CCM na Maslahi ya Taifa

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Ninadhani sifa kuu ya wana CCM ni kulinda maslahi ya chama chao kwa nguvu zote. Hii inatokana na maamuzi ya CC-CCM ya hivi majuzi kuwashughulikia viongozi wa Jumuiya ya Wazazi na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Singida. Leo hii nimeshangaa kuona news hii kwamba UWT nako moto unawaka kisa MKATABA wa ukodishaji wa kitega uchumi chao. Kinachoshangaza hao hao vigogo wa UWT na CC-CCM (wengi wao wamo Bungeni na baadhi ni viongozi waandamizi ndani ya serikali) ukiwaomba mikataba ya serikali ichunguzwe wanakuwa wakali kama nyuki. Hivi hii double standard inatupeleka wapi nchi hii? Hivi kitendo cha serikali kuwa na msimamo wa kugoma kuchunguzwa mikataba na ubadhirifu wa mambo mbali mbali ambayo yameongelewa sana, haioni kwamba inapoteza credibility yake kwenye macho ya wananchi? Iweje leo fedha za CCM ziwe muhimu sana kiasi cha kufukuzana/kusimamishana uongozi ilihali waliotafuna hela za umma tena mabilioni ya kumwaga wanaendelea kutesa mtaani na wako "comfortable" wala hawana pressure. Ina maana kula hela ya CCM ni dhambi kubwa sana na kula hela ya serikali siyo kosa? JK anatupeleka wapi na CCM yake? Afadhali hizo habari za ndani ya CCM zingebaki kuwa siri yao ili wananchi tusijue na tukabaki na imani kwamba labda awamu ya nne haioni kama kuna ufisadi iwe serikalini au kwenye chama chao. Hii ni aibu kubwa kwa uongozi wa CCM na aibu kwa viongozi wa serikali kwa kuwa JK ni president na cheamani wa CCM, akina EL na wengineo ni wajumbe wa CC-CCM na PM pia. Habari kamili hii hapa chini:

UWT kwawaka Baraza likijadili viongozi Dodoma
*Chanzo ni ukodishaji City Ambassador

Na Mwandishi Wetu, Dodoma


SIKU chache baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamisha uongozi wa juu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho kwa tuhuma za ubadhirifu, na kisha Kamati ya Utekelezaji ya jumuiya hiyo kujiuzulu, mambo si shwari ndani ya Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, ambapo uongozi wa juu wa umoja huo uko matatani baada ya kusemekana kusaini mkataba usiozingatia maslahi yao.

Taarifa zilizopatikana jana mjini hapa zimeeleza na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa umoja huo kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi za juu huenda akasimishwa kutokana na tuhuma za kusaini mkataba wa ukodishaji wa jengo la kitega uchumi la UWT la City Ambassador, lililopo karibu na kona ya barabara za Kawawa na Ali Hassan Mwinyi.

Kutwa nzima ya jana, Baraza Kuu la UWT lilikuwa katika harakati za mkutano wa kulijadili suala hilo na mara kadhaa, mmoja wa viongozi wa umoja huo, alikuwa akitolewa nje wakati Baraza likimjadili. Pia alitolewa nje ya kamati ya utekelezaji ya umoja huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kikao cha baraza hilo kilitawaliwa na mvutano ambao msingi mkubwa ni kile kinachoonekana kutoshirikishwa na au kutozingatiwa kwa maslahi ya umoja huo pamoja na ya chama. Kikao kilendelea kwa muda mrefu hadi usiku.

Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliusimamisha uongozi wa juu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho kwa tuhuma za ubadhirifu. Miongoni mwa watu waliosimamishwa na Kamati Kuu (CC) ndani ya jumuiya hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu ni pamoja na Mwenyekiti, Abihudi Maregesi, Makamu wake Ramadhani Suleiman Nzori na Katibu Mkuu, Cosmas Hinju.

Umoja wa Wanawake, Jumuiya ya wazazi na Umoja wa Vijana (U-CCM) ni mihimili muhimu ya CCM, ambayo nayo ni mhimili wa muhimu chama hicho.

