CCM na CUF wamefilisika kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na CUF wamefilisika kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Jul 8, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kati ya urithi mkubwa aliotuachia baba yetu wa taifa Mwl. Nyerere ni umoja wa kitaifa. Umoja huu haukuja kama mvua bali alijenga misimgi imara ya kudumisha umoja wetu. Moja ya misingi hiyo ni kutoingiza udini na ukabila katika uongozi, serikali na siasa za nchi yetu.

  Mwalimu Nyerere alisema huku akishikashika pua kama kawaida yake anapoongea suala zito kuwa, mwanasiasa aliyefilisika kisiasa hukimbilia udini na ukabila ili aungwe mkono. Miaka sita tu baada ya kifo cha mwalimu Nyerere, CCM imefanya kituko cha mwaka kwa kuingiza masuala ya dini ya kiislam- Mahakama ya kadhi katika ilani yake ya uchaguzi. Kwa kufanya hivi CCM wamedhihirisha kufilisika kisiasa kwa vile wanatafuta sasa kura za kidini huku wakijua kuwa ni kuiangamiza nchi yetu.


  Tunajua wazi kuwa mahakama ya kadhi inahusika na mambo ya ibada za kiislam. Mashehe wameshasema kuwa mtume wao aliwafundisha kuwa mahakama ya kadhi inahusika na mambo ya ibada ndiyo maana watu wa dini nyingine hawatakiwi waamue masuala yao. Kumbe CCM na waislam wanajua kuwa mahakama hiyo inahusika na masuala ya ibada za kiislam, kwa nini sasa wanataka iiendeshwe na wananchi wote kwa kulipa kodi na kuingizwa katika sheria za serikali kana kwamba nchi yetu ni ya dini ya kiislam? Mambo ya ibada yanatakiwa yaendeshwe na waislam wenyewe na siyo serikali wala wananchi wote.

  CUF nao kupitia mwenyekiti wao Lipumba anasema eti CCM watekeleza kipengele cha mahakama ya kadhi huku akijua kuwa ni kuingiza masula ya ibada ya dini ya kiislam katika shughuli za serikali. Masuala ya mfungo wa ramadhani, ndoa na mirathi yamefungamana na ibada za kiislam. Ramadhani ni nguzo ya dini ya kiislam na ndoa za waislam zinaruhusu wake wengi, wakati dini nyingine hasa wakristo wanaamini katika mke mmoja. Sasa kwa nini CCM inataka kuwalazimisha watanzania wote hata wasio waislam washiriki ibada za kiislam ili tu wapate kura?

  Mbunge Msambya nae anadhani yuko bungeni kueneza dini ya uislam, na anafikiri anawakilisha bungeni waislam pekee. Ngasongwa naye anatumika kuingiza udini katika ilani yaCCM pamoja na usomi wake.

  Kwa kukumbatia udini CCM na CUF wamefilisika kisiasa na hawastahili kura zetu kwa sababu watatuletea utengano katika taifa letu na hivyo kuvunja umoja alioujenga baba yetu wa taifa.
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi huwa napata shida sana kuona kuwa eti mzee wa Kaya anasema kuwa alikuwa hajui ni nani aliweka kipengele cha mahakama ya kadhi kwenye ilani ya CCM. CUF pia kwa ushabiki wanasema kwa kusupport hilo.
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Chadema wanasemaje kuhusu MyK?...CUF na CCM kuunga mkono MyK ni MTAJI wa kisiasa ...tuelezeni chadema mnaunga MyK au la?
  Tamko la Chadema kuhusu MyK au wanasubiri wakamuulize "Maaskofu" I will be happy to know?
   
 4. j

  jumalesso Member

  #4
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninavyojua mimi Waislamu nao ni walipa kodi sasa kwa nini wasinufaike kwa kodi wanayolipa kwa kuona kwamba wanapata kuamuliwa mambo yao ya ndoa na mirathi kwa mujibu wa sharia zao? Lakini kodi hiyo hiyo wanayolipa inatumika na mahakama ambazo hazihukumu kwa sharia zao sasa haki iko wapi hapa? kama mnaona ubaya wa kutumika kodi basi ombeni zitenganishwe kuwe na sehemu ambapo zinapokelewa za waislamu tu lakini vyenginevyo hamueleweki ikiwa mnataka waislamu walipe kodi halafu itumike kuhukumu kwenye mahakama ambazo hawana ridhaa nazo hapo ni sawa kwenu sio? hekima iko wapi hapa?!!!!
   
