CCM na Itikadi ya Kujuana na muda wa nyongeza katika kuleta Maendeleo Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Itikadi ya Kujuana na muda wa nyongeza katika kuleta Maendeleo Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Jan 19, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nikijibu hoja ya kuhusu Rafiki yangu January Makamba kwenda Bumbuli kutoa magari, kuna mtu alitoa kauli na kuainisha kuwa January, Baba yake Mzee Makamba ni mtu mwenye ushawishi Serikalini. Nikauliza Ushawishi na kujuana kunasaidiaje mtu kuwa kiongozi mzuri, mwenye tija, juhudi, maarifa na ufanisi?

  Sasa nikiwa naendelea kutafakari hilo, Wabunge wawili wameibuka na kutoa kauli kudai kuwa wao wanafaa kuendelea kuwa viongozi kutokana na jinsi walivyojenga mitandao ya ndani na nje ya marafiki ambao huwasaidia hawa Wabunge katika shughuli za MISAADA kwa majimbo yao kama sehemu ya kujipatia ujiko wa kuwa ni Urafiki wao na Kujuana na Watu ndiko kunakochangia maendeleo ya Majimbo yao.

  Waheshimiwa Marmo na Kaboyonga wakijibu hoja ya Wabunge kuwekewa muda maalumu wa kuwa Wabunge walikaririwa wakisema hivi

  Najiuliza, kwa vijisababu walivyotoa hawa Wabunge ambavyo narudia tena naamini ndio taswira halisi ya asilimia 95% ya Viongozi wa CCM (Wabunge, Mawaziri, Wajumbe wa NEC, CC, Viongozi wa Mikoa nk.), je tunafaida gani kama Taifa kuendelea kuamini kuwa CCM ni chama Mbadala ambacho kinaweza ifikisha Tanzania katika maendeleo ya kweli na kuvuka daraja la kuwa nchi tegemezi kwa misaada na kuushinda umasikini?

  Labda niulize, jimbo la Marmo na la Kaboyonga, yamekuwa chini ya himaya ya CCM tangu tupate Uhuru. Je kila baada ya miaka mitano ambao CCM imekuwa ikinadi Wabunge na Rais katika majimbo hayo, imekuwaje kila mbunge aje na ajenda yake na mipango ya maendeleo ambayo ni huru na si kufuata mchakato wa Ilani ya Chama chao?

  Ikiwa Kaboyonga anadai kuwa Tabora mjini imeshindwa kupata maendeleo kutokana na kubadilishwa Wabunge na Marmo anadai kuwa maendeleo wilayani mwake yametokana na "connections" zake binafsi, je kweli watu hawa wanafaa kuwa Viongozi na CCM inafaa kuendelea kuaminiwa?

  Hivi katika majimbo ya hawa ndugu wawili, ni lini wamekwenda kuhamasisha Uzalishaji mali na shughuli za maendeleo bila kuwa ombaomba au kudai wanahitaji muda?

  Je Kaboyonga anapodai kuwa miaka mitano ya kwanza ya Mbunge ni kujifunza taratibu za Bunge na Sheria, ina maana kama jimbo na Taifa tunapoteza muda na fedha zetu kama walipa kodi na kuchapa miguu (makitaimu) tukisubiri mtu, watu au kikundi ambacho kilijinadi kuwa kina uwezo wa kuongoza na kuleta maendeleo kumbe wanahitaji kupigwa twisheni?

  Sasa kwa kauli ya kusema miaka mitano ya kwanza ni kujifunza kazi, kunaonyesha wazi kuwa Watu wengine hukimbiliakuwa Wabunge hata kugombea Urais bila kujua awali ni majukumu gai wanayopaswa kufanya na zaidi ni kuwa wanaupungufu mkubwa wa kiakili na sifa za uongozi kwa madai yao kuwa miaka ya mwanzo ni kujifunza kazi.

  Je kuhamasisha Wananchi wachimbe mifreji, wajenge barabara, wasafishe Mazingira, wapeleke watoto shule, waongeze ufanisi na kufanya kazi kwa bidii iwe ni mashambani, viwandani au maofisini kunahitaji mafunzo ya namna gani na ya muda gani ili Wanajimbo wasikae mguu pande wakimsubiri Mbunge wao afuzu darasa la Uongozi?

  Nikirudi kwenye kauli zao Marmo na Kaboyonga kuwa wao wameleta maendeleo majimboni mwao kutokana na "Connection" za ndani na nje, je ni nini tafsiri ya Maendeleo na ni maendeleo ya namna gani waliyoyaleta kwa kutumia "Connections"?

  Je wanaweza kutuambia masharti ya "Connections" zao ambazo hayatafikia kuhujumu nchi au kuingiza dhululma? Je wanaweza kutuambiakuwa "Connections" hizi ni huru hazina mkono wa Takrima na ufisadi na je wao Marmo na Kaboyonga watalipa vipi Ufadhili na Fadhila za hawa "Connections" wa ndani na nje ya nchi?

  Je kujenga vyoo, kutumia samadi na mbolea, kulima kwa usatadi na kisasa, kuzoa takataka, kusafisha mazingira, kulisha mifugo, kujikinga na maradhi, kuishi kwa maadili, kujituma, kutumia juhudi, kuwa na maarifa, kuongeza tija na kuhamasisha ama kwa motisha au kauli ni lazima tuwe na "Connections na Network" kufanikisha hilo?

  Zi wapi zile kauli na msukumo wa Viongozi kujumuika na Wananchi kuzalisha mali na kuwa mfano wa kuigwa na kujenga jamii inayojitegemea? Je Viongozi wa namna hiyo tumewapoteza kabisa na Mzee Simba wa Vita alikuwa ndiyte pekee aliyebakia?

  NI aibu na inasikitisha jinsi ambavyo kila Mbunge anavyokimbilia kujenga "Connections na Network" za marafiki wa nadni na nje eti kuleta maendeleo jimboni!

  Je ina maana hamuiamini Ilani yenu wenyewe na mipango ya kimaendeleo na Bajeti mnayowaundia Watanzania kila mwaka?

  Hizi "Connections na Network" zenu ndizo zilizotuletea EPA, Meremeta, Richmond, IPTL na matakataka mengi tuu hata hili la leo la Kilimo Kwanza na Matrekta kutoka India!

  Mnauza uhuru na fikra za Mtanzania kwa kudhania kuwa mkitembeza bakuli nje na ndani ya nchi, basi ile misaada na sadaka za wenye fedha ndio zitakazoleta tija na maendeleo kwa nchi yetu.

  Mbaya zaidi ni kuwa mfumo huu wa "Connections na Network" umekomaa hata kuzidi kwenye nyanja ya siasa. Angalia kila NGO, Makanisa, Misikiti na Taasisi nyingine, kila mmoja inategemea "Connections, Network na Ufadhili" wa Nchi, Taasisi, NGO, Dayosisi au Madrass fulani iliyoko nje ya Nchi ili eti tupate maendeleo!

  Je ni lini tutaanza kujivunia maendeleo na matunda ya uhuru wetu kwa kutumia Jasho letu wenyewe bila kumtegemea mtu au kutoa rehani Uhuru wetu kisa tumepewa vitanda vya Zahanati, Vitabu, Mashuka, Baisikeli, Pembejeo, Visima na mengineyo mengi ambayo tunavishangilia kwa jina la msaada wa Wafadhili?

  Ni wazi kuwa CCM ni chama kilichojaa watu wanaotoa kauli lakini si Wachapa kazi!

  Ni dhahiri kuwa ndani ya CCM kuna ukosefu mkubwa wa Watu wenye uwezo wa kuwa Wabunifu wa maendeleo na kuyafanyia kazi kwa nguvu na jasho lao wenyewe na mtji wao bila kungoja msaada au kukimbilia kutegemea ufadhili!

  Ni ukweli usiopingika kuwa kushindwa kwetu kama Taifa kuendelea mbele katika vita dhidi ya Ujinga, Umasikini na Maradhi, kunatokana na Udhaifu wa hali ya juu wa Chama Tawala CCM, kwa kuwa kimekosa dira, mwamko na msisimko wenye nishati ya uchapakazi!

  Je ni miaka mingapi mingine tuvumilie na tuwape CCM nafasi ya wao kuendelea kupoteza muda wetu na kuvujisha hazina yetu ili kujifunza kazi, kufanya majaribio na kuendelea kutafuta "Connections na Network" za kuleta maendeleo kwa Taifa letu?

  Mwaka huu wa 2010, ni mwaka ambao ama tutasuka au tutanyoa, tutakua na kukomaa au kudumaa MILELE!
   
 2. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev. kawaida ya wanasiasa (hasa wa bongo) ni porojo tu hakuna lolote la maana. Ubunge kwao ni ajira ndio maana wanaogopa kuachia kwa visingizio visivyo na kichwa wa miguu!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Januari ametoa magari huko Bumbuli? au I am missing something hapo?

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kidudu Mtu,

  Porojo hizi tumezisikia kwa miaka karibu 50 sasa, ni wakati umefika heri tuwe na sura mpya kabisa katika kila jimbo tujue moja!

  Ni heri tuanze upya kwa sura mpya maana hizi za kina Marmo au Kaboyongana wengine ambao wameng'ang'ania kuwa wao ni pekee walio mabingwa wa kuweza kuleta maendeleo majimboni mwao hazitufikishi popote.

  Jaribu kutafakari Mbunge ambaye anajitapa kuwa amekuwa Mbunge kwa miaka 25 na jmboni kwake mpaka leo kuna watu hawana hata choo au maji safi! Je itawachukua miaka mingapi kujenga vyoo na watu kupata maji safi? Je tukimbilie Japan kwenda kuomba watujengee vyoo?
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hivi kwani kazi za Mbunge ni zipi? Na hela za kuwajengea wananchi wanavyohitaji anazipata wapi?

  - Labda tukiweza ku-establish hilo ndio tunaweza kuwahukumu wabunge wetu, maana si pia kuna na role ya wananchi katika jimbo, ni ipi hiyo? Maana eti na choo nacho ni kazi ya mbunge?

  Respect.

  FMEs!
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa kunisahihisha, ni pikipiki na si magari. Ama habari ilidi kapeleka mipira na misaada mingine kwenye hilo jimbo.
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  FMES,

  Mbunge makini na mchapa kazi, hutumia nyenzo za ndani, nguvu za ndani na rasilimali za ndani kulijenga jimbo lake. Hili linawezekana kupitia uhamasishaji, kuwa na mipango bora inayowiana na malengo ya kichama na serikali ya kimaendeleo.

  Fedha za kuratibu maendeleo na kugharamia shughuli za maendeleo kiutendaji zinatoka Serikali kuu. Aidha kila jimbo lina uwezo wa kujipatia mapato ya ziada kupitia kodi na mauz ya bidhaa zinazozalishwa katika eneo na hivyo kuwezesha kuneemeka kwa sehemu.

  Ukiangalia kwa makini, fedha kutoka Serikali Kuu kupitia TAMISEMI, zimelenga sehemi za matumizi ya kawaida ambayo ni shughuli za kiutendaji (Administration) na za Kimaendeleo ambako huku ndipo kuna mambo ya Shule, Vituo vya Afya, Miundombinu, Maji na mengineyo.

  Kwa upande wa Choo, hilo ni jambo la Mbunge kuwa mfuatiliaji wa makini kuhakikisha kuwa jimbo lake na watu wake, wanajizatiti na kuishi katika mazingira bora na safi!

  Ndio maana Wabunge wanapaswa kuwa na uwezo wa kujua ni wanafunzi wangapi wa shule wanaelimika na hata kufaulu mitihani, kufuatilia takwimu za vifo vya watoto wadogo na mama wazazi na mengineyo mengi yanayohusu jimbo ili kuwa na jimbo lenye watu wenye afya.

  Nimeleta mfano mdogo wa Choo kama kiashiria kuwa kuna baadhi ya mambo madogo madogo ambayo wala hayahitaji Bajeti ya Serikali au Msaada wa Mfadhili, bali ni vitu vya kufundishana ndani ya Serikali ya majumbo na kuhakikisha Serikali za Kata na Vijiji vinafanya ufuatiliaji kuhakikisha watu wanajenga vyoo madhubuti na hawaendi ku nya ku-nya ovyo barabarani au popote wanapotaka kwenda haja.

  Nilipokuwa Tanzania mwezi wa Oktoba mwaka jana, kulikuwa na habari kwenye gazeti moja ambayo ilinifanya nihamaki na kuuliza kama kweli Tanzania tumefikia mahali kama hapo kuwa mwamko wa kujituma hatuna na tunategemea wafadhili.

  Kulikuwa na habari kuwa kwenye wilaya moja, watendaji walikuwa wanaomba msaada wa Wafadhili kujenga vyoo kwa ajili ya Waalimu wa Shule za Msingi. Ombi hili lilifanyika Kitaifa na kutangazwa na vyombo vya habari. Nikajiuliza, iweje kuchimba vyoo nako tutegemee wafadhili?

  Kwa kifupi Bwana FMES, nazungumzia wajibu wa Watu kujituma na kuachana na tabia ya kutegemea misaada! Imekuwa ni tabia ya kawaida sasa kwa Watanzania kutegemea misaada na kwenda kila kona dunia hii kujenga urafiki ili kupata misaada.

