mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Mpaka sasa napata shida kuwaelewa hawa chama tawala. Rais wa nchi ni mwenyeketi wa chama. Waziri Mkuu ni mjumbe wa halmashauri kuu, kiongozi wa caucaus ya CCM bungeni, na ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za serikali. Spika wa Bunge ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama, Mawaziri kibao ni viongozi katika kamati kuu ya chama km kina Mwigulu, Asha Rose, na wengineo. Kwa maneno mengine karibia viongozi wote wakuu wa serikali ndio hao hao viongozi wakuu wa chama tawala.
Sasa inakuwaje kinana na nape wajifanye wanaumizwa sana na matatizo ya wananchi na kushanaa shida zao na kubaki kulalamika km hao wananchi wakati wao ndio wana miundo mbinu yote ya kufanya mabdiliko ili kero za wananchi zipungue? Wanashindwa nini kwa mfano kuamua kwamba kuanzia leo posho posho zilizoeleweka mwisho? Kuanzia leo hakuna kiongozi wa CCM kutumia shangingi? Ni nini kinawazuia kufanya uamuzi imara wa kuabdilisha maisha ya watanzania kwa kuamua kubana matumizi kwa kupunguza kuishi maisha ya anasa huku wengine wanyonge wanaumia? Wanashindwa nini wakati miundo mbinu yote wanayo na uwezo wanao kwa sababu wao ndio wenye serikali?
Kwa nini waje kushangaa huku mitaani matatizo yetu kana kwamba ni mageni na hawakuwahi kuyasikia? Kwa nini wasikae chini waksema enough is enough. sasa tunataka kubadilisha maisha ya mtanzania wakakaa na wakachukua uamuzi bila kuhiatjai kuja mitaani kulia na kulalamika na wananchi wakati wao ndio baba na mama? Wanamlalamikia nani?
Ni lini CCM wataacha haya maigizo na kuhaingaikia shida za wananchi kwa dhati bila unafiki? Wapinzani walalamike na nyie mlalamike? Vipi? CCM tunataka vitendo sio maigizo! Kiongozi mkuu kabisa wa chama huhitaji kuzunguka mikoani kuwaita mawaziri wako ambao kimsingi ni wewe uliyewateua (kwa sababu katibu mkuu na mwenyekiti wa chama wanshirikiana kwa ukaribu kushauriana kuhusu nani ateuliwe) ni mizigo. Huku ni kuwahadaa wananchi. haiwezekanai baba unapita mitaani unamlalamikia mke wako.. oo sijui huyu mwananmke yuko hivi na hivi, oo sijui hafai, sasa si umuache si una maamuzi wewe ya kumuacha km umeshindwa kumrekebisha?
kwani hao mawaziri waliwekwa na vyama vya upinzani? Si mliwaweka nyie? Sini makada wenu? Sasa kwa nini km wanaharibu msiwatoe mnakuja kutulilia sisi wananchi? Vitambi vinazidi kuongezeka huku mnajidai mnawalilia wananchi? Inawezekanje wewe kuwa unaumizwa na matatizo ya wananchi huku kitambi kinazidi kuongezeka? kweli nape? Hulali ukiwaza namna ya kutatua kero za wananchi wakati huo huo likitambi linazidi kumea? Are you serious? C'mon let's be serious!