CCM Na CUF Waanza Kuhujumiana Pemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Na CUF Waanza Kuhujumiana Pemba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Sep 19, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  TABIA ya Wafuasi wa Vyama vya siasa Kisiwani Pemba kufanyiana vitendo vya hujuma bado inaendelea ambapo sasa imehamia katika kuhujumu mifugo.
  Katika matukio mawili yaliyotokea juzi na jana katika Jimbo la Ole, Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kombo Hamad Yussuf, banda lake la kuku zaidi ya 100 wamechomwa moto na watu wasiojulikana.
  Tukio kama hilo pia limemkumba Kiongozi wa Chama Cha Wananchi (CUF) Ali Salim Mussa ambaye kama ilivyo kwa Kiongozi wa CCM naye kuku wake wameteketezwa kwa moto katika banda lake la kuku.
  Akizungumzia matukio hayo, Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman alisema hujuma hizo zimetokea usiku wa manane eneo la Makaani nje kidogo ya Kijiji cha Kangagani katika Jimbo la Ole ambapo kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu linaendelea kwa kusua sua.
  Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwamba matukio yote mawili ni ya kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa Jimbo la Ole uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu bado unaendelea.
  “Hii ni siasa moja kwa moja, sio ajali ya kawaida…ni jambo la kusononesha mifugo kama kuku haina hatia yoyote inachomwa moto ni masikitiko makubwa sana” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya na kuongeza kwamba Serikali itawasaka kwa nguvu zote wahusika.
  Alisema wananchi wa Pemba wanapaswa kufahamu kuwa wana jukumu kwamba ushindani wa kisiasa sio ogomvi wala vitendo vya hujuma hivyo, aliwakumbusha kuzingatia ushindani wa kisiasa kwa hoja.
  Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi Wilayani humo kuwafichua watu wanaoendesha na kufadhili vitendo hivyo kwa kuwapa ushirikiano Askari wa Jeshi la Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa onyo kali kuwa Polisi haitosita kuwakamata watuhumiwa watakaobainika kuhusika na vitendo vya hujuma vinavyoendelea tokea kuaza tena kwa uboreshaji wa daftari la kudumu kisiwani Pemba.
  Kamanda Bugi amesema kwamba msako mkali unaoendelea kuwatafuta wanaotuhumiwa kuhusika na matukio mbali mbali ya hujuma katika Mkoa huo.
  Matukio ya kuhujumiana yamekuwa yakiongezeka kila kukicha kati ya vyama vya CCM na CUF ambapo vitendo vya kuunguziana nyumba, kupigana mawe, kuweka masega ya nyuki na kutiliana upupu katika vituo vya kujiandikishia yamekuwa yakifanyika.
  Katika kituo cha Shumba Mihogoni wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) walishindwa kufunga vifaa vyao katika kituo hicho baada ya kumwangwa upupu katika kituo hicho na kulazimika kubakia na vifaa vyao aktika gari kutwa nzima bila ya kufanyika kazi yoyote kwa siku nzima.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yote wameyataka "wakubwa" wameitengeneza shari imekuwa balaa mtindo mmoja.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pemba sote tunajuwa ni ngome kuu ya CUF. sasa nini tena.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yote hiyo ni mipango ya usalama wa Taifa ,yaani uchome kuku wa huku na huku kwa usiku mmoja ,hawa ni lazima wafanyiziwe ili atakapokamatwa mmoja apewe kisago cha paka mwizi ,iko siku watabakwa tu ,wajue mwindwa akitambua kuwa anawindwa kazi inakuwa kubwa na ya hasara.
   
Loading...