Ccm Na Propaganda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm Na Propaganda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Apr 27, 2008.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "Tuwafanye waamini, wasadiki na pia watuunge mkono 2010" Hii ndiyo kauli mbiu ya ccm kwa sasa, kujiuzuru kwa maziri ndani ya serikali ni danganya toto na kamchezo ka funika kombe mwanahalamu apite.

  Ndugu zangu watanzania poleni sana na haya yote tunayoyaona kwa sasa yakitokea ndani ya taifa letu hili lenye wananchi maskini,mtaamini kuwa CCM ni ndiyo waliotufikisha hapo tulipo,sote tunajua kuwa chama hicho ndicho kinatoa mwongozo na serikali inatekeleza.

  Kulindana ndani ya chama hicho si swala geni kila mtanzania anajua, ila la kushangaza hata haya tunayoyaona kwa macho yetu na kushuhudia kama ufisadi bado wanaziba masikio na kutupuuza, wahusika hawawajibishwi kwa maana ya kufikishwa mahakamani, kila likifunuliwa hili wanalifunika kwa jingine, hebu sisi watanzania ni wajinga kiasi hicho?

  Leo wameanza kuwatuhumu jamaa zao kwa hili na lile, hii waifanya ili sisi tuamini kuwa sasa ccm wamechukizwa na ubadhirifu wa mali za umma lakini si hivyo, lao ni moja Matanzania ni majinga tu"chukua chako ikibainika utajiuzuru hakuna shida" hii ni hatari sana kwa taifa changa kama Tanzania.

  Tanzania kweli tutafika? kweli tutaendelea kuona propaganda za ccm kuwadanganya wananchi kule vijijini kuwa wao ni watendaji wazuri na kuendelea kushinda kwa kishindo? haitawezekana kamwe, watanzania tupeleke ujumbe kule vijijini ili ndugu zetu waujue wizi wa ccm ndani ya Taifa letu, na ndipo mabadiliko yatapatikana.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Apr 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Isaya Na Wewe Umeanza Kulalamika Bila Kutoa Suluhisho La Hayo Malalamiko Na Matatizo ?

  Kweli Hatutafika Kama Kila Kitu Tunamwachia Kiumbe Ccm
   
 3. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi naanza kusema hatuwezi kila kitu ku-blame ccm...wananchi na akili timamu waliwachagua na ni wananchi ambao watawaondoa waliyooza...na si wote CCM wameoza...
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Apr 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbunge Ana Wakilisha Wananchi Wote Wale Walio Mchagua Na Hata Wengine Ambao Hawajamchagua , Watendaji Wa Serikali Ambao Ndio Wanaoboronga Zaidi Wenyewe Hatujui Ni Vyama Gani Lakini Hata Kama Wakichemsha Lawama Zinakuja Katika Ccm , Mara Chama Tawala ?

  Hatuwezi Kuendela Kama Tutaendelea Na Brainwash Hizi
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kabisa wananchi kubaki katika CCM na hivyo wakatumia mshiko huo kuiangusha CCM kama alivyoangushwa ZANU na kocha wao Mugabe ,maana hata kura zikirudiwa kuisabiwa tena basi anajikuta ameanguswa na huu au hii ndio bakora inayohitaji kupigwa CCM ,mfano mdogo tu ni hapo Zanzibar kuna CCM malaki ambao bado wana kadi za CCM na ni wanachama hai tena walio mstari wa mbele katika kuitetea CCM kwenye majukwaa na mitaani lakini ukiwapeleka kwenye sanduku la kupigia kura ,dhamana yao hawaipeleki CCM hata uwape fedha kiasi gani ,fedha ya CCM wataitafuna na kura hawaipigii CCM ndio maana CCM miaka yote hawashindi na hilo wanalijua na karibu wizi wanaoufanya utawatokea puani kilichowapa Pemba basi kinatarajiwa kutokea na kufanyika Unguja ,fikiria Pemba kwa mapambano dhidi ya CCM na vyombo vyao dola walimkata kichwa polisi mbali ya huyu kuna wengi tu waliuliwa na hilo polisi wanalijua ndio kisa kilichowafanya wapeleke helikopta na idadi kubwa ya jeshi la polisi lakini walikuwa wamechelewa.Wakabaki kutesa na kupiga bila ya kuwa na uhakika na wanaempiga kiasi ya kuua watu ambao walikuwepo kwa matembezi.
  Sasa kinachohitajika huku Tanganyika ni mbiu ya ..Ukipewa feza na CCM itafune lakini kura yako huipelekei CCM... baasi yaani maneno hayo ni ya kichawi kutoka Pemba ndio yalioimaliza CCM Zanzibar ,jamaa walikuwa wakijenga na kuezeka bati lakini CCM ikaambulia patupu na nina hakika maneno hayo yakishikakasi Tanganyika basi CCM ndio kwa heri maana hizo fedha ni za wananchi sasa ukiwambia wazikatae utakuwa unawazulumu. Haya shime kuenezakauli mbiu hiyo.
   
 6. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..tatizo wananchi wengi hawafahamu nini kinachoendelea.

  ..kama wangefahamu kila kiongozi angewajibika ipasavyo!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watanzania tunapaswa kuacha kuwa mandondocha, matatizo haya yore tunayatakla wenyewe kwa sababu hao ccm hawakuchukua nchi kwa nguvu. wanaweza kuwa wanaiba kura lakini wiapo watanzania tutaamua kwa wingi wetu, hawawezi kufanya kitu? si tunaona mugabe navyohangaika, licha ya kuhesabu kura mara mbilimbili lakini bado hazitoshi. ufungua wa matatizo yetu tunao wenyewe, tunachotakiwa kufanya ni kuacha kulalamika na kuchukua hatua
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  kama dhamana ya nchi walipewa CCM basi wao ndo wanatakiwa kupokea lawama zoote.

  na huo uongo wanaowapwaga watanzania ili waendelee kuwatawala baadhi ya wenye akili timamu tumeshautambua na kuanza kuutaftia dawa...hakuna malefu yasiyo na ncha
   
 9. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Shy

  Ulivyo kuwa na ile picha ya zamani ulikuwa ni kijana mzuri lakini baada ya kuibadilisja ulibadilika gafla. Ebu tupe siri ya mafanikio na mapungufu katika bubadilisha picha.
   
 10. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mimi nachelea kusema, CCM ndiyo baba wa propaganda ila kwa sasa ccm wameanza kuchemka, nadhani hii ni kwa sababu ya kale kamgawanyiko ndani ya chama tawala na haya mapesa wanayotuibia kwa nguvu, bado napata shida sana, ina maana wafuasi wote wa ccm hawawaoni viongozi wao wakiwasaliti? na kwanini wanachama hao wasitoke ndani ya chama hicho? ama ile bendi yao ndiyo kivutio chao?

  Sote tunataka tuwe mashaidi, kama ccm itashinda kwa kishindo 2010 ktk nafasi za ubunge basi sisi sote watanzania tutakuwa mazezeta.
  Najua kwa upande wa urais bado ccm wana nafasi kwani JK bado hajatutoka watu ndani ya mioyo yetu japo hisia za uoga zimetutawala, ila ktk ubunge kweli tufanye mabadiliko, ili serikali ipate changamoto.
   
Loading...