Elections 2010 CCM na NEC mnaipeleka wapi Tanzania

lufunyo

lufunyo

Member
70
0
Kwanza kabisa niwape pole ndugu zetu wote walioathirika na ubinafsi na ubabe wa chama tawala kupitia wakala wake NEC na jeshi. Nasema hivyo kwani imedhihirika kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inafanyakazi iliyotumwa na chama tawala ya kuhakikisha kuwa kinashinda.

Wananchi wazalendo tumepiga kura kwa amani na utulivu wa hali ya juu lakini inasikitisha kuona kuwa kupata matokeo (yaliyojumlishwa) kutoka kwa wasimamizi wakuu* (wa wizi) wa kura jimboni yanacheleweshwa ili mradi tu wapate muda wa kutosha wa kuchakachua matokeo. Na ukifuatilia kwa makini sehemu ambazo matokeo yanacheleweshwa ni kule ambako chama tawala kimebwagwa! Cha ajabu zaidi ni pale jumla ya matokeo ya vituoni inatofautian na jumla inayotangazwa na hawa jamaa* ref: udiwani ilala.

Naomba ijulikane kuwa amani iliyopo sasa hivi inathamani kubwa lakini itadumu tu iwapo Serikali ya ccm na vyombo vingine vya dola vikitambua kuwa hii ni nchi ya kidemokrasia ambapo wananchi ndiyo wenye jukumu la kuamua nani awe kiongozi na nani asiwe. Kupitia uchaguzi huu nimejifunza kuwa ccm inaamini kuwa kuna watu wachache aka mafisadi wanaweza kupanga ni viongozi gani wawaongoze akina nani. Huu ni UPUUZI mtupu. Dunia inabadilika, Tanzania inabadilika na watanzania wanabadilika kwa kasi ya ajabu! Hivyo basi ili CCM iweze kuongoza kwa amani lazima iangalie wananchi wanataka nini na si vinginevyo. Vinginevyo nchi itakuwa haitawaliki.
 
L

Lorah

JF-Expert Member
1,193
0
Wananchi si tuna uwezo wa kushinikiza katiba mpya kama kenyaaa jamani

haya mambo ya vyombo nyeti kama tume ya uchaguzi wakubwa wao kuteuliwa na rais ndo matatizo yanapoanzia
mwaka huu lazima tushinikize katiba mpya ya nchi..
Zanzibar wameshatupiga bao siye tunalinda amani tuuuuuu amani ambayo haipooooooooo
 
Cassava

Cassava

JF-Expert Member
282
195
:tape::tape::tape::tape: Sina la kusema
 
M

Mantaleka

Senior Member
104
0
Kibaya ni kwamba hao watakao wekwa kwa lazima, nakuthibitishia safari hii hawata dumu hata kidogo inasikitisha lakini hawa nguvu ya kazi ya leo ninavyo waona mmhn tutayasikia, kama jana nimekoswa koswa na mijiwe nikipita na gari yangu bila hatia yoyote je hawa jamaa wa kulazimisha watakuwa salama kweli.
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom