CCM mumeona nchi jirani wasemavyo kuhusu Rais Magufuli?

Mimi naamini kuwa Mh Rais hawezi kutoa maelekezo na maagizo kama aliyoyatoa bila kupata ushauri wa wataalamu, hivyo kama kuna kosa lolote wa kulaumiwa ni Washauri wake wa-kitaalamu, Ikumbukwe, Rais ni Taasisi na siyo mtu mmoja kwa hiyo kumlaumu ni kosa kabisa.

Lakini pia huu si wakati wa kuona nchi ya jirani wakimdharau na kumkejeli Rais wetu na kufurahia. Hii ni sawa na kumsikia au kumuona jirani anamdhalilisha na kumfedhehesha mzazi wako nawe ukafurahia tena na kujiunga nao. Ni wakati wa kuwa kama familia moja kukemea hili hata kama ndani tuna tofauti zetu haiwezekani Rais wetu kama mzazi akakejeliwa halafu tukafurahia, #HAPANAhaikubaliki

Naanza kupata picha mbaya sasa, huenda wapo Watanzania kwa hali hii ya kufurahi mambo haya, iko siku watu watasikia kuwa jirani kapanga jambo baya kuhusu Nchi yetu kama VITA n.k halafu wakafurahia na kuungana nao bila kujua sisi ndio tutakaoathirika, hebu tubadilike kama Haumheshimu Magufuli, basi Mheshimu Rais maana yuko pale kisheria na kuna taratibu za kufuata ili kupata kiongozi mwingine nayo ni kupiga kura au ni lile la kuvunja Katiba na imeelezwa taratibu za kufuata ili kumwondoa Rais madarakani.

Walichokifanya jirani zetu ni kitendo cha aibu na kinapaswa kukemewa na kila Mtanzania hata na mataifa mengine cha kuingilia uhuru wa Taifa lingine..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Actually you are a fool number one...usifikiri wote ni wajinga Kama wewe...humu tunaelimishana na siyo kutanguliza matusi...kwa kutanguliza matusi humu ni uthibitisho wa namna ulivyo mjinga. Kuleta Mambo ya age humu ni uthibitisho wa ujinga wako na ni dhahiri hujakomaa kimawazo...if you don't like to argue here then shut up...Huwezi ukawaita wenzako wajinga halafu tukuache tu..if you continue with this rubbish of yours then nitakureport TCRA...

Is Your ID not 1954?
Then what's wrong calling you Mzee wa 1954....?
Hivi kuitwa Mzee au a Fool(mpumbavu)ni Tusi? Neno Pumbavu hata Rais wako analitumia kila mara mbona hujampeleka TCRA?
TUSITISHANE HAPA JF.....!
Wazungu Wana msemo: "IF YOU CAN'T STAND THE HEAT, GET OUT OF THE KITCHEN..." Hapa JF tunashindana kwa hoja na kama huna hoja ni bora ukae kimya na SIYO kutishia watu na TCRA!
 
Rubbish
Hivi ndio TV za nchi jirani zinavyo m-describe Mzee Baba, kama mtu MKAIDI.

Je, mkaidi ni mtu wa aina gani? Huyo kwa kiingereza ni Stubborn na huwa hafai kwenye jamii kwani aweza kuleta madhara makubwa.

Kwa vile hayo yamesemwa sana hapa ndani na wapinzani wake na kitengo cha propaganda cha CCM kulivalia njuga jambo hili, ni wakati sasa Polepole na timu yake kupambana na majirani zetu wanaomwita Mzee Mkaidi kwa nguvu ileile wanayoitumia humu ndani.

Ila jambo moja la kujiuliza ni kuwa kwa nini kila mtu na akili zake anapata picha kuwa Mzee ni Mkaidi?

View attachment 1396496

Kiswahili cha wa-kenya kina matatizo. wanaweza kuwa walikuwa wanamaanisha ujasiri. Ukaidi hauna uhusianao na Hotuba ya jana kwa taifa, so possibly walimaanisha UJASIRI na si ukaidi.
Wa-Kenya wanaweza wakaongea statement kama hii, BERE YA KURA RIPA, wakimaanisha kuwa lipa kabla ya kula chakula. Tatizo ni Kiswahili, na si mantiki ya neno linalooneka hapo kwenye screen ya tv
 
Wewe ndiye unayepaswa kukaa kimya humu...na sitanii naweza kabisa kuifikisha hoja hii TCRA kwa upotoshaji kuhusu gonjwa hili na namna mnavyomdhihaki Rais...tayari PM na Rais mwenyewe wametoa tahadhari kwamba mitandao ijihadhari...Watch out...Kama mnadhani nyie ni wajanja mtadhibitiwa...Rais anasema hiki nyie mnapotosha makusudi kwa chuki zenu...Pamoja na tishio la Corona watanzania lazima tufanye kazi na Rais hajakosea kwa hili...hakuna nchi iliyosimama kufanya kazi...hata huko italia ambako wamekufa zaidi ya 5000 huku wengine wapatao 60,000 wakiwa wameambukizwa hawajasimama kufanya kazi...Sasa nyie mnapotosha kauli ya JPM aonekane kuwa hajali wakati sivyo...hatuwezi kuvumilia kuwaona nyie mnamsakama Rais pasipo sababu..I am just a citizen na Sina madaraka yoyote kwenye serikali hii..but this is our President and we have to respect him na kuungana naye to fight for this country..
 
