CCM Na Njia Ya Kinana.... ( Makala, Raia Mwema)

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
Na Maggid Mjengwa,

MWANAFALSAFA Benjamin Disraeli anasema;

" Mamlaka zote msingi wake ni imani, tunawajibika katika kuyatekeleza yaliyo kwenye mamlaka zetu, na kwamba, mamlaka yatatokana na watu, kwa ajili ya watu, na chemchem zote za fikra ziachwe hai"- Benjamin Disraeli.

Kwa kukiangalia anachosema Diseaeli tunaona, kuwa kazi ya Chama ya cha siasa haipaswi kuwa ni kuudhibiti umma katika kuhoji yanayofanywa na Serikali, badala yake, Chama kinapaswa kuwa upande wa umma.

Ni katika kuyaelewa mahitaji ya umma. Na kwa vile Serikali inapaswa kuwa mtekelezaji wa yale yaliyoamuliwa kwa niaba ya umma, basi, kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuisimamia Serikali katika kuutekeleza wajibu wake huo.

Tumeona, katika muda mfupi, Abdulahaman Kinana , Kama Katibu Mkuu wa Chama kinachoongoza, CCM, amelitambua jukumu lake kama Katibu Mkuu . Hivyo, amelitambua jukumu la Chama chake. Kuwa wajibu wake wa kwanza ni kuisimamia Serikali. Katika mawimbi mazito iliyoyapitia katika miaka ya karibuni,

Wana- CCM wanapaswa kumshukuru Mwenyekiti wao wa Taifa, Jakaya Kikwete, kwa kufikiria kumweka Kinana kwenye nafasi hiyo ya kiutendaji katika wakati muafaka. Tunayemfuatilia tunajua, kuwa Abdulahaman Kinana ni mchapakazi. Na katika anayoyafanya, hana dhamira ya madaraka ya juu kabisa, bali, kukisaidia chama chake, na taifa.

Maana, inavyoonekana sasa, Abdulahaman Kinana amekisaidia chama chake kuitafuta njia mpya ya kisiasa. Njia ya kisiasa anayokwenda nayo Kinana kwa sasa ni ya ' Kati- Kushoto'. Hii ina maana, Kinana anakipeleka chama chake kwenye kupata miafaka ya kisiasa ya ndani ya chama, na wakati huo huo kutafuta kukubalika nje kwenye umma. Hii ni kwa kuegemea kushoto zaidi. Kushoto ya kiitikadi ndiko waliko wengi.

Na njia ya Kinana ndiyo inayopaswa kufuatwa na wenzake ndani ya CCM. ni njia iliyoonyoka na yenye tija kwa umma na hatimaye, ni njia inayoweza kukinufaisha chama chake. Maana, katika siasa, njia nyingine hazina tija kwa umma wala chama chenye kuchagua njia hiyo. Ona ngojera zile za CCM za ' kuvua magamba'. Ama hakika, mradi wa kisiasa wa ' kuvua magamba' ni moja ya miradi ya hasara kubwa Chama Cha Mapinduzi imepata kuifanya. Ni mradi uliokigharimu zaidi chama hicho kisiasa kuliko kukiletea tija.

Na yumkini, makovu ya mradi huo yatabaki kwa muda mrefu ndani ya chama hicho. Maana, mradi wa kujivua magamba haukulenga kwenye kubadili mfumo uliosababisha tatizo, bali , ulichukua sura ya mbio za Urais wa 2015, na hivyo, ukabeba sura ya kuwindana kisiasa ( Political Witch Hunting) zaidi miongoni mwa wana-CCM wenyewe kuliko kukijenga na kukiimarisha chama chao.

Leo Kinana na wenzake wanazunguka mikoani wakijenga hoja zaidi za kisiasa zenye kuwagusa wananchi. Mathalan, Kinana na wenzake wameonyesha wanavyofanya kazi ya kuisimamia Serikali kwa kuwabana watendaji wa Serikali hadharani. Kufanya hivyo ni moja ya kutekeleza wajibu wa chama cha siasa kinachoongoza nchi; kuisimamia Serikali.

Maana, juma la jana niliweka bayana hapa, juu ya tatizo nililoliona, kuwa linaikabili CCM kama Chama cha Siasa, kuwa CCM imeusahau umma uliochoshwa na malumbano ya kisiasa yasiyoisha, malumbano ambayo msingi wake ni vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Chama.

Vita ya kuwania nafasi za juu za uongozi. Umma ambao kwao wao lililo la msingi, kama alivyosema Askofu Desmond Tutu, ni kuhakikishwa wanapata huduma muhimu za msingi, kama vile ajira, elimu, maji ya bomba, makazi bora, huduma za afya na mengineyo.

Umma unahitaji kutoka kwa wanasiasa, kauli zenye kuwatia matumaini ya baadaye. Kauli zenye kuashiria kwamba mwenye kuzitoa, amedhamiria kutatua matatizo yao ya kimsingi. Nikaweka wazi, kuwa hata kwa maslahi ya nchi yetu, ni heri kuwa na CCM yenye makundi yenye kuwania urais 2015 kuliko CCM yenye magenge yenye kuendesha biashara ya ‘siasa za rejareja na au ‘siasa za mafungu' (retail politics).

Ni kwenye ‘siasa za mafungu' ndipo utawakuta wana-CCM wenye kudhani wao ni wasafi, na wenzao ni wachafu. Wakati, kimsingi, jamii nzima kwa sasa ni kama imeoza kimaadili. Leo utawakuta wala rushwa CCM, na hata kwenye vyama vya upinzani. Utawakuta makanisani, misikitini na hata kwenye sekta ya michezo.

Kinachohitajika ni mkakati wa kitaifa utakaohakikisha kwamba huko tuendako, tunapunguza idadi ya viongozi wa kisiasa, kijamii na hata kimichezo watakaoingia kwa nguvu za fedha, hivyo basi, nguvu ya rushwa. Kama alivyopata kutamka Mwalimu kwenye Kitabu Chake; Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, rushwa ni kama kansa kwenye jamii yetu. Kwa hiyo, ni tatizo la kimfumo zaidi kuliko la baadhi kwenye jamii.

Itaendelea juma lijalo...
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,452
2,000
Nasubiria juma lijalo unichambulie mafanikio ya ziara ya Kinana,bila kusahau kashfa ya pembe za ndovu.!
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
Maggid bwana! Kapenda chongo anaita kengeza.

Any way, namshukuru Amani Karume kutuvumbulia hili la ubongo wa samaki, kumbe alikuwa na maana pana sana.
 
kingukitano

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,971
0
Kinana anahekima sana anahubiri mageuzi ya kiutendaji kwa serikali iliyopewa dhamana na chama ameonekana akitetea masuala ya uwajibikaji anahubiri sera za chama na sio kuwinda wanachama wake hili ni tishio kwa upinzani hoja za kibanda sio za kupuuza wanaokejeli wasubiri kuona nini kitatokea katika kuimarisha CCM KUTEKELEZA
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
maggid,

..kama CCM walikuwa na nia ya kweli ya kuisimamia serikali yao basi wangetenganisha kofia ya uenyekiti na uraisi.

..tatizo lingine ni kwamba Kinana hana MORAL AUTHORITY ya kupiga vita ufisadi kwasababu yeye mwenyewe ana tuhuma zake za miaka iliyopita, kama vile suala la Loliondo na uwakala wa kusafirisha nyara za taifa.

..kwangu mimi nadhani CCM wamefika mahali "wamekubali yaishe." wameamua kwamba moving forward, ni lazima mafisadi na wale wasafi wakae pamoja. Bila kumungunya maneno wengi humo CCM wameamua "kula matapishi yao."

..Katika mazingira hayo ndiyo maana unaona Philip Mangula amerudishwa kundini wakati inaeleweka alipendekeza JK atimuliwe wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea uraisi mwaka 2005. Mangula huyuhuyu alifanyiwa vitimbi na kuonekana hafai hata ktk nafasi ya uongozi kwa mkoa wa Iringa.

.
 
Last edited by a moderator:

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
Ndugu Yangu Kingukitano,
Tatizo letu wanadamu ni ukweli, kuwa kuna wnaopenda kusikiliza wanachotaka kusikia. Kuna umuhimu kwa mwanadamu, wakati mwingine, kusikiliza hata kile usichopenda kusikia. Ndio namna pia ya kujifunza.
Maggid
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Kinana anahekima sana anahubiri mageuzi ya kiutendaji kwa serikali iliyopewa dhamana na chama ameonekana akitetea masuala ya uwajibikaji anahubiri sera za chama na sio kuwinda wanachama wake hili ni tishio kwa upinzani hoja za kibanda sio za kupuuza wanaokejeli wasubiri kuona nini kitatokea katika kuimarisha CCM KUTEKELEZA
 
Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
775
1,000
Kaka Maggid

Nachelea kusema kuwa unafanya makosa ya kufanya hitimisho mapema mno on whether Kinana yuko right or wrong or whether he is moving into a right or wrong direction. Wote tunakijua Chama Cha Mapinduzi na viroja vyake visivyoisha kila kukicha. Katika nyanja ya siasa na uongozi wa taifa siku kumi hazitoshi kufanya suluhisho la jambo lolote.

