CCM na Serikali imewaaminisha wananchi wizi kuwa halali katika mambo yafuatayo

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,855
- Wanafunzi wa form 6 kulipia mtihani kwa gharama kubwa ya elf 50

- Maji kuuziwa unit 1 kwa Bei ya kuanzia 800- 1200

- Wajawazito kununua vifaa vya kujifungulia

- Kulipia gharama za kununua kiwanja cha makazi au shamba kwa mwenyekiti wa mtaa/ kitongoji

- Kusajili shule au taasisi lazima ulipie gharama kubwa kana kwamba Watumishi wale hawalipwi mishahara

- Mihuri ya mahakama kulipiwa na wananchi pale wanapokuwa na shida kama vile wanafunzi/ ukipoteza laini ama kiapo fulani

- kuuziwa mchanga/ mawe ya kujengea ambayo yanatolewa milimani kwa gharama kubwa alikhari Ni miongoni mwa Mali za wananchi, Serikali haisimamii Bei maalum

- Vifurushi vya mitandao ya simu kuuzwa kwa Bei kubwa, mfano, Tsh. 500 mtu anapewa dk 30 tu 😂😂 masaa 24? Serikali ipo kimya

Hayo Ni baadhi tu, wananchi walishazoea nakuona Kama Ni Mambo ya kawaida maishani mwao.
 
Hapo kwa simu kwakweli sielewagi na ilhali tuliambiwa mkongo wa taifa ukikamilika gharama za simu na internet zitakuwa sawa na bure.
 
Hapo kwa simu kwakweli sielewagi na ilhali tuliambiwa mkongo wa taifa ukikamilika gharama za simu na internet zitakuwa sawa na bure.
Haya Mambo sijui kwanini huwa hayaongelewi Sana kwenye kampeni?
 
Kwa hiyo mliataka nani agharamia? au ndio pesa za msaada?....kwani nani kaibiwa?...hizo huduma hao wanatoa hawalipwi mishahara na increment jee zitatoka wapi? Toeni Utopolo hapa.
 
Back
Top Bottom