  Sasa swali langu ni hili, ikiwa Mbunge anaona kuwa Serikali Kuu haipeleki maendeleo au kutumia fedha vizuri kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya/Jimbo lake, kwa nini kila mwaka Mbunge huyu na wenzake wanaafiki kupitisha Bajeti ya Serikali ambayo haitumiki ipaswavyo kwa manufaa ya Wananchi?

  Je Mbunge wajibu wake ni nini ikiwa hawezi kutumia nafasi yake kikatiba kuiwajibisha Serikali kwa kupitia na kutumia taratibu na haki aliyopewa kisheria na kikatiba?

  Sasa kama Mbunge katika jimbo atakuwa na kauli kama za Kaboyonga au Marmo na kuona kuwa ni heri aende nje ya nchi kwenda kuomba fedha za kununua madawati kisa hakuna mgao kutoka Serikali yake au ameshindwa kuhamasisha Wananchi wajizatiti wajinunulie madawati, huoni kuwa huyu Mbunge hafai kuwa kiongozi ?

  Hata kama tutadai Mbunge huyu kafanya hilo la kwenda kutafuta misaada kwa nia nzuri, kushindwa kwa Mbunge huyu kudai haki ya Wananchi wa Jimbo lake na kusimama kidete kukataa kuyumbishwa na Serikali au Chama kumkalisha kikao ili abariki matumizi na bajeti ambayo haijali watu wa jimbo lake, bbado kunaleta picha mbya inayoonyesha kuwa Mbunge huyu ama hajui wajibu na haki yake au basi naye anaridhika na uendeshaji wa Serikali ambao haulengi kuleta maendeleo kwa Mtanzania mvuja jasho na mlipa kodi.

  Hii ndio taswira ya Tanzania na kikubwa imelelewa na CCM kwa kuwa mtaji wa Umasikini na Unyonge wa Mtanzania ni mavuno na Utawala wa Milele kwa CCM!
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Rev darasa zito sana, hebu niweke sawa pale kwenye jimbo kuweza kupata hela za kodi za mauzo yao, sheria ainasema nini hapo maana ndipo hasa kwenye uzito mkubwa wa hela za kuwasaidia wananchi na majimbo, I mean majimbo yetu yenye madini vipi nayo yana hiyo priviledge!

  - Darasa zito sana mengi ni kweli sana, lakini bado wabunge wengi wanaumizwa na political system tuliyonayo, mbunge akizuia bajeti ya wizara basi ujue huenda asirudi bungeni kwa kunyimwa na chama chake, tumeona Spika akisulubiwa bila huruma kule NEC, it took wafadhili kuingilia kati, wakati sisi wananchi tukiikaa pembeni na kubishana kama yaliyotokea ni kweli au sio,

  - Sasa unapokua na wananchi ambao hawawezi kukuunga mkono inapobidi, unaweka ujasiri wa nini? Maana kama kweli tungekwua tunathamini kazi ya Spika wa sasa kutusimamia wananchi, basi angalau tungeandamana, sasa hiyo ni mifano tu ya ni kwa nini sio kosa la wabunge, ila huenda ni letu wananchi na kuridhika kwetu na political system tuliyonayo, au?

  Respect.


  FMEs!
   
 9. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakuu, hii topic ni nzito na nadhani swali kuu hapa ni

  Je wabunge waliokaa muda mrefu ndio bora au wabunge vijana??

  Kwa maoni yangu nadhani hapa inategemea na mbunge binafsi na jimbo binafsi, haiwezi kuwa blanket statement. Kuna baadhi ya wabunge wako bungeni miaka na miaka lakini majimbo yao yako nyuma mno katika elimu, afya, uchumi nk sasa hawa kwa kweli napendekeza wajiondoe au wananchi wawakatae na wajaribu mtu mwingine. Unakuta mtu alikuwa waziri muda mrefu tu lakini kashindwa hata kusukuma serikali kusaidia jimbo lake, huyu to me lazima atolewe.

  Baaadhi ya vijana wanaotaka kugombea wamekuwa wakijituma kwenye mambo mbalimbali, na wananchi wa majimbo wanatakiwa kupima kama hao watu wanavyojinadi wataweza kutekeleza mahitaji ya jimbo?? Je wataweza kuwa tayari kutoa ahadi ( au mkataba) na wananchi kuwa nitafanya a, b, c na nikishindwa baada ya miaka mitano nitoeni??
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tulipofanya mabadiliko ya Katiba mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vipya na hata baada ya lile Azimio la Zanzibar, tulipoteza nafasi moja muhimu sana nayo ni kubadilisha mfumo wa kuratibu mapato ya taifa na jinsi yanavyotumika.

