CCM na "Production Concept"

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,514
2,118
Lengo la makala hii fupi ni kuelezea ni kwa namna gani chama cha mapinduzi kilivyo wahafidhina linapkuja suala la mabadiliko. wanajua wazi kabisa kuwa tatizo liko wapi lakini hawataki kuamini kuwa kubadili mfumo ndio tiba ya mabadiliko na ufanisi.

Tunapozungumzia Production Concept ni pale mzalishaji anapoingia katika kuzalisha bidhaa fulani bila wateja kuridhia, au bila mzalishaji kuangalia matakwa na mahitaji ya wateja. Ni imani ya mzalishaji kuwa bidhaa zake zitauzika kwa kuwa wateja WANAZIHITAJI.

Ni moja ni mbinu ya zamani sana ya uzalishaji ambayo wazalishaji waliitumia. Kutokana na maendeleo ya kiviwanda na uzalishaji wa kifanisi, wengi wamekuwa wakizalisha bidhaa zinazofanana na kwa wingi na ndio maana Production Concept ikafa kwa kuwa haikuwa rahisi tena kuwaamulia wateja ni bidhaa gani wanataka ukichukulia kuwa wazalishaji ni wengi na bidhaa ni nyingi na za ubora tofauti.

Ndio maana wazalishaji baada ya kuona wamechemsha kwenye kulazimishia wateja bidhaa wakaja na Product Concept ambapo inaaminika kuwa mteja anapendelea zaidi bidhaa yenye ubora na yenye kumpa faida ya ziada katika kuitumia. Kwa lugha nyingine, umsikilize kwanza anataka nini ndipo utengeneze bidhaa inayoendana na matakwa yake. Bidhaa ambayo itampatia Value for Money.

Tukirudi nyuma tunaona kuwa bidhaa ni kitu kilichozalishwa kwa kutumia nguvukazi, au juhudi, au ni matokeo ya kitendo au mchakato fulani. Katika muktadha wa kisiasa, mgombea wa nafasi yoyote iwe ya kichama au kiserikali ni bidhaa. Ndio maana huwa wanajinadi au wananadiwa ili kupata kukubalika kwa wananchi katika eneo husika.

Katika muktadha huu huu ndipo CCM inapoingia na bidhaa zake (wagombea) na Production Concept yake (kuwaamulia wananchi waongozwe na nani). Pamoja na kuwa na mabadiliko yote yanayoonekana ikiwa ni pamoja na kuwa mfumo wa vyama vingi, upatikanaji wa habari, na uelewa wa wananchi kuhusu yanayoendelea ndani na nje ya nchi, CCM bado wanang'ang'ania Production Concept.

Hili la kung'ang'ania hii dhana limejidhihirisha zaidi tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chenyewe, kipindi cha kampeni, mchakato wa uchaguzi mkuu, hadi uteuzi wa Spika wa Bunge la JMT. Si ajabu dhana hii ikajidhihirisha tena katika uteuzi wa baraza la mawaziri pamoja na watendaji mbalimbali ndani ya serikali. Si nia yangu kutaka kurudia yaliyotokea tangu kura ya maoni hadi uteuzi wa Spika bali wote tunafahamu kuwa CCM na serikali yake inaendelea kuwaamulia wananchi ni nani wa kuwaongoza bila kujali wananchi wana mawazo, mitazamo na mapendekezo gani.

Tumemsikia Ndugu Kikwete na watendaji wengine kama Lowasa na Pinda wakiwa wanajiuliza ni wapi wametetereka hadi yakatokea yaliyotokea. Majibu wanayo, sema tu ni uhafidhina unaochochewa na kuwepo maslahi binafsi, uchoyo na umimi. Kama wakiendelea na hii dhana, basi ni dhahiri kabisa kuwa wananchi ndio watakaoamua ni viongozi wa aina gani wanaowafaa. Tena sio wataamua bali walishaamua sema tu wahafidhina walitumia dola kwa maslahi yao. Mabadiliko ni muhimu
 
Lengo la makala hii fupi ni kuelezea ni kwa namna gani chama cha mapinduzi kilvyo wahafidhina linapkuja suala la mabadiliko. wanajua wazi kabisa kuwa tatizo liko wapi lakini hawataki kuamini kuwa kubadili mfumo ndio tiba ya mabadiliko na ufanisi.

Tunapozungumzia Production Concept ni pale mzalishaji anapongia katika kuzalisha bidhaa fulani bila wateja kuridhia, au bila mzalishaji kuangalia matakwa na mahitaji ya wateja. Ni imani ya mzalishaji kuwa bidhaa zake zitauzika kwa kuwa wateja WANAZIHITAJI.