Tangu kuundwa kwa CCM Februari 5, mwaka 1977, baada ya kuvunjwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shiraz (ASP), jumuiya hizo zimekuwa nguzo muhimu suala lolote linalozigusa jumuiya hizo ni suala la chama
.
Kwa vingunge wa CCM maslahi ya chama ni muhimu sana kuliko maslahi ya nchi. Kweli tutafika?
 
Kwa vingunge wa CCM maslahi ya chama ni muhimu sana kuliko maslahi ya nchi. Kweli tutafika?


Mhe Mwanakijiji aliwahi kusema hapa kuwa fedha za CCM zinauma sana. Mimi naona hizi ni jitihada za kuwaondoa wale wote wasio wanamtandao ndani ya jumuiya za Chama.
 
Mhe Mwanakijiji aliwahi kusema hapa kuwa fedha za CCM zinauma sana. Mimi naona hizi ni jitihada za kuwaondoa wale wote wasio wanamtandao ndani ya jumuiya za Chama.
Kutokuwa mwanamtandao hakuhalishi ubadhirifu wa mali za chama; bora hao wachache washughulikiwe labda kidogo kidogo itachangia kuelimisha jamii yetu kuwa rushwa ni kitu kibaya.

Vita vya panzi neema ya kunguru!
 
Hoja bungeni ziangalie maslahi ya Taifa (Maoni)

Kutoka gazeti la Mwananchi.

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi lilimsimamisha ubunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kujishughulisha na shughuli za Bunge hadi Januari mwakani kwa madai kuwa kasema uongo.

Akitangaza maamuzi hayo baada ya kutolewa hoja na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, iliyojengwa kwa misingi kwamba Zitto kazungumza uongo, Spika wa Bunge, Samwel Sitta, alisema mbunge huyo amesimamishwa kuhudhuria vikao viwili hiki kinachoendelea na kile kitakachofanyika Novemba.

Awali Mbunge Zitto akitoa hoja hiyo binafsi, alihoji kuhusu utaratibu uliotumiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini haraka mkataba wa mradi wa madini wa Buzwagi, wilayani Kahama.

Ziito alilitaka Bunge likubali kuunda kamati hiyo teule ili kuchunguza mwenendo mzima wa kusainiwa kwa mradi huo kulikofanyika jijini London, Uingereza Februari mwaka huu.

Kinyume na ilivyotarajiwa na wengi, hoja hiyo ililigeuza Bunge kuwa uwanja wa mapambano ya kiitikadi miongoni mwa wabunge waliochangia.

Wabunge walirushiana vijembe na kejeli kutoka miongoni mwa wabunge wa chama tawala, CCM dhidi ya wale wa upinzani ambao kwa kiasi kikubwa uchache wao uliwafanya waonekane dhaifu na hivyo kushindwa kuhimili vishindo.

Kwa hakika mjadala huu umewasikitisha Watanzania wengi waliokuwa wakifuatilia kwa karibu baada ya wabunge wengi kuacha kuchangia hoja na kujikita katika kumshambulia mtu binafsi badala ya kujenga hoja.

Tunasema hivyo kwa sababu hoja ya Mbunge Zitto haikuangaliwa kama ilikuwa na maslahi ya nchi, bali kwa wabunge wa CCM ambao ndio wengi waliangalia zaidi imetolewa na nani na anatoka chama gani.


Ni wazi kabisa kwamba kama hoja hiyo ingetolewa na Mbunge wa CCM mvutano mkali wa kiitikadi ambao ulijitokeza bungeni kujadili hoja hiyo usingekuwapo.

Hoja iliyokuwa mbele ya Bunge ilikuwa ni kujadili utata uliojitokeza katika mkataba wa madini ambao serikali ilikwenda kusaini Uingereza, lakini katika hali ya kushangaza, hoja hiyo iliachwa na badala yake mtoa hoja akaadhibiwa kwa madai kuwa kasema uongo.

Kama hali hii ikaachiwa iendelee, maana yake ni kuwa wabunge watakaokuwa wanahoji hitilafu za utendaji wa serikali watakuwa wale wa kutoka upande wa upinzani na hivyo kuiathiri kwa kiasi kikubwa dhana ya Bunge kuisimamia serikali.

Sisi tunaunga mkono hoja iliyotolewa hivi karibuni na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Joseph Warioba kuwa ipo haja ya kubadilisha baadhi ya vipengele vya katiba ili kulipa uwezo zaidi Bunge kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

Tunahoji uhalali wa Bunge kukataa hoja ya Mbunge Zitto ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza utata uliopo katika mkataba huo kwa madai kuwa ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi, wakati Bunge hilo hilo liliunda tume iliyotumia Shmilioni 100 kuchunguza mvutano kati ya Mbunge wa Mkurunga, Adam Malima na mfanyabiashara, Reginald Mengi ambayo matokeo yake ilikuwa ni uamuzi wa Spika Sitta kuwapatananisha watu hao.

Tunadhani hapa maslahi ya taifa hayakuangaliwa kabisa bali kilichoangaliwa ni nani ametoa hoja hiyo na ushabiki wa kiitikadi ndio ambao ulichukua nafasi yake.

Kilio cha Watanzania wengi ni mikataba mibovu inayosainiwa na watu waliopewa kuisaini kwa niaba ya Watanzania na kisha mzigo wake unaachiwa kwa wananchi. Tumeshuhudia miakata ya IPTL ambayo sasa ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

Tunaamini kwamba kupitia kamati ya Bunge iliyokuwa imependekezwa na Mbunge Zitto, ukweli wa jambo hilo ungeweza kupatikana na hivyo kuondoa wingu la wasiwasi lililotanda katika mkataba huo.

Zitto katoa hoja na Karamagi kajibu hoja kwa nini Bunge ligeuke na kumwona Zitto kasema uongo bila ya kuachia kazi hiyo chombo kingine kuchunguza?
 

DOWUTA yawashangaa wabunge

na Hellen Ngoromera
TAnzania Daima

CHAMA cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), kimeeleza kushangazwa na hatua ya wabunge kuitaka serikali kuvunja sasa mkataba wa Kampuni ya Kimataifa ya Huduma ya Makasha (TICTS), kikisema kuwa kilishatoa taarifa za TICTS kutaka kuongezewa muda wa mkataba kabla haujasainiwa.
Kauli hiyo ya DOWUTA imekuja siku moja baada ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kulijia juu suala hilo na kutaka serikali kuvunja mkataba huo sambamba na muda ulioongezwa kuondolewa.

Katibu wa DOWUTA, Abdallah Kibunda alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, hatua ya wabunge kutaka mkataba huo kuvunjwa italiingiza taifa katika hasara kubwa kwa sababu ikiwa utavunjwa, itabidi ilipe fidia kwa kuuvunja mkataba huo bila sababu.

"Suala hilo si geni masikioni mwa wabunge hao, kwani walilielewa tangu mapema. Awali niliposikia fununu kuwa TICTS inataka kuongezewa muda wa mkataba kabla ya ule wa awali haujamalizika, nilikwenda kumweleza aliyekuwa Mshauri wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Kingunge Ngombare Mwiru na kumwambia rais ameshauriwa vibaya.

"Kingunge aliniambia hakuwepo katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichomshauri rais kuiongezea muda TICTS, lakini aliniambia atalifanyia kazi. Pamoja na Kingunge nilikutana pia na baadhi ya wabunge wa Kamati ya Miundombinu, nao waliniambia watalifanyia kazi, lakini hakukuwa na lolote hadi leo, kwa kweli wanatufanyia kiini macho," alisema Kibunda.

Kwa mujibu wa Kibunda kama wabunge hao wanataka kuisaidia serikali na wananchi, walishauri Bunge na rais kuunda kamati kama iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu uliofanywa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili kujua chanzo na mazingira yaliyosababisha muda wa mkataba huo kuongezwa kabla ule wa awali haujamalizika.

Sakata hilo liliibuka juzi baada ya baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Kamati ya Miundombinu kuhoji kitendo cha serikali kuongeza muda wa mkataba wa Kampuni ya TICTS, ilhali muda wa awali ukiwa haujamalizika.

Wabunge hao pia walihoji ukimya wa serikali katika uongezaji wa muda katika mkataba kutoka miaka 10 hadi 25.
 
Wabunge wahoji mkatabawa TICTS
na Tamali Vullu

BAADHI ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamehoji kitendo cha serikali kuongeza muda wa mkataba wa kampuni ya upakuaji mizigo bandarini ya TICTS, ilhali muda wa awali ukiwa haujamalizika.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati ya Miundombinu, pia wamehoji ukimya wa serikali baada ya uongezaji wa muda katika mkataba kutoka miaka 10 hadi 25.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Anne Kilango Malecela (Same Mashariki-CCM), alisema jana kuwa awali, mkataba huo ulikuwa wa miaka mitano, lakini hata kabla muda huo haujamalizika, serikali iliamua kuongeza miaka 15 bila kuweka suala hilo hadharani.

"TICTS kazi zao ni mbovu, lakini cha kushangaza serikali imeongeza miaka 15 zaidi katika mkataba… tena ndani ya mkataba kuna kipengele ambacho kinafanya kampuni hiyo kuwa monopoly (uhuru wa kuwa peke yake katika biashara).

"Kipengele hicho kinaeleza kampuni hiyo itakapokuwa na uwezo wa kuingiza kontena 600,000 kwa mwaka, ndio wataruhusiwa washindani wengine katika biashara hiyo," alisema.

Alisema kipengele hicho cha mkataba kinasababisha kampuni hiyo kufanya kazi kidogo kidogo, ili wasipate washindani.

Mbunge huyo alishauri kipengele hicho kifutwe katika mkataba huo haraka, sambamba na kuondolewa kipengele cha ukodishwaji kwa miaka 15 iliyoongezwa katika mkataba huo.

Mjumbe mwingine, Mtutura Mtutura (Tunduru-CCM), alisema utendaji mbovu wa TICTS unatokana na mkataba mbovu ulioingiwa baina ya serikali na kampuni hiyo.

Alisema kwa kutumia kipengele cha monopoly, kampuni hiyo ina uhuru wa kuchezea huduma hiyo na aliishauri serikali kuangalia upya mkataba huo.

Pia alihoji kwa nini serikali iliamua kuupitia upya mkataba huo wakati muda wa awali wa mkataba huo ulikuwa haujamalizika.

"Tena serikali ili-renew (huisha) mkataba huo katika kipindi cha uchaguzi mkuu. Je, serikali ilikuwa na haraka gani?" alihoji Mtutura.

Akijibu hoja kwa wabunge hao, mmoja wa maofisa wa TICTS, alisema kwa siku bandarini wanapokea karibu kontena 60, na sehemu yenyewe ni ndogo, ndiyo maana kunaonekana kuna mlundikano wa mizigo.

Hata hivyo, alisema wana ghala la kuweka makontena eneo la Ubungo, lakini tatizo ni jinsi ya kuyasafirisha mpaka eneo hilo na kusema kwamba wameshazungumza na Shirika la Reli (TRL) ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

"Tumezungumza na mwekezaji mpya wa TRL na kuanzia Februari mwaka huu, tutaanza kupeleka kontena Ubungo, ili kupunguza msongamano," alisema.

Hata hivyo, mbunge mwingine, Philemon Sarungi (Rorya-CCM), alisema TICTS haijatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Edward Lowassa la kuwataka wapunguze mlundiko mkubwa wa makontena bandarini hapo.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Dk. Batholomew Rufunjo, alisema serikali iliamua kuongeza muda wa mkataba huo kutokana na maendeleo mazuri yaliyoonekana bandarini.

Hata hivyo, jibu hilo liliwafanya baadhi ya wabunge kuguna na kumtaka Rufunjo kutoa sababu za msingi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga, aliingilia kati na kusema: "Watu wanahoji kulikuwa na haraka gani ya serikali kuongeza muda na mbona ilikuwa kimyakimya? Haikutangazwa?"

