CCM na Polisi ni makatibu enezi wa Chadema

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Habari ndio hiyo. Hayo yamesemwa na Dk Slaa katika mkutano wao na waandishi wa habari kuhusiana na tukio zima la Nyololo lililopelekea kuuawa kikatili kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na Mwenyekiti wa wanahabari mkoani Iringa- marehemu Daudi Mwangosi. Kumbe kazi ya John Mnyika sasa imekuwa rahisi zaidi maana pilisi na chama tawala wanafanya kazi yao kwa ufanisi sana. Ufanisi wa kuvuta hisia za wananchi pale ambapo cdm wanakuwa katika shughuli zao za kichama sehemu mbalimbali nchini, na hasa kupitia huu mkondo wa sasa wa Vuguvugu la mabadiliko (M4C).

Asanteni ccm na polisi kwa kazi nzuri ya uenezi ila hatutaki tena mauaji maana kazi ya uenezi haihusiani na mauaji bali sera, uhamasishaji, na utoaji taarifa chanya kwa jamii. Asanteni kwa maana mnarahisiaha mchakato wa kuelekea 2015 ambapo kazi yenu tukuka tutaienzi pale cdm itakaposhika Dola.
 
mungu ibariki Tanzania mungu ibariki cdm pia mungu tubariki sisi wazalendo wa nchi hii. msichoke makamanda chama sasa kimekuwa maarufu sana, hongerenikwa kazi nzuri.
 
Kiukweli ccm kwa sasa wako engo mbaya sana maana hawatakiwi kumumunya wala kumeza. Wakiwaacha cdm, cdm inachanja tu. Wakiwaletea polisi, publicity inaongezeka. Kaaz kwel kwel
 
ivi mauaji ya moro yameishia wapi?????hakuyaongelea nayo

Nakumbuka nilihojji hili kwenye uzi mmoja kuwa, wale wasio na visemeo ni nani angewasemea? Wanahabari walitumia taaluma yao. Wamachinga na wakereketwa wa kawaida nao wapate jukwaa na wala wasisahauliwe
 
Back
Top Bottom