 5. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Seif wa CUF naye ameunguruma, CCM na CUF ni wa kuogopa kama ukoma-wadini kwelikweli.
   
 6. A

  Albano Member

  #6
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ndugu yangu Jumalesso, kwa makusudi au kwa kutokufahamu anatuchanganya katika hili. Kulipa kodi ni wajibu wa kila Mtanzania. Lakini kuitumia hiyo kodi kwa ajili ya kunufaisha kundi moja la kiimani ni kosa kubwa na kwa nchi yeyote ile yenye mlengo wa kutofungamana na dini yeyote kama sisi ni tatizo kubwa. Naomba nikukumbushe kidogo kuhusu hotuba alizowahi kutoa Baba wa Taifa: alisema "Watanzania wana dini lakini Tanzania haina dini". Katika dunia hii ya leo kuanza kufikiria kufinance mahakama ya kadhi ili hali sheria zilizopo zimekidhi haja kwa kiasi kikubwa ni upuuzi usiovumilika. Kwa muono wangu sioni kama tutapungukiwa kwa kuto kuwa na mahakama hiyo; kwani toka tumepata Uhuru ni miaka zaidi ya 48 mtu aliyezaliwa miaka hiyo iliyopita tukimuuliza amekosa nini kwa kutokuwa na mahakama hiyo ya kadhi ninauhakika atatujibu hajakosa chochote zaidi tu ya ukubwa wa kuitwa kadhi mkuu nk.
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani waislamu wakubali kuwa myk siyo lazima na wameishi bila kuwa nayo kwa miaka zaidi ya 40. sasa huu uhitaji ambao umekuwa muhimu sana wakati huu unatoka wapi? Basi walete mchanganuo kuwa fedha za kuendesha zinatoka wapi, maana fedha za walipa kodi wote zinatumika kuendesha mahakama isiyo kuwa ya kadhi. Nadhani pia hi myk itakuwa source ya income kwa masheikh na ndiyo maana wanaishadidia.
   
 8. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyo ndio muasisi wa UDINI Tanzania. Baba wa Udini a.k.a Baba wa Taifa.
   
 9. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #9
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CUF ni chama cha kidini hili halina ubishi, CCM walichemsha kujaribu kucheza ngoma ya CUF 2005 kuingiza mambo ya Udini kwenye Ilani yao, leo wanamtafuta mchawi. CHADEMA wanajitahidi kujijengea taswira ya kitaifa hili wanastahili pongezi (makofi tafadhali).
  Maalim Seif nje ya wigo wa uzanzibar isomeke Upemba na Udini haoni zaidi ya hapo. shame on him.
   
 10. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani gharama za kuendesha mahakama ya kadhi ni kiasi gani ukilinganisha na umoja wetu??

  Mimi ni Mkristo ila naona iangaliwe njia bora na ya wazi ya kuijumuisha hiyo mahakama ya kadhi kwenye mfumo wetu, hata kwa kutumia kodi zetu. Wote si waTZ, mbona mafisadi wanakula kodi zetu na kina TRL lakini tupo tupo tu.

  kama ishu ni kodi sioni shida ila kama kuna sababu zingine za kisheria na kitaalam then zijadiliwe na mipaka iwe wazi.
   
 11. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You nailed them; YES WAMEFILISKA;

  Nashangaa watu wanaoomba CHADEMA itoe msimamo; mimi nasema hata huyo anayesema huwa anatoa msimamo vitu vyote visivyo mhusu? Chadema keep silence pls; tunawaheshimu na kuwategemea; pilipili isiyokuhusu yakuwashia nini; Chadema haina maslahi na MYK; ina maslahi na WATZ that all. Waache wafu wawazike wafu wenzao
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa kama ni hivyo mbona hakukiondoa.. mbona alijipigia debe kwa ilani hiyo yenye kipengele hicho na kukitumia kuomba kura!!!!
   
 13. M

  Mswahela Member

  #13
  Jul 24, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF ni UDINI tu hawana sera ya maendeleo;bahati nzuri Watanzania walio wengi wameshaelewa malengo na makusudio ya chama hicho. Ni chama cha Wapemba hicho hivyo ni aibu kwa Prof. wa Uchumi bw. Lipumba kuwa kiongozi wa chama kinachoweka mbele UDINI/uisilam. Maalim Seif jana alitia aibu kwa kudhani kwamba Watanzania hawana akili kwa yeye kukosoa waraka wa Wakatoliki kwasababu tu ni Wakatoliki bila kujali contents za waraka huo.Waraka huo ni maoni tu ya dhehebu hilo. Serikali inaweza kuukataa au kuukubali.Hakuna ubaya kwa madhehebu mengine nayo kutoa maoni yao.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Kweli umenena..tuache wafu wawazike wafu wenzao. Hii meli tunayoidandia sasa ya udini will get us nowhere.Infact, it is a sinking vessel. Tuna hiari ya kuchagua kuipanda au la, at our own peril!!!
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,380
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  cuf na ccm wana ndoa moja na ilani zao zinafanana''UDINI aka UISLAMU KWANZA''hii ndio ajenda kichefuchefu wanayoieneza.Pamoja na BAKWATA kuuamua kuusoma waraka kwa makini na kutangaza kwa waumini wake kuwa waraka huo hauna tatizo na unafaa,bado utamsikia Lipumba pamoja na kujifanya msomi anakomalia waraka lakini wakati huo huo anakwambia mahakama ya kadhi haina tatizo na anajaribu hata kuishurutisha ccm itekeleze ilani yake la sivyo cuf watatekeleza ilani kama hiyo.Kioja kingine kimetoka kwa mdau mkuu wa udini huyu si mwingine bali ni seif sharif hamad kaushikia bango waraka lakini wakati huohuo anakwambia mahakama ya kadhi si tatizo hawa wote wamefilisika na wamepotoka mwishowe wamefulia.Nawaombeni mnaoitakia mema nchi hii,pigeni vita hivi vyama mamluki na uchwara kama ccm na cuf,JARIBU KUSOMA ANDIKO LA MWANDISHI MMOJA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA 22-07-2009ANAPOULIZA''VIJANA TUCHAGUE CHAMA KIPI KATI YA CHADEMA AU CUF''?
  Naamini nimesomeka..............
   
 16. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Mlezi mkubwa wa udini ni JMK, kumbuka baraza lake la kwanza la mawaziri alivyoamua kuteua mawaziri wa dini yake kuongoza wizara zote nyeti mpaka watu tukampigiaa kelele.Kama kawaida yake anauendesha udini kwa romote control hasa baada ya kujidhihirisha kuwa ni kiongozi dhaifu sana, asiyejua aliomba uongozi kuiifanyia nini nchi.Lengo lake kubwa lilikuwa kuingia ikulu na kutembelea nchil mbalimbali na kutamba mitaani kwa misafara ya magari tu.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema kuna wababe wanatembea na mabomu.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Chadema ni chama kilichosheheni wasomi.
  Hawawezi kuvunja katiba ya nchi kwa ujinga huu na usitegemee kupata jibu hapa.
  Muulize Mh Zitto kama atakupa jibu. Najua yeye yuko bussy akisakama wanaokwiba mali zetu. si ujinga huu usio na tija kwa nchi yetu.
   
 19. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sula siyo kodi tu bali kusilimisha nchi, soma story yote utaelewa
   
 20. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ishu ni kodi sioni shida ila kama kuna sababu zingine za kisheria na kitaalam then zijadiliwe na mipaka iwe wazi.[/QUOTE]

  Ishu ni kodi lakini pia kusilimisha nchi nzima, soma story yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho utaelewa
   
Loading...