CCM na Polisi ndiyo maadui wa watanzania kwa sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Polisi ndiyo maadui wa watanzania kwa sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by makoye2009, Nov 24, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Wajameni,

  Kwa hali tunayoendelea nayo kwa sasa katika nchi yetu inaonekana kuwa Tanzania ina maadui wakubwa wawili wanaodumaza DEMOKRASIA NA KUVIZA UCHUMI NA USTAWI WA TAIFA LETU. Si wengine baali ni Chama Cha Magamba-CCM na Jeshi la Polisi.

  CCM na POLISI wameamua kuungana ili kubaka demokrasia ya nchi hii. Kitendo cha POLISI kuwa wanazuia maandamano na kuwakamata viongozi wa vyama vya upinzani kila siku pasipo sababu za msingi ni jambo lisilokubalika mahali popote wakti wowote. Jeshi letu la Polisi kwa sasa linafanya kazi kama ROBOTS kwa remote control ya CCM!

  Maandamano ni haki ya Kikatiba ya kila Mtanzania.Kila mu anajua kuwa kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na KUSIMAMIA NA KUSINDIKIZA MAANDAMANO YA WANANCHI WAKTI WOWOTE PALE YANAPOANZA MPAKA YANAPOMALIZIKA. Polisi wanachopaswa ni kupewa taarifa ya Maandamano na baada ya hapo ni kazi yao kulinda na kusimamia maandamano hayo kuwa yaanze salama na kuisha salama. Si kazi ya Polisi kutoa kibali au kuzuia maandamano! Lakini tunachoshuhudia Watanzania kwa sasa ni Polisi kutumiwa na CCM kuzuia maandamano hata yale ambayo ni ya msingi na haki ya kila Mtanzania kulingana na Katiba mbovu iliyopo.

  Polisi wamekuja na KISINGIZIO CHA INTELIJENSIA ili kuhalalisha kuzuia maandamano. Hii ni sababu ambayo ni dhaifu na ya kijinga kabisa kwa Jeshi la Polisi lenye wasomi. Yawezekana kabisa Jeshi la Polisi tulilo nalo limejaa mambumbumbu wa elimu kwa maana ya kuwa Mabolisi wengi huwa wana ajiriwa baada ya kuwa wamekosa mahali pa kwenda kutokana na poor performamce shuleni. Tunajua majangu wengi wameishia la darasa la Saba(Std VII),Form IV na Form VI failures ambao hawakuweza kwenda ualimu wala kujiunga na vyuo vyovyote. Ndiyo maana kufikiri kwa Polisi wetu ni kudogo sana maana IQ yao iko chiiiiiiiiiiiini sana sana kama ya kuku!!!

