CCM na CHADEMA Wasijiandae KUKIUKA Sheria ya Mikataba Juu ya KATIBA MPYA

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
CCM na CHADEMA wasidhubu kuitana faragha na KUJITOLEA maamuzi namna gani MADAI YA WANANCHI JUU YA KATIBA MPYA ifanyike, kwa kuwa kisheria katika sheria za MIKATABA moja kwa moja wanapoteza UHALALI huo bila kushirikishwa WANANCHI wote kwenye mjadala kama huo.

Endapo vya hivi viwili vyenye nguvu sana nchini wanaona ulazima kabisa kabisa kwenda mikutanoni faragha na bas wanao uhuru na haki ya kufanya hivyo hadi pale ambapo mijadala yao yote yatakua ni katika ngazi ya chama na chama kuhusu mambo yao ya KICHAMA zaidi na wala si KUTOLEA MAAMUZI MWENENDO WA HARAKATI ZA WANANCHI kujitafutia katiba mpya.

Katika mkutano kama huo binafsi pia wanaweza kubadilishana maoni juu ya (i) Uchaguzi Mkuu uliopita na rafu zake, (ii) mipango ufunguzi zaidi wa matawi ya vyama vyao huko mashinani, (iii) utoaji wa ruzuku kwa vyama uweje na (iv) kujipangi mikakati jinsi watakavyoshirikiana kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Kujadili KATIBA LAKINI SI kutuamulia juu ya MCHAKATO UWEJE. Serikali itimize kazi yake ya KUANZISHA na KUFADHILI na KUSHAURI pindi tu inapoombwa, kwa gharama ya kodi zetu mchakato mzima LAKINI UMILIKAJI WA MCHAKATO MZIMA NI JUKUMU LETU wananchi wenyewe bila kuingiliwa na mtu wala chombo chochote.

Kwa kuwa sote tunaelewa ukweli kwamba Katiba ni MKATABA rasmi kati ya WATAWALA na WATAWALIWA, CCM kama mtawala na CHADEMA kama mtawala mtarajiwa wote hawana jukumu hilo kutuamulia hatima yetu na katiba mpya kama taifa KIFICHONI!!!

Hakika hili halina ubishi ya kwamba kitendo cha watu au kikundi kamwe hawawezi KUJITENGA FARAGHA NA kuanza kujadili MKATABA WA UTAWALA (KATIBA) wakati sehemu muhimu ya mkataba huo imefungiwa njee kamwe halikubaliki!!!

Na kwa misingi hii naona kwamba ni hitaji la dharura kwenu enyi wanasheria mliobobea katika fani zenu waelewesheni wazee hawa mapema KUTOKUFIKIRIA KUVUNJA SHERIA YA MIKATABA kuhusiana na masusla ya Katiba mpya.

Kila wanapozungumza kwenye vyombo vya habari, siku zote napata picha ya kwamba licha ya serikali kugawa nakala za katiba kila ofisi, wengi wao viongozi wetu ni MBUMBUMBU kabisa kuhusu yaliomo ndani kwa kuwa hawajawahi kukifunua na kukisoma. Unaposema SI MUDA mwafaka kujiandikia katiba mpya, hilo linakua ni wazo binafsi au ni maelekezo ndani ya katiba yanayotuzuia kufanya hivyo??????

Nielewavyo mimi CCM ni MTAWALA (Japo wa kujitawaza mwenyewe), na CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wote hawa ni WATAWALA MBADALA wanaoendelea kupiga jaramba pembeni mwa uwanja ili tukawape tiketi ya kuanza kazi.

Hivyo, kwa msingi huu katika haki yangu ya uraia naona ni makosa makubwa tena sana WATAWALA kuitana faragha kutaka kutubadilishia katiba kwa mtindo watakaopenda wao. Kosa hili nalo lilitendeka Zanzibar kwa Maalim Seif Kukubaliana kugawana madaraka ya visiwa hivyo. Wazanzibari waliitwa tu kwenye KUTIA MUHURI harakati hizo za CCM na CUF kwenye KURA YA MAONI. Sisi tunasema hatutotumika kama mihuri katika hili.

Yale maoni yatakayoonekana ni sawa na sote tumekubaliana kwa pamoja katika itikadi zet tofauti tofauti na basi yataingizwa kwenye katiba moja kwa moja.

Na endapo kuna mambo mengine yatakayoonekana kuwa ni MAGUMU SANA na hatukubaliani vema basi hayo NDIO TUTAKAYOYAPELEKA KWENYE KURA YA MAONI, na baadaye kupewa kamati ndogo ya pamoja yenye wataalam wa sheria KUYAUNDANDA MATAKWA YETU HAYO toka katika lugha ya mitaani kuja kwenye lugha inayokubalika kisheria. Lakini mara hii hatutumiki kama mihuri na wala katiba mpya hatuandikiwi na MADALALI WA KUTEULIWA NA WATAWALA wenyewe.

Nasema msianze kukaribisha utata wa kisheria hapa. Bora tukajiandikie katiba yetu taratibu bila kubisha mlango wa pili kwa mivutano mikubwa KISHERIA. Mikutano ya pembeni pembeni yabakia kuwa ni mikutano ya vikundi vikundu kama WASHIKADAU wa KATIBA kujipanga jinsi watakavyowakilisha MATAKWA YAO KWENYE MKUTANO MKUU WA TAIFA wa kujadili KATIBA MPYA.

Kwenye mkutano huu watu wote TUJE KWENYE MKUTANO PALE UWANJA WA TAIFA TUKIWA TUNAFIKIRI KAMA RAIA NA WALA MTU AU KIKUNDI KISIJE PALE NA MADARAKA YAKE WALA VYEO. Mijadala ya katiba hu ni mitamu zaidi kwa sababu ndio sehemu pekee ambapo mkulima wa kahawa kule Mbinga anakua na haki sawa kwa sasa na mtu kama Jakaya Mrisho Kikwete au msomi aliebobea kama Prof Issa Shivji. Mbele ya mjadala wa katiba, hakuna cha (i) Vyeo, (ii) Usomi wala (iii) ukada wa aina yoyote ile.

Uongozi wa masuala ya Katiba HATUTAKUJA NAO TOKA NYUMBANI BALI NI KWAMBA NI WAJUMBE WA KWENYE HUO MKUTANO WA KITAIFA ndio watakaojiamulia akina nani wakawaongoze katika hilo. Enyi mlioko serikalini kwa sasa, ombeni DARASA mapema katika hili kabla hanjaumbuka zaidi.

Mama kombani si wajibu wako kupokea maoni yetu bali ni jukumu lako KUANZISHA na kugharamia mchakato kwa kodi zetu hapo hazina full stop!!!

SWALI:

Kwa kuwa sote tunakubali ya kwamba KATIBA ni MKATABA wa HAKI YA KUTAWALA kati ya Watawala (Serikali) na WATAWALIWA (Sisi Wananchi) je, ni sahihi WATAWALA (CCM) wa sasa hivi kuitana faragha na WATAWALA WATARAJIWA (CHADEMA / CUF / TLP) KUTHUBUTU KUJADILI jambo lolote juu ya MADAI YA KATIBA MPYA na hata kudiriki kuitolea MAAMUZI bila ya sisi WANANCHI moja kwa moja kuhusishwa???


Nawashilisha hoja.
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
168
kama cuf walivyoamua kukataa kukaa tuu huku nguruwe wakila shamba na wao kuamua kula shamba pamoja nguruwe kule Unguja na kugawana keki ya taifa! (maneno ya HR)
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
Mkuu,
kama si usumbufu, edit hii na iweke kwenye black,hizi rangi ulizotumia zinaumiza macho.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
kama cuf walivyoamua kukataa kukaa tuu huku nguruwe wakila shamba na wao kuamua kula shamba pamoja nguruwe kule Unguja na kugawana keki ya taifa! (maneno ya HR)

Gad Oneya, nakupata hapa. Si kweli kabisa kwamba sisi wananchi wa taifa hili tumeamua kudai katiba mpya halafu kuje kuishie kugawana vyeo (keki) kwa watu wachache, hapana.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe. Sisi wananchi tumejaa tele hapa halafu CCM ianze na vijimbinu za Bunuasi mara ooohh leteni mapendekezo, ooohhhh nateua tume ...

Nani kakuambia hayo yote?? Mzee Mkono peleka darasa kuhusu maswala ya MIKATABA pale CCM na ikulu wapate kuelewa ya kwamba ushiriki wetu wananchi moja kwa moja KUJIANDIKIA KATIBA MPYA tutakavyo wenyewe ni suala ambalo halikwepeki, la sivyo tukutane mahakamani. Wewe MTAWALA na MARAFIKI ZAKO hamuwezi kujijadilia MKATABA HALALI niliokuweka nayo kazini na kujitilia sahihi wakati ningali nipo hai kama raia wa nchi hii.

Atakaedhubutu kuleta janja za nyani kula shamba zima hapa ujue mgogoro wa kisheria itakua inasubiri. Hatutaki tena UDALALI katika swala zima la KATIBA MPYA!!! Udalali wa kuleta utani wa KUJITEULIA tume na HADIDU-ZA-REJEA nazo utoe wewe, usimamizi wake pia ni wewe na kuja kututangazia kwamba ni 'Wa-Tanzania asilimia 2%' ndio wanaotaka mabadiliko nayo ufanye wewe, aa wapi!!!!
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
wtf is up with ur font.. its annoying

Mkuu,
Nilimshauri abadilishe lakini pengine hakupata ujumbe. Kwa vile ameleta mada poa, nafikiri ataridhia kwa mimi kuibandika tena katika fonts hizi.

Ni hii mkuu,

Re: CCM na CHADEMA Wasijiandae KUKIUKA Sheria ya Mikataba Juu ya KATIBA MPYA!!


CCM na CHADEMA wasithubutu kuitana faragha na KUJITOLEA maamuzi namna gani MADAI YA WANANCHI JUU YA KATIBA MPYA ifanyike, kwa kuwa kisheria katika sheria za MIKATABA moja kwa moja wanapoteza UHALALI huo bila kushirikishwa WANANCHI wote kwenye mjadala kama huo.

Endapo vyama hivi viwili vyenye nguvu sana nchini wanaona ulazima kabisa kabisa kwenda mikutanoni faragha na basi wanao uhuru na haki ya kufanya hivyo hadi pale ambapo mijadala yao yote itakua ni katika ngazi ya chama na chama kuhusu mambo yao ya KICHAMA zaidi na wala si KUTOLEA MAAMUZI MWENENDO WA HARAKATI ZA WANANCHI kujitafutia katiba mpya. Katika mkutano kama huo binafsi pia wanaweza kubadilishana maoni juu ya (i) Uchaguzi Mkuu uliopita na rafu zake, (ii) mipango ufunguzi zaidi wa matawi ya vyama vyao huko mashinani, (iii) utoaji wa ruzuku kwa vyama uweje na (iv) kujipangia mikakati jinsi watakavyoshirikiana kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Kujadili KATIBA LAKINI SI kutuamulia juu ya MCHAKATO UWEJE. Serikali itimize kazi yake ya KUANZISHA na KUFADHILI na KUSHAURI pindi tu inapoombwa, kwa gharama ya kodi zetu mchakato mzima LAKINI UMILIKAJI WA MCHAKATO MZIMA NI JUKUMU LETU wananchi wenyewe bila kuingiliwa na mtu wala chombo chochote.

Kwa kuwa sote tunaelewa ukweli kwamba Katiba ni MKATABA rasmi kati ya WATAWALA na WATAWALIWA, CCM kama mtawala na CHADEMA kama mtawala mtarajiwa wote hawana jukumu hilo kutuamulia hatima yetu na katiba mpya kama taifa KIFICHONI!!!

Hakika hili halina ubishi ya kwamba kitendo cha watu au kikundi kamwe hawawezi KUJITENGA FARAGHA NA kuanza kujadili MKATABA WA UTAWALA (KATIBA) wakati sehemu muhimu ya mkataba huo imefungiwa nje kamwe halikubaliki!!!

