CCM na dhana ya kujivua gamba

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Huyo Lowassa majuzi tu wana CCM wenziye walitulazimisha tuamini kwamba yeye ni gamba akiwa pamoja na Rostram Aziz na Andrew Chenge vipi leo eti Lowassa huyo huyo amageuka kuwa eti ndiye mtu anayefaa kutuongoza hadi eti kwenye nchi ya ahadi?

Lowassa huyu huyu kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 jina lake lilitolewa kwa aibu katika ngazi ya interview leo eti jana anatulazimisha tuamini eti kura hazikutosha Lowassa katika kipindi kile alipigiwa kura na nani wakati alifukuzwa ? (kwa lugha ya staha jina lake liliondolewa kwa kukosa sifa).

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 Lowassa hakuchukua form akijua wazi kabisa mzimu wa mwaka 1995 ungemtafuna kwa hiari yake mwenyewe akakubali kuwa mpiga debe wa JK leo eti jana anatulazimisha tuamini eti walikaa kiti na JK wakakubaliana JK aanze yeye atamalizia, kwa makubaliano hayo hii imekuwa ni nchi au papai ambalo watu wanaweza kugawana nusu kwa nusu.

Kwenye kashifa ya Richmond ni Lowassa ndiye aliibuka kinala wa kashifa ile hadi ikapelekea yeye kuwajibika kwa kutokutimiza wajibu wake ipasavyo, ni kwa bahati tu cheo cha uwaziri mkuu mtu anaweza kuwajibika sasa leo anavyodai eti yeye ndiye anayefaa kuwa rais asipotimiza wajibu wake wa urais ipasavyo kama alivyofanya kwenye uwaziri mkuu tutakuja tufanyeje watanzania? Tukae chini tulieee hadi mda wake ufike aondoke, tuanze kuishi kwa matumaini hadi mada wake wakuondoka madarakani ufike ndiyo hiyooo safari yake ya matumaini anayosema.

Mzee Kingunge nae nina kila sababu ya kumwambia anazeeka vibaya , wakati serikali inamny`ang`anya tenda yake ya kinyonyaji na yakifisadi ya kukusanya ushuru stand ya mabasi ubungo alilalamika sana kwamba serikali imemhujumu yeye na familia yake, sasa jana akawa ndiye dodoki wa kumsafisha Lowassa anataka tuelewe kwamba mafisadi kwa mafisadi wanasafishana?

Kwa alichofanya Lowassa jana ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu, kujifanya yeye yuko juu ya chama na kukigeuzageuza chama anavyotaka mithiri ya Messi anavyowageuzageuza walinzi wa timu pinzani, sasa nasema kazi ni moja tu KUKATA JINA LAKE.

Chama cha mapinduzi ni taasisi siyo mtu mmoja,CCM ndicho maarufu siyo Lowassa, nguvu ya Lowassa iko ndani ya CCM akitoka nje ya CCM Lowassa ni mwepesi kama karatasi, alikuwa maarufu Mrema ndani ya CCM aliondoka CCM wala haikuteteleka, jina la Lowassa litakatwa aende kokote anakotaka.

Kangi Lugola mbunge ndiye pekee akichukua mike kumpigia debe Lowassa falisafa yake ni nini? Kangi Lugola na Deo Filikunjombe ni mabunge wanaomiliki majimbo ni wabunge ambao akienda chama chochote atapata ubunge , Kangi Lugola alifanya hivyo akimananisha kwamba lolote na liwe siyo Lowassa au mbunge mwingine, Lowassa akikatwa jina kwingine hatopokelewa aelewe hili tafadhari.

Philip Mangula mguu sawa tayarisha kalamu na rula kata jina la Lowassa kwa ukosefu wa maadili uliokithiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom