CCM na jipu la ardhi: ofisi ya ccm karibu na kwenu ipo ktk kiwanja halali

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Maeneo mengi nchini ofisi za ccm zimejengwa ktk maeneo ya wazi au maeneo yasiyokuwa rasmi! Ktk eneo ninaloishi Mimi, kuna ofisi 4 za shina za ccm ambazo zote zipo ktk maeneo ambayo awali yalijulikana kama maeneo ya wazi! Na kwa bahati mbaya jinsi ofisi hizo zilivyokaa utaona tu kuwa wao wapo tofauti na wakazi wengine ktk maeneo hayo, maana hii ni mitaa iliyopimwa so sio rahisi kwa kiwanja kimoja kuwa nje ya line za kawaida kwa wakazi wote!
Serikali ya ccm ioneshe uwajibikaji kwa vitendo kwa kurejesha maeneo hayo ya wazi ili na wananchi waliojenga kiholela wasione taabu kuhama linapokuja suala la kuwatoa ktk maeneo yaliyovamiwa!
Mdau hebu iangalie ofisi ya ccm mahali pako na useme kama ilistahili iwepo mahali hapo!
 
bila kupepesa maneno..kama wamejenga kwenye eneo la wazi watoke mara moja.

CCM si chaka ama kimbilio la mafisadi.
 
Hongera mkuu kwa kuliona hilo maana ni kweli kabisa ofisi nyingi za ccm zilijengwa katika maeneo yaliyokuwa ya wazi.Serikali iache unafiki jipu hilo nalo walishughulikie.Na kwa kuwa mwezi huu walalahoi wengi wanatarajiwa kubomolewa nyumba walizojenga mabondeni uzi huu kwangu nauchagua kuwa uzi bora wa mwezi kwani unaonyesha undumilakuwili wa serikali katika maamuzi yake mengi.
 
Wameiba kipande cha kiwanja cha shule, pale Ubungo Msewe, nakumbuka lilikuwa eneo la choo cha shule miaka ya 76. Pia sasa wako katika mikakati ya kupora eneo la serikali ya mitaa.
 
Back
Top Bottom