Sidhani Kama uko sahihi katika hili.,!
Watangazaji wa TV na Radio za Kenya wanaongea Kiswahili na Kiingereza Fasaha kabisa.
Kusema Neno UKAIDI walikuwa wakimaanisha ati UJASIRU si kweli..!
Kwa Kiingereza Ukaidi ni STURBONESS na Ujasiri Ni BRAVENESS...Kwa hiyo wako sahihi kusema Ni UKAIDI wa Rais Magufuli kukaidi maelekezo sahihi ya kitaalamu kuhusu janga la Covid-19!!
 
Kabisa mkuu! Uko sahihi. Kiswahili cha Wakenya ni kibovu.

Utasikia anasema "Usibaki bikibiki kwa faranda" Yaani usipaki pikipiki kwenye varanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani Kama uko sahihi katika hili.,!
Watangazaji wa TV na Radio za Kenya wanaongea Kiswahili na Kiingereza Fasaha kabisa.
Kusema Neno UKAIDI walikuwa wakimaanisha ati UJASIRU si kweli..!
Kwa Kiingereza Ukaidi ni STURBONESS na Ujasiri Ni BRAVENESS...Kwa hiyo wako sahihi kusema Ni UKAIDI wa Rais Magufuli kukaidi maelekezo sahihi ya kitaalamu kuhusu janga la Covid-19!!
Tukio havina uhusiano na neno. Still, watangazaji Kenya hawawezi kuwa so harsh kwa Raus Magufuli, na hata kama wakiwa, basi sina shaka Serikali yao inaweza ikawahoji. Kuna oversight tu hapo itakuwa imefanyika na si kwamba wamemaanisha kinachoonekana kwenye maandishi hayo
 
Kuna upuuzi unataka kuletwa duniani and Magufuli is well aware with that.
Time will tell and numbers dont lie.Baada ya miezi miwili mje humu mtuambie whether he was right or wrong,ila mimi niko nae kwenye hili.He is right.Dunia imelikuza janga hili for reasons unknown to many.Hivi mlitaka awaambie mjifiche uvunguni?trend ya corona kwa Africa ikoje?watu wangapi wamekufa Africa?wangapi wapo seriously ill?tangu lini imeingia?Open up your eyes my fellow africans!Hili janga la Ulaya huko,wao wana janga moja tu corona,huku tuna mambo mazito zaidi ya hili,lazima akili yetu igawanyike vizuri,ukiibana sehemu moja yale mengine makubwa zaidi yatatumaliza.Ndivyo nilivyomuelewa jana.Corona ni hofu Italia,ila si lazima iwe hofu Tanzania.Mafua ya kawaida tu ni hofu Ulaya,vipi wewe na mie pua bapa,ushawahi kupoteza ndugu yoyote kwa flu?!hebu fungueni mioyo hiyo.
 
Wewe ndiye unayepaswa kukaa kimya humu...na sitanii naweza kabisa kuifikisha hoja hii TCRA kwa upotoshaji kuhusu gonjwa hili na namna mnavyomdhihaki Rais...tayari PM na Rais mwenyewe wametoa tahadhari kwamba mitandao ijihadhari...Watch out...Kama mnadhani nyie ni wajanja mtadhibitiwa...Rais anasema hiki nyie mnapotosha makusudi kwa chuki zenu...Pamoja na tishio la Corona watanzania lazima tufanye kazi na Rais hajakosea kwa hili...hakuna nchi iliyosimama kufanya kazi...hata huko italia ambako wamekufa zaidi ya 5000 huku wengine wapatao 60,000 wakiwa wameambukizwa hawajasimama kufanya kazi...Sasa nyie mnapotosha kauli ya JPM aonekane kuwa hajali wakati sivyo...hatuwezi kuvumilia kuwaona nyie mnamsakama Rais pasipo sababu..I am just a citizen na Sina madaraka yoyote kwenye serikali hii..but this is our President and we have to respect him na kuungana naye to fight for this country..

Bwana 1954, huwezi kuninyamazisha hapa JF. Only the moderator can ban me if I misbehave but no you or TCRA...!!Hii nchi ni ya WATANZANIA wote and we're all citizen of this country whether you're CCM member or CHADEMA etc. The problem we have now is that CCM MEMBERS thinks they are CLASS 1 CITIZENS of this country which is not!