Ni moja ni mbinu ya zamani sana ya uzalishaji ambayo wazalishaji waliitumia. Kutokana na maendeleo ya kiviwanda na uzalishaji wa kifanisi, wengi wamekuwa wakizalisha bidhaa zinazofanana na kwa wingi na ndio maana Production Concept ikafa kwa kuwa haikuwa rahisi tena kuwaamulia wateja ni bidhaa gani wanataka ukichukulia kuwa wazalishaji ni wengi na bidhaa ni nyingi na za ubora tofauti.

Ndio maana wazalishaji baada ya kuona wamechemsha kwenye kulazimishia wateja bidhaa wakaja na Product Concept ambapo inaaminika kuwa mteja anapendelea zaidi bidhaa yenye ubora na yenye kumpa faida ya ziada katika kuitumia. Kwa lugha nyingine, umsikilize kwanza anataka nini ndipo utengeneze bidhaa inayoendana na matakwa yake. Bidhaa ambayo itampatia Value for Money.

Tukirudi nyuma tunaona kuwa bidhaa ni kitu kilichozalishwa kwa kutumia nguvukazi, au juhudi, au ni matokeo ya kitendo au mchakato fulani. Katika muktadha wa kisiasa, mgombea wa nafasi yoyote iwe ya kichama au kiserikali ni bidhaa. Ndio maana huwa wanajinadi au wananadiwa ili kupata kukubalika kwa wananchi katika eneo husika.

Katika muktadha huu huu ndipo CCM inapoingia na bidhaa zake (wagombea) na Production Concept yake (kuwaamulia wananchi waongoawe na nani). Pamoja na kuwa na mabadiliko yote yanayoonekana ikiwa ni pamoja na kuwa mfumo wa vyama vingi, upatikanaji wa habari, na uelewa wa wananchi kuhusu yanayoendelea ndani na nje ya nchi, CCM bado wanang'ang'ania Production Concept.

Hili la kung'ang'ania hii dhana limejidhihirisha zaidi tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chenyewe, kipindi cha kampeni, mchakato wa uchaguzi mkuu, hadi uteuzi wa Spika wa Bunge la JMT. Si ajabu dhana hii ikajidhihirisha tena katika uteuzi wa baraza la mawaziri pamoja na watendaji mbalimbali ndani ya serikali. Si nia yangu kutaka kurudia yaliyotokea tangu kura ya maoni hadi uteuzi wa Spika bali wote tunafahamu kuwa CCM na serikali yake inaendelea kuwaamulia wananchi ni nani wa kuwaongoza bila kujali wananchi wana mazazo, mitazamo na mapendekezo gani.

Tumemsikia Ndugu Kikwete na watendaji wengine kama Lowasa na Pinda wakiwa wanajiuliza ni wapi wametetereka hadi yakatokea yaliyotokea. Majibu wanayo, sema tu ni uhafidhina unaochochewa na kuwepo maslahi binafsi, uchoyo na umimi. Kama wakiendelea na hii dhana, basi ni dhahiri kabisa kuwa wananchi ndio watakaoamua ni viongozi wa aina gani wanaowafaa. Tena sio wataamua bali walishaamua sema tu wahafidhina walitumia dola kwa maslahi yao. Mabadiliko ni muhimu

Hoo hi ni mzuri sana. Unastahili pongezi, maana hawa wanao jiita SISIEMU FEKI maana original CCM alikufa nayo Mwl Nyerere, wanalazimisha watu watawaliwe na maamuzi yao si watu waliochaguliwa na kura zao. Umeliona hilo, tuchukue hatua. Bandu bandu umaliza gogo, tusikate tamaa. 2015 Tutapata majibu sahihi. Aluta Continua. Mapambano bado yanaendelea.
 
Bahati mbaya ccm iko kwenye point of no return as far as destruction is concerned
 
Hoo hi ni mzuri sana. Unastahili pongezi, maana hawa wanao jiita SISIEMU FEKI maana original CCM alikufa nayo Mwl Nyerere, wanalazimisha watu watawaliwe na maamuzi yao si watu waliochaguliwa na kura zao. Umeliona hilo, tuchukue hatua. Bandu bandu umaliza gogo, tusikate tamaa. 2015 Tutapata majibu sahihi. Aluta Continua. Mapambano bado yanaendelea.
Hope madhara ya kuwaamulia wananchi nini wanataka tunayaona sasa. Kamwe wanasiasa hawawezi tena kuwaamulia wananchi juu ya hatima zao. Wakifanya hivyo wanaipeleka nchi kwenye kona ya maafa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom