Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 299
- 58
Posted Date::3/8/2008
Mtoto wa Komandoo Salmin aburuzwa kortini
Na Tausi Ally
MTOTO wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salmin Amour, Amin Amour (36), amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka ya kula njama na kujipatia dola za 6,000 za Marekani kwa njia ya unganyifu.
Ilidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Rose Kangwa kuwa, Februari mwaka huu mshtakiwa huyo, Munir Juma (35) na wenzao wawili ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya kujipatia fedha hizo kwa Baosheng Ge baada ya kumdanganya kuwa wana nyumba kwenye kiwanja namba
MKC/MCA 1207 uko Mikocheni ambayo wangempangisha wakati wakijua kuwa si kweli.
Ilidaiwa kuwa, washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho, Februari Mosi, majira ya saa 10:30 jioni katika maeneo hayo ya Mikocheni
Washitakiwa walikana mashtaka na upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu Kangwa aliamuru washitakiwa hao warudishwe rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana . Kesi hiyo, itatajwa tena Machi 19.