  Tuangalie mifano hai ya maandamano ambayo yamezuiwa na polisi pasi na sababu za msingi na zuio hilo halikuwa na tija yoyote zaidi ya kuleta mtafaruku,vurugu, vifo na upotevu wa mali.
  1. MAANDAMANO YA ARUSHA: Kabla ya siku ya Maandamano Polisi walitoa kibali na wakakubali kusimamia kuongoza msafara. Lakini siku moja kabla wakawa vigeugeu kuwa hakuna maandamano. Sababu? Intelijensia! Kila mtu anajua kilichotokea siku ilipofika na watu 3 walipoteza uhai kwa sababu za kipumbavu za majuha wa Jeshi letu la Polisi. Lakini baada ya siku kadhaa CHADEMA wakaandaa mkutano wa maandamano ya mazishi ambapo Polisi walisusa na CDM wakaweza kusimamia kila kitu na hakuna kilichoharibika. Kumbe Polisi ndiyo wanaosababisha vurugu na uvunjifu wa amani. Sijui kama hawa jamaa huwa wanafanya tathmini yoyote ya operesheni zao kujua failures and achievements. Sina hakika!
  2. MAANDAMANO YA MBEYA: RC Kandoro kaenda kuwahamisha Wamachinga kwa nguvu toka sehemu zao za Biashara ili waende sehemu zingine ambako hakuna miundombinu wala wateja. Sijui Kandoro alikuwa anategemea nini na hao mapolisi wake wasioenda shule! Matokeo Chingas wakagoma. Ikaanza piga nikupige.Polisi anapiga bomu la machozi Chinga anarusha ngumijiwe mpaka Polisi wakatimua mbio na kuomba msaada wa mgambo na JW. Huu ulikuwa ni uchokozi wa wazi kabisa wa Jeshi la Polisi. Uonevu wa mchana kweupe ambao mtu yeyote hawezi kuuvumilia. Hapa naona Mungu aliamua kuwatetea Chingas kutokana na uonevu huu usiomithilika na ndo maana Polisi walishindwa vibaya
  3. MAANDAMANO YA UDSM: Wale wanafunzi wa Chuo Kiuu waliandaa maandamano kupinga uonevu/unyanyasaji unaofanywa na BODI YA MIKOPO kwa kuwacheleweshea pesa zao za kujikimu na gharama za masomo. Kwa Jeshi la Polisi la watu walioenda shule hakukuwa na sababu ya kuwazuia hawa Wanachuo maana walikuwa na jambo la msingi kabisa na hata Rais Kiwete alishawahi kulalamikia Bodi ya mikopo kuwa haiwatendei haki Wanafunzi. Sasa iweje leo wakiandamana wewe Polisi unaanza kuwapiga mabamu? Kosa lao ni nini? Hivi kudai haki yao kwa maandamano ni kosa kweli??
  4. MAANDAMANO YA KUPINGA MCHAKATO WA KATIBA MPYA: Haya ndiyo yalikuwa kwenye mchakato wa kufanyika Jumamosi hii lakini tayari Polisi wameingilia kati na kuyazuia pasipo na sababu za msingi. Wimbo ni ulueule wa maandamano yatasababisha uvunjifu wa amani kulingana na intelijensia zao za kipuuzi. Lakini tuwajuvye Polisi tu kuwa huu ujinga wao wa kutumiwa na CCM kulinda maslahi yake kuna siku itakuja kula kwao! Watanzania wa sasa si wale wa miaka ya 1950s, 1960s na 1970s enzi za ujima wa Chama kimoja. Kwa sasa ni vyama vingi na wajue kabisa kuwa hao hao viongozi wa upinzani na wabunge wanaowapiga MABOMU YA MACHOZI NA RISASI ZA MOTO KUNA SIKU WATAKUJA KUBANA ****** NA KUWAPIGIA SALUTI!!!
   
 2. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jeshi la polisi kuingilia maandamano na kuamua yawepo au yasiwepo ni ubakaji wa demokrasia! Wao wanapaswa kuyasimamia na kuyalinda maandamano yafanyike ktk hali ya utulivu kwani hata Katiba inaruhusu. Uzoefu unaonyesha namna polisi walivyochangia kuleta fujo ktk maandamano yaliyowahi kufanyika nchini. Maandamano ni haki ya kikatiba.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Serikali ya CCM wanafikiri watu wakitulia ndiyo amani, kumbe hakuna amani, bali watu wanaogopa nguvu ya dola.

  - Hatutaki Amani inayotokana na nguvu ya dola kwa kutumia Jeshi la Polisi.

  - Tunataka amani inayotokana na mioyo iliyoridhika.
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  adui wa watanzania ni watanzania wenyewe.
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono hoja. Unajua the principle of existence says, "Every man will be promoted to the level of his competence." Mtu amepata division four form IV au four VI, huyu anapaswa kutumikia taifa katika level ya chini kabisa. Hapaswi kuwa na cheo cha kuongoza watu zaidi ya 500 katika jamii isipokuwa katika jensi kama inawezekana. Sasa huyu anapitishwa na baadae anaongoza milioni 40 ya watu. Kimsingi haya ni makosa ya kisera. Huyu mtu uwezo wake wa kufikiri upo chini sana, hawezi kutetea hoja na kuibua hoja. Yupo chini. Hawezi kuunganisha hoja zilizoparanganyika. Hawezi kuona mbele na ndo maana wengi wao wanakubali kuishi kwenye nyumba za ajabu.
   
Loading...