  Tumeingia katika mfumo wa kibepari na kama sikosei, CHADEMA wanadai kuwa wakiingia madarakani wataleta mfumo wa majimbo na hivyo kurudisha mapato ya uzalishaji mali kwa majimbo.

  Nafasi tuliyopoteza na kupotezwa na wawakilishi wetu ni kuwa na majadiliano mapya na Serikali kuu katika kuhakikisha kuwa mavuno ya Rasilimali zetu, yanatumika kwa kiwango kikubwa katika kuzijenga na kutoa faida za kiuchumi kwa sehemu husika.

  Mfano, kule Mwanza na Shinyanga ambako kunavunwa dhahabu, au Songea, Mbeya na Rukwa wanakozalisha chakula, au hata Dar, Dodoma, Kigoma na Mtwara, palitakiwa kuwe na makubaliano mapya ambapo mapato yote yangegawanywa kati ya Serikali Kuu na Tawala za Mkoa (TAMISEMI) kwa makubaliano ya Asilimia ya mapato na si kile ambacho Serikali Kuu inadhani na kupanga kukigawa kwa mikoa.

  Si nia yangu kuleta mfumo wa Majimbo , lakini mgawanyo wa mapato ungelenga kuwafaidisha wazalishaji na kuwapa motisha ya kuongeza uzalishaji, kuona hali zao za kimaisha zinapiga hatua ya mbele na huduma za kijamii kama elimu, afya, chakula, maji, nishati na miundombinu ingeweza kufanikiwa kwa kuwepo kwa mkataba kati ya Tawala ya Mkoa na Serikali kuu kubainisha ushirikiano wa pande zote mbili katika kuleta maendeleo na vitendea kazi nilivyovitaja hapo juu.

  Ikiwa kama kungekuwa na mikoa ambayo iko kwenye machela, mfano uzalishaji wa Lindi hauwiani na Mwanza, basi ni jukumu la Serikali kuu kuwapa Mwanza gawio lao la mapato na Serikali kuu kujifunga mkanda na kuwapa Lindi gawio la nyongeza ili kukidhi mahitaji ya Wananchi.

  Mfumo tulionao sasa hivi unatoa mwanya kwa Serikali Kuu kupitia CCM kunyanyasa Wananchi na kuwanyima gawio la jasho la kazi zao na rasilimali za mahali pao. Ama Serikali kwa kuwa imejitwalia madaraka yote na kujiundia mfumo hasi, basi shughuli za uwekezaji na hasa kupitia wazalishaji wageni vinakuwa vimewekwa bila ushirikishi kamilifu wa Wananchi na ndio maana haishangazi kusikia TIC na Ole Naiko wakipanga viwango vya mapato ya kodi na ushuru na hata kutoa misamaha kwa Wawekezaji na kuwaacha Wananchi wa sehemu husika Solemba.

  Aidha mfumo huu wa kiuzalishaji ambao unadhibitiwa na Chama cha Kisiasa kupitia Serikali, ndio unaozalisha viongozi na wawakilishi ambao hujiona ni Miungu na kuwa na dhana potofu na kukosa motisha wa kujituma kufanay kazi kama jinsi majibu ya Marmo na Kaboyonga yanavyoonyesha.

  Viongozi kama hawa ni rahisi kuuza utu wao kwa vikao vya Chama vya kutiana masingi badala ya kusimama kidete na kutetea haki ya mwananchi. Jambo hili linaturudisha kule kule tulipoongea na Mwanakijiji kuhusiana na Wajibu wa Wanachama wa vyama kuwa ni kwa Vyama na si Taifa.

  Hivyo kunyanyaswa kwa Mbunge kwa kutumia kikao cha Chama kutokana na maamuzi yake ya Kitaifa na utendaji wa kazi yake kwa manufaa ya Taifa ni dhahiri na kutaendelea mpaka hapo tutakapokuwa na Wanasiasa wasio na woga na walio tayari kujitoa mhanga kumtetea Mtanzania na kuilinda Katiba ya Tanzania na si kufanya kazi na kuilinda CCM!
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kuwa watu wanafikiri tukiwapa Wawakilishi muda zaidi, watapevuka na kufanya kazi ipaswavyo!

  Jiulize yule Bingwa aliyejiandaa kuwa kiongozi kwa miaka 10 halafu alipopewa dhamana, akaduwaa na kushngaa feri kama vile hajui alichopaswa kufanya!
   
 12. J

  Jekyll+Hyde Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo nakupa tano mkuu, uliyosema yote ni nakubaliana na wewe
   
Loading...