CCM na Chadema ni Njaa Kali

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wana Jf, Kwa sasa hivi vyama viwili vinapitia maisha ya hovyo kuwahi kutokea kwenye siasa Zake za miaka kumi iliyopita. kipindi cha Raisi Kikwete vilinufaika sana kipesa. Kamati nyingi zilizoundwa bungeni wakati wa JK zilishirikiana sana kimkakati hasa kwenye matumizi ya pesa.

Wabunge wengine walihongwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kuitetea kwenye kamati, Wabunge wengine waligeuka kuwa wauwaji wa Tembo wakimiliki silaha za kuulia wanyama
Yote haya yalifanyika kwa ushirikiano mzuri wa hizi kamati zilizoundwa na CCM na Chadema .

Hivi vitendo vya hama hama na kuikejeli serikali ni mbinu zinazotumiwa na wabunge wetu kwa sasa kutafuta shibe ya matumbo yao, Wengi walikopa pesa kipindi cha kampeni 2015 mambo yamekwenda ndivyo sivyo kwao

Ni muhimu kwa sasa kuanza kuwapuuza hawa wanasiasa wa hivi vyama viwili CCM na Chadema kama ilivyofanyika kwa kukipuuza chama cha CUF Maalim na Lipumba wake

Ni muhimu kuanza kuwaandika wanasiasa mmoja baada ya mungine kwa kuwaambia ukweli, Njaa na Tamaa zao zisiwayumbishe raia zaidi ya milioni 50

Ukiwaangalia Nape, Zitto,Nyalandu Kigwangala, Bashe na Mwigulu aliyejifanya kondoo sasa kwa ukimya ni njaa na uroho wa madaraka unawasumbua
 
Kuna hoja unayo mkuu..... Mi kuna mtu alihamia chadema na licha ya kumpigia kura lkn bado siioni dhamira yake ya kuwa mpinzan zaidi ya kuongeza uchafu tu uku Ken upinzani.......
 
Kuna hoja unayo mkuu..... Mi kuna mtu alihamia chadema na licha ya kumpigia kura lkn bado siioni dhamira yake ya kuwa mpinzan zaidi ya kuongeza uchafu tu uku Ken upinzani.......
Wamegeuka wasoma upepo hawa wanasiasa wanaangalia usalama wao na maslahi binafsi, Hakuna ishu ya maana kati ya Nyalandu na Masha ni vyeo na maslahi ya usalama wao
 
ipo siku mtatuelewa tunaowaambia huko upinzani wamejaa wasanii tu.
 
Kuna hoja unayo mkuu..... Mi kuna mtu alihamia chadema na licha ya kumpigia kura lkn bado siioni dhamira yake ya kuwa mpinzan zaidi ya kuongeza uchafu tu uku Ken upinzani.......

Mkuu usiongee kwa kuficha ficha, sema Lowassa. Mbona kamanda unakuwa muoga. Chama kimefubazwa na siasa za kikondoo. Cdm tunataka jembe kama Lissu sio mtu wa siasa za kubembeleza huku anachukua mshahara kila mwezi serekalini. Mbowe atafungasha na parcel lake. Huku kuficha ficha ndo kunafanya chama chetu makamanda kinashikwa sehemu mbaya na ccm. Tuseme kwamba Lowassa hakuwa mtu sahihi kwetu cdm na Mbowe alikosea. Tunaheshimu mchango wa Mbowe, lakini kwa hili hapana na yeye ni wakati muafaka wa kupumzika kiroho safi.
 
Back
Top Bottom