CCM na CHADEMA katika kubadilisha msimamo kijamii, kisiasa na kiuchumi - nani zaidi kati yao?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,680
1,250
Nimetafakari sana kuwa ni nani zaidi kati ya CCM na Chadema katika kubadilisha msimamo kijamii, kisiasa na kiuchumi? Kwa mfano CCM walikuwa na msimamo kuhusu katiba mpya haki kuanzisha mchakati uliopelekea kukusanya maoni ya wananchi.

Pia ilikuwa na msimamo kuwa Corona haipo Tanzania kwa tumeomba Mungu ameiondoa na sasa haipendelei kuongelea katiba mpya na kuhusu Corona sasa inakubali ipo na kukubaliana pia na chanjo yake.

Kwa upande wa Chadema wakati wa mchakato wa Katiba mpya walitoka nje ya mjadala ili kuikwamisha na sasa wanaongelea kuhusu Katiba mpya.

Pia Chadema iliwahi kuwaita viongozi fulani waandamizi serikali kuwa ni mafisadi lakini baadaye waliwakaribisha kwenye chama chao na kuwapa nafasi ya kugombea uongozi.

Wanajamvi misimamo kama hii mnaionaje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom