CCM na demokrasia ya kununua wapinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na demokrasia ya kununua wapinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jul 16, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni limezuka wimbi la kuwarubuni wapinzani hasa viongozi kujiunga na chama cha mapinduzi kwa njia mbalimbali zikiwemo pesa na ahadi,
  sina haja ya kutaja matukio ambayo pengine na wewe unayashuhudia yakiendelea kutokea kwa baadhi ya madiwani wa upinzani kurubuniwa.

  Sijui kwanini hii hali inatokea sasa au labda ni baada ya Chama cha Mapinduzi CCM kuona kinazidi kupoteza mvuto mbele ya wananchi
  siku hadi siku au ni baada ya kuhisi filosofia yao ya kujivua gamba waliyoianzisha haijapokelewa kama walivyotarajia.

  Najaribu kujiuliza hii demokrasia mpya ya kulazimisha a forced democracy imetoka wapi na inatupeleka wapi, na je hii demokrasia itakisaidia chama au ndiyo inakididimiza zaidi, je wapinzani wamejipanga vipi kukabiliana na wimbi hili ambalo linatishia uhai wa vyama vyao.

  Je hao viongozi wenye tamaa hiyo naweza kuwaita waroho jamii iwafanye nini pindi wanapobainika kwa sababu wanakera wanaudhi na wanarudisha nyuma maendeleo chukulia mfano wa sakata la madiwani wa Arusha.

  Na mwisho je ni halali kwa chama kutumia mbinu hii kuvutia wananchi? katiba inasemaje, vipi msajili wa vyama anaafiki maana sijasikia akikemea jambo hili. Nimeongelea CCM zaidi lakini sina maana kuwa vyama vya upinzani havirubuni wanaCCM kujiunga navyo kwa njia ya pesa. Naomba kuwasilisha.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,025
  Likes Received: 3,051
  Trophy Points: 280
  Uko sawa kabisa na kwa mfano ishu ya Mbeya na Arusha ni mkakati wa kukichanganya CDM ili kipoteze utulivu,mvuto na wapoteze mda mwingi katika kutatua matatizo ya chama na hatimaye washindwe kufanikiwa kwenye commonness ya maandamano na masuala mengine kama kudai katiba mpya n.k

  Naishauri CDM itulie igawe majukumu kwa maafisa/makamanda wa chama katika kufanya mgawanyo wa majukumu mbalimbali kulingana na mipango ya chama kwa mwaka huu ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali,na pia ningeshauri chombo cha kusettle peace na harmony ndani ya chama ipewe umakini mkubwa ili kuweza kuovercome fitina nyingi ambazo inaonekana CCM wanaziratibu kitaalamu sana ili kuweza kuidefeat CDM

  Nahisi mengi yatatengenezwa ila CDM hatutakiwi kuyumba na inatakiwa hili lieleweka vizuri kwa wanachama na wananchi ili kuondoa hofu ambazo wanachama wanaweza kuzipata kwa yanayotokea/yatakayotokea
   
 3. p

  plawala JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dawa ya tatizo hilo ni elimu ya uraia iliyokamilika,kwa sababu katika haya manunuzi walengwa huwa ni viongozi katika nafasi zao hasa madiwani,wabunge,wenyeviti wa vyama ambavyo vina nguvu nk

  Viongozi walionunuliwa huwa hawajifichi, kwa hiyo dawa yake ni kupigwa chini,ndipo utakapokuata zoezi zima linakosa mvuto na wawekezaji ktk hiyo biashara kwisha kabisa

  Dawa kama hjiyo itawafaa wagombea ambao huwa wanahonga ili kununua wapiga kura,mgombea akitoa fedha ili kupewa kura asipopewa ndiyo mwisho wake
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani hili iwe alert kwa vingozi wetu wa cdm, now that we know CCM's strategy to lure cdm leaders, viongozi wa ngazi ya za juu katika chama wanapaswa kuwa makini katika kuwaelimisha viongozi wao wa ngazi zote na wanamchi kwa ujumla....watu tusidanganyike na kupoteza focus. Watanzania wanaendelea kuumia every single day mostly kwa sababu ya utawala potovu wa CCC, je mpaka lini? CDM ndio tumaini la wengi, kwa hiyo viongozi msinunuliwe na kutuuza sisi wanyonge
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hili jambo watu wengi humu tunaweza kulielezea kwa uchungu sana maana linavunja matumaini ya kuiona Tanzania mpya.

  Nadhani jambo hili lichukuliwe na wananchi wenyewe wawaajibishe viongozi wanaoiiomba kura halafu baada ya muda wanauza uongozi waliopewa na wananchi kwa kupokea rusha kutoka kwa magamba.


  Nadhani hii ni rushwa sawa na rushwa zingine japo hii inaumiza wananchi wengi na inarudisha nyuma harakati za watu kujikomboa.


  Kuna habari ya diwani huko mbeya kutaka kufanya kitu kama hiki na wananchi wakamwambia watamkata kichwa ameamua kufuta kauli kwa kuandika barua nyingine ya ku recall wamuzi wake.

  Nadhani wananchi waelimishwa kuwa wananpompa mtu uongozi haina maana kwamba ni mali yake anaweza kuutumia kuuweka rehani akapata hela na kudai amejihudhuru. Ni lazima chama kama chadema wawe wakali na jambo hili kwa kuwapa wananchi mamlaka ya kuwasulubisha watu kama hawa mara wanapobainika kuwa na mbinu za kuuweka uongozi waliopewa rehani.


  viongozi wengi wa cdm hasa madiwani na wabunge bado hajajua kuwa wameupata uongozi huo kwa sababu ya chama na si kwa umaarufu wao. Wananchi wanachagua chadema na si mtu , kuna sehemu hata ukiweka gogo watu watachagua madam linagombea kwa tiketi ya chadema maana wamechoka na ccm.  Tumeona mtafaruku wa madiwani huko Arusha nao ni mtazamo wa madiwani hao kudhani kuwa wao wako juu kuliko cham. Sasa wameanza kupata fundisho baada ya juhudi zao zakutaka kuungwa mkono na wananchi kugonga mwamba kwa kushindwa kuwashawishi watu kufika kwenye maandamano yao na ccm kwa ajili ya kujipongeza kwa upuuzi wao.  Nadhani cdm ni welevu kuliko ccm, hivyo watashinda vita hivi kiurahisi kabisa.
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ngonini

  Pamoja na wananchi kuelimishwa pia elimu kubwa inatakiwa kupewa viongozi kuwa cheo alichonacho si mali yake ni mali ya wananchi wapiga kura na endapo atakiuka makubaliano awe tayari kusulubiwa. Na uongozi wa chama kilichompa dhamana kiwe na utaratibu wake wa kuwafuatilia viongozi kama hawa toka mwanzo kabla ya uteuzi na utaratibu wa kuwaadhibu ili kuwa fundisho kwa wengine.

  Nakumbuka kabla ya uchaguzi CDM waliambiwa wanabeba makapi ya CCM kuna watu walipinga mtindo huo wakabezwa lakini leo tunajionea wenyewe viongozi waliopatikana kwa njia hiyo mfano wa Shibuda, kwa hiyo chama kiwe na utaratibu unaojulikana na si kusubiri siku ya uchaguzi na kukurupuka. Sitashangaa kwa mfano kusikia CDM hadi leo haina mgombea mwenye sifa jimbo la Igunga wanasubiri watakaotemwa na CCM, mtindo huu si mzuri na unarudisha nyuma si maendeleo tu ya chama bali ya wananchi wa sehemu husika, mtu unachaguliwa leo baada ya siku mbili unasema unajiuzulu haileti picha nzuri kwa waliokuchagua.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Better you put evidence kuliko hizi porojo zako ulizotuwekea hapa halafu mavuvuzela yakasupport kama kawaida yao. Non sense thread.
   
 8. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nafikiri maadili ya uongozi ni muhimu sana. Madiwani wengi waliopo vyama vya upinzani wengi wao hawana ile elimu ya uongozi na baadhi yao si wanasiasa halisi. Chadema imepata umaarufu sana katika kipindi cha bunge la 9, baada ya operation sangara na baada ya kuwataja watuhumiwa wa ufisadi. Kutokana na umaarufu huo CDM kilihitaji kusimamisha madiwani wengi na wabunge wengi ili kupata viti vingi vya kuchaguliwa. Kutokana na ukata wa wagombea, mtu yeyote aliyesimama kwa tiketi ya cdm hata kama hakuwa mgombea makini alikuwa na nafasi ya kushinda kutokana na umaarufu wa chama. Hivyo basi kwenye msafara ya mamba na kenge wakawemo.

  Cha kufanya sheria zifuate mkondo wake pale itakapo bainika vitendo vya hongo vimefanyika. Wananchi nao wanayo haki ya kuwashughulikia hao madiwani kwa jinsi wanavyoona inafaa, maana waliwaamini na kuwapa dhamana ya kuwawakilisha.
  Jambo jingine ni CDM kuharakisha mpango wao wa chuo cha maadili ya uongozi ambacho mzee Sabodo alitoa fedha kusaidia uanzishwaji wake. Hii itasaidia kuwapa mafunzo viongozi wa chama waliopo uongozini na wanachama wanaotarajia kugombea hapo baadae.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nashukuru, hapa sihitaji support kama unavyofikiri nahitaji maoni ya watu yawe positive au negative, anyway thanx for your comment.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda si unawajuwa kwa kulalamika?
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Joss asante

  Maadili ya uongozi-umenikumbusha kitu muhimu sana kuwa CDM wana mpango wa kuanzisha chuo hicho maana wengi wa wagombea mfano wa CDM walikuwa ni wa kutafuta kuulizana nani anaweza au fulani anajulikana sana kwa kuuza mahindi sokoni basi ngoja agombee bila kuwa ethics za uongozi.

  Ni kweli unavyosema elimu na background ya wagombea wengine inaweza kuwa tatizo lets say ndogo haiwezi kuhimili mikiki mikiki ya kisiasa hasa ya kipindi hiki akiona polisi basi anaanza kujihisi makosa labda aliyoyafanya nyuma nk.

  Pengine ni uchanga kiumri na kiuwezo say kipesa unakuta labda diwani ndiyo kwanza kamaliza shule au hajawahi kushika 1M cash akipewa 3M anaona nyingi mno. Pengine inawezekana baada ya uchaguzi chama kimekuwa mbali naye anakosa msaada wa karibu kwa hiyo akipata mtu au chama cha kumtwist kidogo tu anasahau majukumu yake. Haya yote yanaweza kuwa sababu ya kwa nini viongozi wanarubuniwa.
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  plawala

  Kweli dawa ya hawa ni kupigwa chini lakini kumbuka akishaingia kumtoa huwa ngumu sana ni bora kumzuia kabla ya kuingia, akishaingia chama kinahitaji uangalifu wa hali ya juu kumtoa vinginevyo anaweza kuleta madhara, moja anaweza kuonekana ameonewa au waliomchagua wakasema sisi tumewapa mtu tuliyemtaka hatuna mwingine na mambo kama hayo.
   
 13. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Katibu wa vijana Jimbo la Mbozi wa Chadema Warren Kaminyonga akionyesha kadi yake
  kabla ya kumkabidha Nape leo kwenye mkutano Mbeya (kanunuliwa huyo)
   
 14. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  There is neither fair game nor moderator in a political arena my friend,just stick on the ball direction as the opposite team does.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Matukio kabla ya CCM kufanya mkuano Mbeya
  • Mbunge wa Chadema Mbeya (Sugu) kulazwa mahabusu na kufunguliwa mashtaka
  • Kuwahonga Madiwani wa Chadema Arusha kuwaingiza kwenye mwafaka kinyemela bila ridhaa ya viongozi wa chama
  • Kushambuliwa mchumba wa Slaa
  • Madiwani wa Chadema Mbeya kuhongwa ili waasi chama
  • Shule kushinikizwa kuhudhuria maandamano
   
 16. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  kaka hapo patamu cdm wamehongwa ngapi kwa kila diwani
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,798
  Trophy Points: 280
  upumbavu ni mzigo tena huelemea, na ujinga ni upupu, utajikuna mpaka m..at..a.koni mbele ya mkweo, si ajabu mpumbavu kujivika ujuvi kuwacheka werevu, mmesahau shetani anavyomkebehi muumba! upupu waweza poa, upumbavu kichwa chako labda utengane nacho!!!!!
   
 18. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni cccc wametufanya tuwe masikini kwa miaka 50 toka uhuru naiii inafanya baadhi ya watu ambao siyo makini wa kubali kunnuliwa kama uyo jamaa hapo juu umasikini wa tangu uhuru ndiyo unao msumbua na hata hao madiwani wa Arusha wame nunuliwa ili wajivua gamba wajisafishe yote chanzo ni fedhatufanye mabadiliko ya uongozi 2015 wana JF wote. Ili haya yote ya kununuliwa yasiwepo ivyi kwa akili ya kawaida hata kama siyo greater thinker kuna kipi kizuri cha kuhamia ccm 2naona mavyuoni wa2 wana jikana kuwa ccm eti huyo jamaa tena katibu mzima anaamiaa.wana JF kama mna profile ya huyo jamaaa nitumieni kidogo nimjuee
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kilichobaki CCM ni pesa tu hakuna cha sera ukimuuliza mtu itikadi ya chama chako ni nini atakwambia pesa
  ----wananunua madiwani
  ----wanasomba watu kuja kwenye mikutano na kuwalipa tuliona jana Arusha wanalipana waziwazi siku hizi hata ile haya hawana.
  ----wanalazimisha wanafunzi kuandamana nk nk

  kama wameshindwa kukiendesha chama kwa hoja za kisiasa na wanajiona wana pesa

  kwanini wasijibadili wawe CCM Kampuni tujue moja labda wataeleweka kwa urahisi.
   
 20. Ticha

  Ticha Senior Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kusema ukweli kinachokimaliza chama cha CDM ni wana CDM wenyewe.HUYU MKUU WETU ABADIRIKE,AACHE UJIMBO NA UMIMI,Tusipo angalia Mbeya atakosa Majimbo yote aliyopata.Labda yatabaki ya huko kaskazini tu.Wanachama si kuwa wananunuliwa na CCM,Ila Chama kimewasahau viongozi wa huko.
   
Loading...