All in all NI MAPEMA MNO KUSEMA LOLOTE KUHUSU UONGOZI AU MAFANIKIO YA KINANA!
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,522
1,225
Kaka majjid nimekuwa nikiheshimu sana fikra zako na mchango wako mkubwa katika kufundisha,kutoa mawazo yako na kupashana habari,natambua weledi wako katika uandishi na kila mwana JF analifahamu hilo, naelewa umekuwa muumini usiyefungamana na upande wowote ila kuna jambo hapa nataka kukwambia kaka yangu, inawezekana kabisa unayoyaona kwa Kinana na kwa jinsi ambavyo umesema unamfahamu yakawa ya kweli lakini Kinana huyuhuyu ndiye yuleyule ambaye ana kashfa za kusafirisha nyara zetu,Kinana huyuhuyu ndiye aliyeamua kuachana na siasa kwa kujiuzulu nyazifa alizokuwa nazo eti anawaachia wengine na uongozi ni kupokezana vijiti, sasa kilichomrudisha tena kwenye siasa ni kitu gani?

Au kaka Majjid hujaliona hilo?Leo hii nasema nyama fulani siitaki,baada ya siku kupita nakaribishwa kwenye sherehe na kukubali kula,nitaelewekaje?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
437
250
Ndugu, safari hii mbona unakuwa mwepesi wa kuamua, ndiyo kwanza Kinana ameanza kazi tayari umeisha anza kumsifia. Sijaelewa tofauti ya Kinana na Mkama.

Ndugu Mjengwa ufahakuwa kuwa chama ni 'system' na chama siyo mtu. Aliyofanya Mkama haukuwa mpango wake kama Mkama bali ulikuwa mpango wa CCM, na haya anayofanya Kinana ni mpango wa chama (ccm). La msingi ujue kuwa haya yote wanayofanya ni kutapatapa baada ya kuona maji yako shingoni.

Wanatafuta namna ya kujinusuru. Tegemea kuona mabadiliko mengi kabla ya 2015. Kama kweli Kinana anaweza basi akamate watuhumiwa wa EPA, Kagoda, Meremeta na kadhalika na ufisadi, rushwa na kashifa za kila aina zilizomo ndani ya serikali.
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,289
2,000
Maggid bwana! Kapenda chongo anaita kengeza.

Any way, namshukuru Amani Karume kutuvumbulia hili la ubongo wa samaki, kumbe alikuwa na maana pana sana.
Ipo kazi kwa magamba.Hata vijana wenye exposure kama huyu jamaa Maggid .Akiwa nje ya nchi anaweza jifanya kuwa ni sehemu ya mageuzi ila akirudi ndani ni sehemu ya scavengers wa CCM.
 
Pancras Suday

Verified Member
Jun 24, 2011
7,758
2,000
Na Maggid Mjengwa,

MWANAFALSAFA Benjamin Disraeli anasema;

¡° Mamlaka zote msingi wake ni imani, tunawajibika katika kuyatekeleza yaliyo kwenye mamlaka zetu, na kwamba, mamlaka yatatokana na watu, kwa ajili ya watu, na chemchem zote za fikra ziachwe hai¡±- Benjamin Disraeli.

Kwa kukiangalia anachosema Diseaeli tunaona, kuwa kazi ya Chama ya cha siasa haipaswi kuwa ni kuudhibiti umma katika kuhoji yanayofanywa na Serikali, badala yake, Chama kinapaswa kuwa upande wa umma.

Ni katika kuyaelewa mahitaji ya umma. Na kwa vile Serikali inapaswa kuwa mtekelezaji wa yale yaliyoamuliwa kwa niaba ya umma, basi, kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuisimamia Serikali katika kuutekeleza wajibu wake huo.

Tumeona, katika muda mfupi, Abdulahaman Kinana , Kama Katibu Mkuu wa Chama kinachoongoza, CCM, amelitambua jukumu lake kama Katibu Mkuu . Hivyo, amelitambua jukumu la Chama chake. Kuwa wajibu wake wa kwanza ni kuisimamia Serikali. Katika mawimbi mazito iliyoyapitia katika miaka ya karibuni,

Wana- CCM wanapaswa kumshukuru Mwenyekiti wao wa Taifa, Jakaya Kikwete, kwa kufikiria kumweka Kinana kwenye nafasi hiyo ya kiutendaji katika wakati muafaka. Tunayemfuatilia tunajua, kuwa Abdulahaman Kinana ni mchapakazi. Na katika anayoyafanya, hana dhamira ya madaraka ya juu kabisa, bali, kukisaidia chama chake, na taifa.

Maana, inavyoonekana sasa, Abdulahaman Kinana amekisaidia chama chake kuitafuta njia mpya ya kisiasa. Njia ya kisiasa anayokwenda nayo Kinana kwa sasa ni ya ¡® Kati- Kushoto¡¯. Hii ina maana, Kinana anakipeleka chama chake kwenye kupata miafaka ya kisiasa ya ndani ya chama, na wakati huo huo kutafuta kukubalika nje kwenye umma. Hii ni kwa kuegemea kushoto zaidi. Kushoto ya kiitikadi ndiko waliko wengi.

Na njia ya Kinana ndiyo inayopaswa kufuatwa na wenzake ndani ya CCM. ni njia iliyoonyoka na yenye tija kwa umma na hatimaye, ni njia inayoweza kukinufaisha chama chake. Maana, katika siasa, njia nyingine hazina tija kwa umma wala chama chenye kuchagua njia hiyo. Ona ngojera zile za CCM za ¡® kuvua magamba¡¯. Ama hakika, mradi wa kisiasa wa ¡® kuvua magamba¡¯ ni moja ya miradi ya hasara kubwa Chama Cha Mapinduzi imepata kuifanya. Ni mradi uliokigharimu zaidi chama hicho kisiasa kuliko kukiletea tija.

Na yumkini, makovu ya mradi huo yatabaki kwa muda mrefu ndani ya chama hicho. Maana, mradi wa kujivua magamba haukulenga kwenye kubadili mfumo uliosababisha tatizo, bali , ulichukua sura ya mbio za Urais wa 2015, na hivyo, ukabeba sura ya kuwindana kisiasa ( Political Witch Hunting) zaidi miongoni mwa wana-CCM wenyewe kuliko kukijenga na kukiimarisha chama chao.

Leo Kinana na wenzake wanazunguka mikoani wakijenga hoja zaidi za kisiasa zenye kuwagusa wananchi. Mathalan, Kinana na wenzake wameonyesha wanavyofanya kazi ya kuisimamia Serikali kwa kuwabana watendaji wa Serikali hadharani. Kufanya hivyo ni moja ya kutekeleza wajibu wa chama cha siasa kinachoongoza nchi; kuisimamia Serikali.

Maana, juma la jana niliweka bayana hapa, juu ya tatizo nililoliona, kuwa linaikabili CCM kama Chama cha Siasa, kuwa CCM imeusahau umma uliochoshwa na malumbano ya kisiasa yasiyoisha, malumbano ambayo msingi wake ni vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Chama.

Vita ya kuwania nafasi za juu za uongozi. Umma ambao kwao wao lililo la msingi, kama alivyosema Askofu Desmond Tutu, ni kuhakikishwa wanapata huduma muhimu za msingi, kama vile ajira, elimu, maji ya bomba, makazi bora, huduma za afya na mengineyo.

Umma unahitaji kutoka kwa wanasiasa, kauli zenye kuwatia matumaini ya baadaye. Kauli zenye kuashiria kwamba mwenye kuzitoa, amedhamiria kutatua matatizo yao ya kimsingi. Nikaweka wazi, kuwa hata kwa maslahi ya nchi yetu, ni heri kuwa na CCM yenye makundi yenye kuwania urais 2015 kuliko CCM yenye magenge yenye kuendesha biashara ya ¡®siasa za rejareja na au ¡®siasa za mafungu¡¯ (retail politics).

Ni kwenye ¡®siasa za mafungu¡¯ ndipo utawakuta wana-CCM wenye kudhani wao ni wasafi, na wenzao ni wachafu. Wakati, kimsingi, jamii nzima kwa sasa ni kama imeoza kimaadili. Leo utawakuta wala rushwa CCM, na hata kwenye vyama vya upinzani. Utawakuta makanisani, misikitini na hata kwenye sekta ya michezo.

Kinachohitajika ni mkakati wa kitaifa utakaohakikisha kwamba huko tuendako, tunapunguza idadi ya viongozi wa kisiasa, kijamii na hata kimichezo watakaoingia kwa nguvu za fedha, hivyo basi, nguvu ya rushwa. Kama alivyopata kutamka Mwalimu kwenye Kitabu Chake; Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, rushwa ni kama kansa kwenye jamii yetu. Kwa hiyo, ni tatizo la kimfumo zaidi kuliko la baadhi kwenye jamii.

Itaendelea juma lijalo...
Ndugu yangu maggid, hebu tujaribu kuuachia muda naona ucheze sehemu yake ndipo tuanze kupima utendaji wa Kinana, watu tumeegemea sana katika kumhukumu Kinana pasipo kumuachia muda angalau wa kupima utendaji wake. Hapa ndo ninapokuwa na wasiwasi juu ya wale wote wanamuhukumu Kinana aidha kuwa si lolote au wale wanaosema Kinana kamaliza kila kitu katika uongozi wake, nijuavyo mimi huwezi kufanya evaluation ya kitu pasipo output ambayo imetokana na input kupitia processing, input yetu hapa ni Kinana ambaye yupo kwenye processing, lakini bado hatujaiona output ya Kinana ili tuweze kuifanyia evaluation
 
Top Bottom