Na kwa misingi hii naona kwamba ni hitaji la dharura kwenu enyi wanasheria mliobobea katika fani zenu waelewesheni wazee hawa mapema KUTOKUFIKIRIA KUVUNJA SHERIA YA MIKATABA kuhusiana na masuala ya Katiba mpya.

Kila wanapozungumza kwenye vyombo vya habari, siku zote napata picha ya kwamba licha ya serikali kugawa nakala za katiba kila ofisi, wengi wao viongozi wetu ni MBUMBUMBU kabisa kuhusu yaliyomo ndani kwa kuwa hawajawahi kukifunua na kukisoma. Unaposema SI MUDA mwafaka kujiandikia katiba mpya, hilo linakua ni wazo binafsi au ni maelekezo ndani ya katiba yanayotuzuia kufanya hivyo??????

Nielewavyo mimi CCM ni MTAWALA (Japo wa kujitawaza mwenyewe), na CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wote hawa ni WATAWALA MBADALA wanaoendelea kupiga jaramba pembeni mwa uwanja ili tukawape tiketi ya kuanza kazi.

Hivyo, kwa msingi huu katika haki yangu ya uraia naona ni makosa makubwa tena sana WATAWALA kuitana faragha kutaka kutubadilishia katiba kwa mtindo watakaopenda wao. Kosa hili nalo lilitendeka Zanzibar kwa Maalim Seif Kukubaliana kugawana madaraka ya visiwa hivyo. Wazanzibari waliitwa tu kwenye KUTIA MUHURI harakati hizo za CCM na CUF kwenye KURA YA MAONI. Sisi tunasema hatutotumika kama mihuri katika hili.

Yale maoni yatakayoonekana ni sawa, na sote tumekubaliana kwa pamoja katika itikadi zetu tofauti tofauti, basi yataingizwa kwenye katiba moja kwa moja.

Na endapo kuna mambo mengine yatakayoonekana kuwa ni MAGUMU SANA na hatukubaliani vema basi hayo NDIO TUTAKAYOYAPELEKA KWENYE KURA YA MAONI, na baadaye kupewa kamati ndogo ya pamoja yenye wataalam wa sheria KUYAUNDA MATAKWA YETU HAYO toka katika lugha ya mitaani kuja kwenye lugha inayokubalika kisheria. Lakini mara hii hatutumiki kama mihuri na wala katiba mpya hatuandikiwi na MADALALI WA KUTEULIWA NA WATAWALA wenyewe.

Nasema msianze kukaribisha utata wa kisheria hapa. Bora tukajiandikie katiba yetu taratibu bila kubisha mlango wa pili kwa mivutano mikubwa KISHERIA. Mikutano ya pembeni pembeni yabakie kuwa ni mikutano ya vikundi vikundu kama WASHIKADAU wa KATIBA kujipanga jinsi watakavyowakilisha MATAKWA YAO KWENYE MKUTANO MKUU WA TAIFA wa kujadili KATIBA MPYA.

Kwenye mkutano huu watu wote TUJE KWENYE MKUTANO PALE UWANJA WA TAIFA TUKIWA TUNAFIKIRI KAMA RAIA NA WALA MTU AU KIKUNDI KISIJE PALE NA MADARAKA YAKE WALA VYEO. Mijadala ya katiba hii ni mitamu zaidi kwa sababu ndio sehemu pekee ambapo mkulima wa kahawa kule Mbinga anakua na haki sawa kwa sasa na mtu kama Jakaya Mrisho Kikwete au msomi aliebobea kama Prof Issa Shivji. Mbele ya mjadala wa katiba, hakuna cha (i) Vyeo, (ii) Usomi wala (iii) ukada wa aina yoyote ile.

Uongozi wa masuala ya Katiba HATUTAKUJA NAO TOKA NYUMBANI BALI NI KWAMBA NI WAJUMBE WA KWENYE HUO MKUTANO WA KITAIFA ndio watakaojiamulia akina nani wakawaongoze katika hilo. Enyi mlioko serikalini kwa sasa, ombeni DARASA mapema katika hili kabla hamjaumbuka zaidi.

Mama kombani si wajibu wako kupokea maoni yetu bali ni jukumu lako KUANZISHA na kugharamia mchakato kwa kodi zetu hapo hazina full stop!!!Kwa kuwa sote tunakubali ya kwamba KATIBA ni MKATABA wa HAKI YA KUTAWALA kati ya Watawala (Serikali) na WATAWALIWA (Sisi Wananchi) je, ni sahihi WATAWALA (CCM) wa sasa hivi kuitana faragha na WATAWALA WATARAJIWA (CHADEMA / CUF / TLP) KUTHUBUTU KUJADILI jambo lolote juu ya MADAI YA KATIBA MPYA na hata kudiriki kuitolea MAAMUZI bila ya sisi WANANCHI moja kwa moja kuhusishwa???
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,010
9,181
Katiba siyo Mkataba baina ya Watawala na Watawaliwa, bali katiba ni sheria mama(isiyo mkataba) yenye kuonyesha majukumu ya msingi na haki za msingi za kila mmoja kwa taifa, yenye kuonyesha taifa liendeshwe vipi, Watawala na wasio watawala lazima waheshimu sheria hii.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Profesa Shivji ataka Katiba-Mpya Ishirikishe Wananchi Send to a friend Monday, 20 December 2010 20:31

Hussein Kauli

MWANAZUONI na mtaalamu wa sheria nchini, Profesa Issa Shivji, amesema suala la katibu mpya linahitaji kushirikisha wananchi kupata suluhisho la kudumu.Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Baraza la Afrika la Maendeleo ya Tafiti za Sayansi ya Jamii (CODESRIA) jana, Profesa Shivji alisema suala la kuandikwa katiba mpya lazima wananchi washirikishwe.

Profesa Shivji alisema kwa sababu serikali imeonyesha nia ya kukubali, suala hilo linahitaji kuzipatia suluhu changamoto muhimu zinazowakabili mwananchi wa kawaida.

Alisema iwapo mwananchi wa kawaida hatashirikishwa kwenye katiba hiyo, Tanzania haiwezi kufika popote, kwani taifa linahitaji kuwafikisha wananchi pale wanapotaka.


"Uchumi wetu na uzalishaji ni mambo yanayohitaji kuangaliwa kwa makini, bila ya kuyaangalia hayo hatuwezi kufika popote, jamii inahitaji Tanzania mpya ili tufike kwenye Tanzania tunayoitaka," alisema Profesa Shivji.


Alisema kupata katiba mpya, ni vyema serikali ikawashirikisha wananchi wa kawaida ili kupata suluhisho la umikishaji ardhi ambalo ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Kuhusu mkutano huo unashirisha wasomi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Profesa Shivji alisema baada ya nchi za Afrika kupitia kwenye kipindi kigumu, wanahitaji kukaa na kuangalia njia za kuboresha uchumi wake.


"Haitoshi kusema uchumi wa nchi unakua kwa asilimia tano, badala yake, tunatakiwa kuangalia hali ya wananchi ikoje ili kujenga uchumi utakaowanufasha," alisema.

Alisema katika kufikia huko, Watanzania wanahitaji kuangalia upya sera na mambo yanayochangia ukuaji uchumi kama uwekezaji ili kutoa mchango wao.

Profesa Shivji alisema wasomi hao kutoka vyuo vikuu mbalimbali barani Afrika, wanaangalia mambo muhimu yanayochangia kujenga uchumi wa Afrika ili kujua kinachokosekana ili malengo yafikiwe.


Katika hotuba yake ya ufunguzi, Profesa Shivji alisema wasomi wa Afrika wanahitaji kufanya Uafrika kuwa njia bora ya kuwaamsha kupigania maendeleo.

Kwa upange wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema ni aibu kubwa baada ya kupita miaka takriban 50 ya Uhuru wa Tanzanyika, nchi imeendelea kuwa maskini.My Take:


Nimependezwa sana na huyu msomi na mzoefu mkubwa wa sheria, katiba na siasa za nchi yetu, Prof Shivji, kuona sababu za sisi WANANCHI kushirikishwa moja kwa moja katika kujiandikia KATIBA MPYA.


Endapo hili wazo litafanyiwa kazi kwa uwazi wote unaohitajika basi safari hii itakua ni kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.


Hongera sana Prof Shivji na Wanaharakati wengine wa aina yako. Pongezi pia ziwaendee CUF na Prof Lipumba kwa kujitokeza kwao katika swala la kudai KATIBA MPYA bila unafiki, tofauti za kiitikadi wala kigugumizi chochote kile.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
'ZAKUMI' NA SABABU ZA KUTAKA KATIBA MPYA TANZANIA

Kama kawaida, ningependa kutoa salaam kwa waZalendo wenzangu. Katika mjadala huu wa katiba kuna mambo mengi yanajitokeza. Moja ya jambo lililojitokeza ni kutaka kufanyia amendment ya vipengere ya katiba ya sasa. Mzee Mwinyi amesimamia hilo jambo. Kwanza nilimuunga mkono lakini kwa sasa naona kuwa umefika wakati wa katiba mpya.

Kwanini tunahitaji katiba mpya na sio kubadilisha? Zifuatazo ni sababu zangu za kutaka katiba mpya. Kumbuka hizi ni sababu za kutaka katiba mpya na sio vitu vitakavyokuwa ndani ya katiba hiyo.


Kwanza: Katiba ya sasa ni ngumu kiuandishi. Imeandikwa kwa lugha ya mwanasheria. Inatakiwa iandikwe kwa lugha ambayo itamfanya mtu yoyote kuelewa katiba hiyo.


Pili: Katiba ina muundo wa check and balance ya chama kimoja. Katika mfumo wa chama kimoja, chama tawala kilikuwa ni mhimili mwingine wa utawala na chujio la kupata viongozi. Kwa sasa check and balance iwe mikononi mwa watu. Watu wawe na uwezo wa kumwingiza mtu madarakani na vilevile kumvua madaraka. Shughuli za bunge, mahakama na serikali ziwe za kutazama utendaji mzuri na sio kulindana.


Tatu: Baada ya uhuru marais wengi wa Africa walijilundikia madaraka hili kufanya reforms au kuzuia mgawanyiko wa kidini na kikabila. Wengi waliboronga na wachache walitumia madaraka yao vizuri. Hivyo wimbi la marais kuwa na madaraka mengi hili kuondoa tofauti za kikabila na kidini zimepitwa na wakati. Kwa Tanzania ni muda wa kurudisha madaraka kwa wananchi wenyewe. Hakuna sababu mtu ambaye hana interests na maendeleo ya watu wa Mtwara awe mkuu wa Mkoa wa Mtwara.


Nne: Katiba inawakilisha historia ya nchi na watu wake. Katiba ya sasa inawakilisha maoni viongozi wa juu. Viongozi hao walitaka nchi iwe kwa mtazamo wao. Kwa mfano kujenga taifa la kijamaa ni madhumini ya katiba ya sasa. Hivi toka tumepata uhuru kuna mtanzania wa kawaida aliyetaka kujenga Ujamaa kwa hiari yake?


Tano: Katiba lazima imlinde na kumpa haki mtanzania katika kushiriki katika shughuli za uongozi wa nchi yake. Katiba ya sasa ina mpa haki mwanachama wa chama cha kisiasa.Kwa vipengere nilivyoweka hapo juu na vingene vitakavyokuja, dai katiba mpya. Itasaidia kama utasoma katiba ya sasa. Lakini hakuna ulazima wa kuisoma katiba yenyewe.


Wenu:


Z10
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Mheshimiwa Kikwete, njia salama na pekee ya kuandikwa kwa KATIBA MPYA nchini ni kwa KUSHIRIKISHA WADAU WOTE TANGU MWANZO hadi mwisho. Kwenye katika hakuna cheo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom