Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Ukweli ndio huo, labda kwa mtu asiye na uwezo wa kufikiri ndio hataona kwamba CCM na Magufuli wanataumia ajali ya moto Morogoro kama mtaji wa kisiasa.
Hatukatai kwamba wakati wa hili janga na msiba, labda si vema kuanza kuhukumiana, kama alivyosema Rais Magufuli, japo haina maana baada ya msiba kusiwepo kabisa kuhukumiana. Lakini sasa Rais Magufuli mwenyewe na CCM si kwamba tu hawahukumu, bali wanaenda mbali zaidi kwa kutumia tukio hili kama mtaji wa kisiasa, kujiuza kwa wananchi kisiasa.
Hawa watu waliokufa wakiiba mafuta kwenye ajali wote tunajua ni wahalilifu, vibaka. Tunachoona sasa ni kwamba wamegeuzwa kuwa mashujaa wa namna fulani. Majushaa wa kuiba kwenye tukio la ajali?
Zaidi ya zawadi za maelfu ya pesa yakitangazwa live na vyombo vya habari, kuambiwa serikali itagharamia matibabu (yaani mimi mlipa kodi nigharamie matibabu ya vibaka wa mafuta) sasa tunaambiwa wajajengewa mnara wa kumbukumbu!
MImi kama mlipa kodi wa Tanzania, sitaki hela yangu ya kodi itolewe kama zawadi kwa mhalifu, wala imjengee mhalifu mnara wa kumbukumbu. Labda kwa huruma inaweza kugharamia mazishi, kwa kuwa mhalifu aliyekufa hawezi kujizika.
Hivi tangu lini mhalifu amekuwa akitukuzwa kiasi hicho? Tangu lini Tanzania limewkuwa taifa la kutukuza uhalifu? Hivi CCM wamekuwa desparate kujiuza hadi kufikia kiasi hiki? Au CCM na Raisi Magufuli wanaona kuwa wao ndio kisababishi cha hali mbaya ya mzunguko wa fedha nchini kiasi kuwafanya watu kufanya chochote kujipatia fedha kidogo?
Binafsi wala hata sikuona haja ya raisi Magufuli kuwatembelea hawa watu hospitali na kufanya matangazo mengi ya kutoa msaaada wa fedha huku akitaja kiasi wanachopewa. Na wala sioni haja ya kuwajengea mnara wa kumbukumbu. Na kama ikibidi kujenga huo mnara, basi tuandike maandishi "hapa wamezikwa watu waliokuwa wakiiba mafuta baada ya ajali ya lori. Tujifunze ili tukio kama hili lisije tokea tena.
Sikatai kutoa maneno ya pole kwa wafiwa, lakini jambo la ajabu ni kuona Magufuli na CCM yake wakienda mbali zaidi na kulifanya tukio hili kuwa mtaji wa kisiasa. Hili ni tukio la kihalifu, kwa kiyo serikali na Raisi Magufuli walipaswa watende kwa umakini wakijua hilo, sio kulitumia kujijengea umaarufu wa kisiasa. Hivi mmefikia kuwa desparate kiasi hicho katika kujaribu kufanywa mpendwe na wananchi? CCM kimekuwa chama kibaya cha kujitembeza?
Ajali nyingi sana zimetokea nchini na kuua watu wasio na hatia. Ni mara ngapi umesikia Raisi Magufuli akitembelea majeruhi wa ajali hizo na kuwapa maelefu ya fedha au kuwajengea mnara wa kumbukumbu au ajali hizo kufanywa tukio la kitaifa? Kwa nini hii ya wahalifu hawa ionwe tofauti - au kwa kuwa inakuja tukielekea uchaguzi Mkuu kukiwa na tetesi kwamba serikali ya Magufuli inazidi kuporomoka katika umaarufu na kuwa katika uchaguzi wa haki hataweza kushinda?
NB: Kwa tukio kama hili Raisi Magufuli alipaswa kufanya yafuatayo badala ya kulitumia tukio kisiasa
Raisi angetoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kuwapa pole wafiwa. Angetamka kwamba serikali itagharamia mazishi ya waliokufa ikiwa hawatatambuliwa na ndugu zao, na kugharamia matibabu kwa majeruhi.
Na pia angekumbusha Watanzania kwa ujumla kwamba wajiepushe na kujichukulia mali pale ambapo ajali zinapotokea, iwe gari binafsi au ya mizigo, kwa kuwa kufanya hivyo sio tu sio ubinadamu bali pia ni kitendo cha uhalifu na wanaofanya hivyo wakikamatwa watachukuliwa hatua kali.
Basi, hiyo ingetosha kabisa. Hakuna kutembelea hospitali na kutangaza "nakugawia laki tano ukanunue juice", hakuna kutangaza kujenga mnara wa kumbukumbu, hakuna la zaidi. Kwa kuwa wengi waliopatwa na janga hili kimsingi ni wahalifu.
La sivyo tutarajie siku moja Raisi Magufuli akitembelea majambazi waliojeruhiwa na polisi kwa risasi wakiwa wamelazwa hospitali na kuwapa pole na zawadi za fedha, kwa kuwa anajali sana utu.