Hata hivyo, baada ya hoja hizo, alipotakiwa kujibu, Rufunjo alisema ameshaeleza sababu za kuongezwa kwa muda wa mkataba huo na kumuomba Mwenyekiti aendelee kuzungumza.

Malecela alisikika akisema swali hilo ni gumu na kusema kamati hiyo inahitaji kuuona mkataba huo, ili iweze kuishauri serikali baadhi ya vipengele vya kuvirekebisha.

Kamati hiyo iliamua kuhoji kuhusu mkataba huo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Wakati fulani alipotembea kitengo hicho bandarini hapo, Lowassa aliagiza TICTS ifanye kazi kwa saa 24 kama njia ya kupunguza mlundikano wa makontena na kupunguza kero za wafanyabiashara.

Source: Tanzania Daima
 
je wajumbe wa kamati ya miundombinu ni walewale au wamebadilika?
na hata kama wamebadilika ni vyema kujua kama suala hili liliwekwa katika ripoti yao ya makabidhiano/kumaliza muda (kama ipo) na je wajumbe wa kamati mpya walilijua hili tangu awali au la.

mzee kingunge inabidi awekwe kitimoto kuhusu hili.
 
Usanii wa JK na kundi lake unaendelea, hatuwezi kupiga hatua wakati wanaofanya maovu wanaachiwa waendelee kufaidi pesa za walipa kodi.
 
How much it will cost the country

2008-11-16 12:00:00
By The Guardian on Sunday Team


The newly proposed parliament size that will increase the number of MPs from the current 232 to 360 in 2010 will cost the taxpayers an extra stunning Sh43.94billion, should the proposal by the ruling party be approved.

The amount includes salaries and allowances for five years, interest- free car loan and gratuity for the lawmakers.

This amount can fully funds 5000 university students for four years or can build 380km of tarmac roads.

If the proposal submitted by the ruling party sail through, the taxpayers will have to pay Sh15.984billion as annual salaries and allowances to their law makers.

This amount is 55percent extra cost to what taxpayers who are reeling with war against poverty in a country where half of the 38million plus population still survive in a less than a dollar per day, pay their current 232 MPs.

With the current size of the parliament, the nation is paying a heft pay amounting to Sh10.3billion per year, apart from interest free loans granted to the legislators as well as the annually sitting allowances.

The interest free loans for the MPs? posh cars will cost Sh7.2billion if after 2010 election will adopt the proposed 360 lawmakers.

Not only that but also, taxpayers will have to dig deeper into their pockets to pay the gratuity amounting to Sh9billion to proposed 360MPs when their five year term expires.

This is a 55 percent extra to what the current legislators will pocket in 2010 when their term expires.

But this cost is subject to increase, depending on how the lawmakers would review their heft pays after the 2010 election as well as the country`s economic trend.

Currently, the MP receives Sh1.5million as basic salary, Sh700,000 as constituency allowance, Sh500,000 as fuel allowance, plus another Sh 500,000 as driver/ car maintenance allowance, per month.

The lawmakers also receive another Sh500,000 for personal assistants per month.

During parliamentary sessions a legislator earns Sh80,000 per day as sitting allowance.

The longest session is the budget session which takes more than 70 days from mid-June to August compared to three other sessions lasting a fortnight each in January, April and October each year.

The MPs also are entitled to receive a gratuity amounting to Sh25million after the end of their five years term.

In terms of size, the Tanzania parliament will be bigger than highly developed African countries like South Africa, according to the available online information.

South Africa with an estimated population of over 45million plus annual Gross Domestic Product valued at $170billion owns the quarter of Africa?s economy, according to the World Bank report of 2007.

In East Africa, the proposed parliament will be leading in terms of size, being followed by Uganda which has 332 MPs, while Kenya will be the third with 213 MPs.


SOURCE: Sunday Observer

Comment on this article
 
Back
Top Bottom