CCM na serikali mnamlaumu Lissu, lakini ukweli udhaifu na makosa ya Rais Magufuli ni mengi mno, na yako dhahiri

Timm Wu

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
506
1,000
Rais Magufuli ana nafasi ya kusafisha the dark side of his administration kama ambavyo ameanza hivi karibuni kuwakemea wakuu wa wilaya baada ya miaka mitatu ya ukora wa waziwazi pamoja na kuwataka TRA wawe na staha wanapokusanya kodi kwa wafanyabiashara - baada ya miaka mitatu ya kuua biashara za watu na kuwafilisi - huku yeye mwenyewe Rais akiwaita majizi, mashetani na kila aina ya jina baya...

Lakini bado Makosa ya kiuongozi ya Ndugu Magufuli ni mengi mno, na yako dhahiri mno - mengi yakifanyika kwa maelekezo yake mwenyewe, ama akiyasimamia mwenyewe...

Sasa mimi huwa sielewi ataepukaje na yeye kupata SULUBA anazowapa wenzake mara baada ya kumaliza muda wake wa Uongozi - whether kiongozi atakayefuatia awe anatokea upinzani ama CCM kwenyewe - nahisi huyu ndugu atapata tabu sana na mimi huwa natokwa machozi kila nikimfikiria maisha yake baada ya zamu yake Ikulu maana namwonea sana huruma...

Yan makosa ni mengi mno, mengi ya kujitakia...

Angalia alivovuruga zao la korosho..

Angalia alivovuruga Bunge...

Angalia alivovuruga Mahakama...

Angalia anavotaka kuiua hifadhi ya Selous...

Angalia anavolitumia jeshi la Polisi kunyanyasa raia na bado anatamka hadharani kwamba polisi wanaoua raia wasichukuliwe hatua zozote za kisheria - hivi haya si ni makosa ya dhahiri ya kiuongozi, Lissu analaumiwaje? Kosa lake ni kuyakemea?

Naamini Magufuli akimaliza muda wake ataiacha hazina haina hata sh.100....kwa hiyo hivi kuna mtu honestly anafikiri madai ya upotevu wa trilioni 2.4 yatapita hivi hivi bila kuhojiwa? Iwe CCM ama Upinzani, Magufuli will have to explain this thoroughly...tabia ya kutembea na mabulungutu ya hela cash na kugawa hovyo hovyo kwa watu wake naamini haitapita hivi hivi bila mtu kupata taabu kidogo...akiambiwa hii tabia si nzuri, mnakimbilia kudai Lissu anamchafua...kwanini asijirekebishe?

AU, SADC na mashirika mengine ya kikanda yanajulikana kuwa upande wa Marais wanaovuruga nchi zao nyakati za chaguzi - sasa tunaye Rais asiyejulikana AU ama SADC ama popote pale - sasa huyu tuseme mwaka 2020 akafanya figisu kwenye uchaguzi ujao kama inavyotarajiwa kwamba atafanya, mtetezi wake atakuwa nani? Hivi AU ama SADC watahangaika kumlinda mtu aliyejifungia chumbani kwake na kuwadharau? Hili ni kosa kubwa sana kufanywa na Rais wetu, atapata tabu sana - akina Mahiga hawajamshauri vizuri.

Bado ana nafasi ya kujirekebisha na kuponya vidonda na majeraha aliyowapa watu, AKITAKA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom