CCM na Polisi haya matendo si ndo yale tuliyoyapinga kwa makaburu?

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Tukitaka nchi hii iendelee tuondoe ubaguzi huu wa KIPUMBAVU unaopandikizwa na wanasiasa kwa kutumia vyombo vya dola. Kumbagua mtanzania mwenzio kwa sababu ya itikadi za kisiasa haina tofauti na ubaguzi wa rangi, au ubaguzi mwingine wowote ule. Ni UPUMBAVU kufikiri kuwa ukiwa CCM unakuwa binadamu zaidi kuliko mwenzio asiye CCM.

Tar.03/11/2019 Chama cha mapinduzi tawi la UDOM, kilitoa taarifa ya kuwakaribisha chuoni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Taarifa hiyo ilibandikwa ktk mbao za matangazo (kwa ruhusa ya uongozi wa chuo), kwenye miti, kuta za mabweni, na maeneo mbalimbali ya chuo. Pia ilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Hakuna aliyehoji, aliyekemea, wala aliyesema CCM wanaingiza siasa vyuoni.

Siku chache baadae, Shirikisho la wanafunzi ambao ni wanachama wa CHADEMA chuoni hapo (CHASO UDOM) nao wakatoa tangazo kama lile la CCM la kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni. Walipoenda kwa Dean of students kuomba kibali cha kubandika tangazo hilo kwenye mbao za matangazo wakanyimwa, na kukaripiwa vikali.

Kwa ustaarabu hawakutaka kuchafua kuta za mabweni (kama wenzao walivyofanya), badala yake wakaamua kusambaza taarifa yao kupitia mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa tawi hilo Bw.Henry Mang'era ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 akatuma taarifa hiyo kwenye magroup mbalimbali ya whatsapp. Kesho yake akakamatwa na kupelekwa mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga. Kosa lake ni kusambaza taarifa inayoleta taharuki na kushawishi wanafunzi kufanya siasa chuoni kinyume cha sheria.

Kwa muda wa wiki mbili sasa polisi wamemshikilia, wakimpiga bila kumpeleka mahakamani. Wamekataa kumpatia dhamana licha ya jamaa zake kuwaomba polisi kumpa dhamana au kumpandisha mahakamani ili akajibu mashtaka yanayomkabili.

Waliomtembelea kituoni juzi wanasema alikua anachechemea na kushindwa kusimama vizuri. Inadaiwa alipigwa na kupata majeraha sehemu za goti.

Polisi wanafanya haya wakijua kabisa ni kinyume cha sheria, kwa sababu mtuhumiwa hapaswi kukaa kituoni masaa 48 bila kupandishwa kizimbani. This is detention without trial, ambayo haina tofauti na waliyofanya makaburu kule SA. Mang'era apelekwe mahakani, kama kuna kosa mahakama itaamua.

#Justice4Mangera
FB_IMG_1575208344308.jpeg
 
CCM watu wa ajabu sana, sasa wanadhani kwa vitendo kama hivyo ndio wanawashawishi wasomi wa UDOM kuipenda na kuunga mkono uharamia unaofanywa dhidi ya wenzao?
Hata kule kusini matendo ya makaburu yalikuwa yanawauzi pia wazungu wenye akili.
Hivyo kwa UDOM wanafunzi wapumbavu ndio wanaweza unga mkono matendo hayo kwa wenzao, lakini wenye akili hawawezi hata kidogo na ninaamini vijana wetu sio wapumbavu.
 
Kutoka chama cha Mwalimu Nyerere mpaka kua chama kinachowaogopa CHADEMA .
CCM imekataliwa duniani na mbinguni, Tanganyika na Zanzibar .
 
Vijana kuna msemo ( motto ) unasema, SOMA VITABU UPATA MAARIFA. Hayo yote yapo na yalishatendeka, zamani na hayo ni marudio tu, na kinachotakiwa si kugombana wala kuwachukia wote wanaotenda uovu huo. Hakika hawajui walifanyalo. Kumbuka biblia inasema mtenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. Na mtumwa ana mamlaka juu ya mwili wake mwenyewe. HAOHAO MUDA UKIFIKA NDO WATAKUWA WAPAMBANAJI NA WAPIGANIA DEMOKRASIA NA HAKI HADI TONI LAO LA DAMU. HEBU SOMA HII HABARI Matendo ya Mitume 9:1-4
[1]
Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
[2]akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
[3]Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
[4]Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
Matendo ya Mitume 9:1-4

Kazi ya polisi ni kuilinda ccm,polisi ni Mali ya ccm,
Watailinda hadi lini, Mbona CCM imeshajifia!!? Leo hii muulize hata zezeta atakuambia hataki kuhesabiwa na hayawani aitwaye ccm. CCM imevunda na siku ikizikwa Polisi wengi wataozea kwenye kaburi lake.
Ni juzi tu walibanwa Zimbwabwe dictator Mugabe alipotimuliwa. Hawajifunzi, kazi kuonea watu wema wasio na hatia. Mbaya zaidi kwa akili zao za form four ziro hawaelewi, wanatumiwa kama mpira wa kona siku ukipasuka wasiseme hatukuwaonya.
 
Hapa ndipo uongozi wa chadema unapofeli. Likitokea jambo kama la vijana wanaopigania chama kuteswa na polis CCM ,it's vyombo vya habari taarifu uma A to Z. Hao polis CCM wanapowatesa hao vijana pia huwakejeli kwamba wakowapi viongozi wa chadema kukutetea, mbona uko peke yako. Tunaomba sauti ya Viongozi wa chama iwe inaonekana kukemea uonevu huu at least
 
Watailinda hadi lini, Mbona CCM imeshajifia!!? Leo hii muulize hata zezeta atakuambia hataki kuhesabiwa na hayawani aitwaye ccm. CCM imevunda na siku ikizikwa Polisi wengi wataozea kwenye kaburi lake.
Ni juzi tu walibanwa Zimbwabwe dictator Mugabe alipotimuliwa. Hawajifunzi, kazi kuonea watu wema wasio na hatia. Mbaya zaidi kwa akili zao za form four ziro hawaelewi, wanatumiwa kama mpira wa kona siku ukipasuka wasiseme hatukuwaonya.
Wa chini wanapokea maagizo kuogopa kufukuzwa kazi toka kwa mabosi zao ambao ni wanufaika
 
Back
Top Bottom