Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
CCM na CHADEMA wasidhubu kuitana faragha na KUJITOLEA maamuzi namna gani MADAI YA WANANCHI JUU YA KATIBA MPYA ifanyike, kwa kuwa kisheria katika sheria za MIKATABA moja kwa moja wanapoteza UHALALI huo bila kushirikishwa WANANCHI wote kwenye mjadala kama huo.
Endapo vya hivi viwili vyenye nguvu sana nchini wanaona ulazima kabisa kabisa kwenda mikutanoni faragha na bas wanao uhuru na haki ya kufanya hivyo hadi pale ambapo mijadala yao yote yatakua ni katika ngazi ya chama na chama kuhusu mambo yao ya KICHAMA zaidi na wala si KUTOLEA MAAMUZI MWENENDO WA HARAKATI ZA WANANCHI kujitafutia katiba mpya.
Katika mkutano kama huo binafsi pia wanaweza kubadilishana maoni juu ya (i) Uchaguzi Mkuu uliopita na rafu zake, (ii) mipango ufunguzi zaidi wa matawi ya vyama vyao huko mashinani, (iii) utoaji wa ruzuku kwa vyama uweje na (iv) kujipangi mikakati jinsi watakavyoshirikiana kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Kujadili KATIBA LAKINI SI kutuamulia juu ya MCHAKATO UWEJE. Serikali itimize kazi yake ya KUANZISHA na KUFADHILI na KUSHAURI pindi tu inapoombwa, kwa gharama ya kodi zetu mchakato mzima LAKINI UMILIKAJI WA MCHAKATO MZIMA NI JUKUMU LETU wananchi wenyewe bila kuingiliwa na mtu wala chombo chochote.
Kwa kuwa sote tunaelewa ukweli kwamba Katiba ni MKATABA rasmi kati ya WATAWALA na WATAWALIWA, CCM kama mtawala na CHADEMA kama mtawala mtarajiwa wote hawana jukumu hilo kutuamulia hatima yetu na katiba mpya kama taifa KIFICHONI!!!
Hakika hili halina ubishi ya kwamba kitendo cha watu au kikundi kamwe hawawezi KUJITENGA FARAGHA NA kuanza kujadili MKATABA WA UTAWALA (KATIBA) wakati sehemu muhimu ya mkataba huo imefungiwa njee kamwe halikubaliki!!!
Na kwa misingi hii naona kwamba ni hitaji la dharura kwenu enyi wanasheria mliobobea katika fani zenu waelewesheni wazee hawa mapema KUTOKUFIKIRIA KUVUNJA SHERIA YA MIKATABA kuhusiana na masusla ya Katiba mpya.
Kila wanapozungumza kwenye vyombo vya habari, siku zote napata picha ya kwamba licha ya serikali kugawa nakala za katiba kila ofisi, wengi wao viongozi wetu ni MBUMBUMBU kabisa kuhusu yaliomo ndani kwa kuwa hawajawahi kukifunua na kukisoma. Unaposema SI MUDA mwafaka kujiandikia katiba mpya, hilo linakua ni wazo binafsi au ni maelekezo ndani ya katiba yanayotuzuia kufanya hivyo??????
Nielewavyo mimi CCM ni MTAWALA (Japo wa kujitawaza mwenyewe), na CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wote hawa ni WATAWALA MBADALA wanaoendelea kupiga jaramba pembeni mwa uwanja ili tukawape tiketi ya kuanza kazi.
Hivyo, kwa msingi huu katika haki yangu ya uraia naona ni makosa makubwa tena sana WATAWALA kuitana faragha kutaka kutubadilishia katiba kwa mtindo watakaopenda wao. Kosa hili nalo lilitendeka Zanzibar kwa Maalim Seif Kukubaliana kugawana madaraka ya visiwa hivyo. Wazanzibari waliitwa tu kwenye KUTIA MUHURI harakati hizo za CCM na CUF kwenye KURA YA MAONI. Sisi tunasema hatutotumika kama mihuri katika hili.
Yale maoni yatakayoonekana ni sawa na sote tumekubaliana kwa pamoja katika itikadi zet tofauti tofauti na basi yataingizwa kwenye katiba moja kwa moja.
Na endapo kuna mambo mengine yatakayoonekana kuwa ni MAGUMU SANA na hatukubaliani vema basi hayo NDIO TUTAKAYOYAPELEKA KWENYE KURA YA MAONI, na baadaye kupewa kamati ndogo ya pamoja yenye wataalam wa sheria KUYAUNDANDA MATAKWA YETU HAYO toka katika lugha ya mitaani kuja kwenye lugha inayokubalika kisheria. Lakini mara hii hatutumiki kama mihuri na wala katiba mpya hatuandikiwi na MADALALI WA KUTEULIWA NA WATAWALA wenyewe.
Nasema msianze kukaribisha utata wa kisheria hapa. Bora tukajiandikie katiba yetu taratibu bila kubisha mlango wa pili kwa mivutano mikubwa KISHERIA. Mikutano ya pembeni pembeni yabakia kuwa ni mikutano ya vikundi vikundu kama WASHIKADAU wa KATIBA kujipanga jinsi watakavyowakilisha MATAKWA YAO KWENYE MKUTANO MKUU WA TAIFA wa kujadili KATIBA MPYA.
Kwenye mkutano huu watu wote TUJE KWENYE MKUTANO PALE UWANJA WA TAIFA TUKIWA TUNAFIKIRI KAMA RAIA NA WALA MTU AU KIKUNDI KISIJE PALE NA MADARAKA YAKE WALA VYEO. Mijadala ya katiba hu ni mitamu zaidi kwa sababu ndio sehemu pekee ambapo mkulima wa kahawa kule Mbinga anakua na haki sawa kwa sasa na mtu kama Jakaya Mrisho Kikwete au msomi aliebobea kama Prof Issa Shivji. Mbele ya mjadala wa katiba, hakuna cha (i) Vyeo, (ii) Usomi wala (iii) ukada wa aina yoyote ile.
Uongozi wa masuala ya Katiba HATUTAKUJA NAO TOKA NYUMBANI BALI NI KWAMBA NI WAJUMBE WA KWENYE HUO MKUTANO WA KITAIFA ndio watakaojiamulia akina nani wakawaongoze katika hilo. Enyi mlioko serikalini kwa sasa, ombeni DARASA mapema katika hili kabla hanjaumbuka zaidi.
Mama kombani si wajibu wako kupokea maoni yetu bali ni jukumu lako KUANZISHA na kugharamia mchakato kwa kodi zetu hapo hazina full stop!!!
SWALI:
Kwa kuwa sote tunakubali ya kwamba KATIBA ni MKATABA wa HAKI YA KUTAWALA kati ya Watawala (Serikali) na WATAWALIWA (Sisi Wananchi) je, ni sahihi WATAWALA (CCM) wa sasa hivi kuitana faragha na WATAWALA WATARAJIWA (CHADEMA / CUF / TLP) KUTHUBUTU KUJADILI jambo lolote juu ya MADAI YA KATIBA MPYA na hata kudiriki kuitolea MAAMUZI bila ya sisi WANANCHI moja kwa moja kuhusishwa???
Nawashilisha hoja.