VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Sasa siasa zinafanyika kweli. Siasa ni hoja,mbinu na mikakati.Maneno yakutosha;sera za ‘kumwaga';wagombea wenye 'sifa', nia kweli na vyama vyenye ushawishi mkubwa. Hii sasa ndiyo siasa. Ingawa sote tunalenga kuijenga nchi yetu ya Tanzania, tofauti lazima ziwepo. Bila ya tofauti hakutakuwa na kujirekebisha wala kusonga mbele.Hatutaendelea. Tutabaki tulipo.
CCM na CHADEMA sasa ni ‘hatua kwa hatua',bega kwa bega. Halali mtu;ukilala hauamshwi. Upinzani umeenea karibu nchi nzima. Kuanzia Mashariki hadi Magharibi;Kaskazini hadi Kusini. Siasa za vyama vingi si tu kama zipo lakini pia zinaonekana kuwepo.
Hapa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake;pale Freeman Aikaeli Mbowe na makamanda wake. Siasa zinafanywa Bungeni,runingani,majukwaani,mitaani,kwenye kampeni na kwingineko. Mchuano huu sasa umefika patamu. Sasa ni hama huku-njoo huku. Yaani mbaya huku,mzuri kule.
Siasa za CCM na CHADEMA zinafanywa kidijitali sana. Watu wanapondana na baadaye wanakutana. Wanasemana baadaye wanachekeana. Ndizo siasa za kisasa. Matusi na kejeli zisizo na mpango hazina nafasi. Tuanataka sera na si hela.
Jumapili kutafanyika Uchaguzi Mdogo wa nafasi za Udiwani katika mikoa mbalimbali nchini. Kila mkoa,CCM na CHADEMA mpambano ni moto. Kila upande unatarajia ushindi.Ni kama enzi za mpambano wa ndondi kati ya Mohammad Alli na George Foreman. Jumatatu, watanzania wataanza kupokea matokeo. Washindi watatangazwa.Watakuwa watumishi wetu.
Upinzani wa dhati uliopo nchini kwasasa unasaidia mambo mengi. Viongozi hawajisahau tena. Ufisadi unapungua. Uhakika wa kushinda kwakuwa uko chama fulani haupo tena. Hakuna urahisi wa kupita bila kupingwa.Miradi ya maendeleo inakodolewa macho na kulindwa. Tunapata maendeleo.
CCM na CHADEMA, endeleeni hivyo hivyo hadi kieleweke!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.