilipo Kwanza tujiulize, Wana CCM na Watumishi wengine watiifu kwa serikali simu zao za smartphone wanazitumia kufanya nini Kama awawezi kuibua na kuchangia mijadala kwenye akaunti za Chama na serikali?

Lakini pia tatizo lianza na viongozi wakuu wa nchi, Mawaziri ,viongozi wa chama na viongozi wa dola. Hakuna sehemu utawwkuta wamekaa wawili au watatu wasijadili hoja zinazojadiliwa kwenye akaunts za wapinzani na activists, hii maana yake Mawaziri, wakuu wa Mikoa, wakuu wa taasisi mbalimbali wameinstal au wanaperuzi akaunti za wapinzani kuliko wanavyoperuzi akaunti za wizara, idara na chama.

Nini matokeo yake, upo uwezekano mkubwa wapo Mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya, wakuu wa idara na vitengo, wakuu wa chama Tawala wanaikosoa serikali kutokana na wao wenyewe kukosa imani nayo.

Ndugu zangu, Kama ninaichukia ACT na sipendezwi na sera zake siwezi kwenda kukaa natafuta na kusoma akaunti zao. Hii ni Hali yakibinadamu kabisa kwamba ukikichukia kitu hauwezi kukipa umaarufu. Hawa viongozi wanakwenda kwenye akaunti za upinzani kwa sababu wanazipenda na wanaamini kinachopatikana huko ndicho sahihi.

Leo unamsikia Waziri anajadili space means yeye mwenyewe anaingia huko kwa ID anayojua yeye na inawezekana anachangia mada kwa sauti zakupikwa. Tusiamini Sana waliopo serikalini kwamba niwaadilifu, binadamu nimwadilifu pale penye haki lakini hakuna namna unaweza mlazimisha aamini kisicho cha haki.

Mawaziri walazimishe kuanzisha space akaunti watu wajadili maendeleo ya sekta zao tuone kama space za akina maria zitapata wafuasi wengi, mkiruhusu Uhuru wakutoa maoni hata hao akina Tundulisu na Lema watajoin space zenu na mtajibizana kwa hoja.

Vinginevyo waziri atuambie Taarifa za space anazipata wapi? Lazima anajoin anasikiliza na hivyo ndivyo Dunia ilivyo. Kiongozi lazima ujue nchi inavyokwenda, lakini kosa la Mawaziri wengi baada yakubaini mbinu mpya inayotumika awatafuti nikwanini inatumika wanakimbilia kufungia. Mkifunga watu wanahamia upande mwingine na tatizo linabaki palepale.

Juzi tunamwona Kigwangala anajiweka karibu na Kigogo na wanashirikiana, unajiuliza huyu Waziri mstaafishwa anashirikianaje na mtu aliyeleta damage kubwa kwenye awamu iliyopita? Lakini kwa reasonable person unabaini hatukuwa tunapambana na Kigogo tulikuwa tunapambana na matendo yake. Leo hii Kigogo kakimbiwa na watu wote, kwa sababu Hana taarifa za kweli, akiwa na taarifa za ukweli atapata wafuasi tu. Na hapa Kuna somo, Kama Kigogo Leo Hana taarifa, je aliyekuwa anatoa taarifa hawezi kuwa alikuwa ndani ya watu wa karibu wa awamu iliyopita na Sasa ametolewa ndo maana habari hazivuji? Kama ndivyo, kwanini tusiamini kwamba wanaotoa boko kwenye space na akaunti nyingine wapo ofisini kwenu na wanakerwa na mnayoyafanya? Msipambane n watu pambaneni na hoja waatu awajawahi kuisha mtawaacha.
 
NENO LA UKWELI SIYO ZURI NA NENO ZURI HALINA UKWELI NDANI YAKE..../

GOOD MESSAGE ,AND NICE CHOICE AT RIGHT TIME.
 
Shida ya kujaza chama kimoja bungeni ndio hii, wao wenyewe wanatamani kujua Twitter Spaces wanajadili nini
 
Wanajua fika hawana ushawishi kwa wananchi, hivyo wanafuatilia wanachoongea wapinzani na wanaharakati ili kuona kwanini wana mvuto kuliko wao. Wamedhibiti redio, TV na magazeti wakidhani wakibaki wanasifiwa watapata mvuto. Matokeo yake TV, magazeti nk yamepoteza mvuto, na sasa wanafuatilia space maana wanajua mvuto umehamia huko. Hayo ndio madhara ya kutawala kwa mabavu bila ridhaa ya watu.
 
Back
Top Bottom