Baba wa Taifa Mwl.Nyerere(rip) alituachia utamaduni kukosoa na kukosolewa. Kwamba KIONGOZI yeyote awe Rais au Nani LAZIMA AKUBALI KUKOSOA NA KUKOSOLEWA. Watz wanapo kuchagua/kukupa ridhaa ya kuwaongoza(siyo kutawala) haimaanishi kuwa wewe Ni MALAIKA kwamba unajua kila kitu na upo Juu ya Sheria....!!
Hii Ni nchi yenye mfumo wa Multipartism na Katiba ya JMT iko clear. Hivo usitegemee kuwa ati Rais Magufuli hatakosolewa kwenye maswala ya msingi yanayo lihusu Taifa letu kwa vile yet Ni Rais hilo sahau labda kama CCM mtalazimisha kubadili Katiba Tanzania irudi kwenye mfumo wa Singleparty system.

Maadamu kwa sasa tuna mfumo wa vyama vingi KUKOSOLEWA Ni lazima na kukosoa siyo dhambi wala kosa la JINAI labda kwa kutumia hizo MBINU za watu kubambikiwa kesi za Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha!
 
Tukio havina uhusiano na neno. Still, watangazaji Kenya hawawezi kuwa so harsh kwa Raus Magufuli, na hata kama wakiwa, basi sina shaka Serikali yao inaweza ikawahoji. Kuna oversight tu hapo itakuwa imefanyika na si kwamba wamemaanisha kinachoonekana kwenye maandishi hayo

Nakushauri uwasiliane na Prof. Kabudi au Ubalozi wa Kenya kwa ufafanuzi zaidi kuhusu hiyo taarifa.....maana hapa tutabishana mpaka mtondogoo....!
 
Kuna upuuzi unataka kuletwa duniani and Magufuli is well aware with that.
Time will tell and numbers dont lie.Baada ya miezi miwili mje humu mtuambie whether he was right or wrong,ila mimi niko nae kwenye hili.He is right.Dunia imelikuza janga hili for reasons unknown to many.Hivi mlitaka awaambie mjifiche uvunguni?trend ya corona kwa Africa ikoje?watu wangapi wamekufa Africa?wangapi wapo seriously ill?tangu lini imeingia?Open up your eyes my fellow africans!Hili janga la Ulaya huko,wao wana janga moja tu corona,huku tuna mambo mazito zaidi ya hili,lazima akili yetu igawanyike vizuri,ukiibana sehemu moja yale mengine makubwa zaidi yatatumaliza.Ndivyo nilivyomuelewa jana.Corona ni hofu Italia,ila si lazima iwe hofu Tanzania.Mafua ya kawaida tu ni hofu Ulaya,vipi wewe na mie pua bapa,ushawahi kupoteza ndugu yoyote kwa flu?!hebu fungueni mioyo hiyo.

Wewe unatakiwa kuwa wa Kwanza KUSHTAKIWA kwa Upotoshaji unaozungumziwa na Serikali. Hii dhana ya kudai Covid-19 Ni ugonjwa wa Wazungu Ni Upotoshaji mkubwa Sana...!
Covid-19 ilianzia China na Wachinazaidi ya 3200 wamepoteza maisha. Kauli za kwamba HUO NI UGONJWA WA WACHINA zilitamkwa na watu wakaidi Kama wewe akiwemo Rais Trump wa Marekani aliyesema hivo ni VIRUS VYA WACHINA....Leo Trump anajutia kauli yake maana kibao kimegeuka baada ya Wamerekani zaidi ya 200 kupoteza maisha mpaka sasa na maambukizi zaidi ya 60,000 na yanaendelea.

Italy walikuwa na mawazo haya ya kupuuza na kuchukulia POA.Leo Corona imemtikisa mpaka BABA MTAKATIFU mjini Vatican City!!Kwa Takwimu za Sasa Italy ndiyo imeathirika kuliko hata China. Zaidi ya vifo 4000+ vimerekodiwa mpaka Sasa....! Reason behind: KUPUUZA NA KUONA ATI NI UGONJWA WA WATU AU NJI FULANI..... !
 
Hivi ndio TV za nchi jirani zinavyo m-describe Mzee Baba, kama mtu MKAIDI.

Je, mkaidi ni mtu wa aina gani? Huyo kwa kiingereza ni Stubborn na huwa hafai kwenye jamii kwani aweza kuleta madhara makubwa.

Kwa vile hayo yamesemwa sana hapa ndani na wapinzani wake na kitengo cha propaganda cha CCM kulivalia njuga jambo hili, ni wakati sasa Polepole na timu yake kupambana na majirani zetu wanaomwita Mzee Mkaidi kwa nguvu ileile wanayoitumia humu ndani.

Ila jambo moja la kujiuliza ni kuwa kwa nini kila mtu na akili zake anapata picha kuwa Mzee ni Mkaidi?

View attachment 1396496

Sent using Jamii Forums mobile app
Tv gani hiyo imesema hivyo tuwekee tuone wenyewe kile wameongelea

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ndio TV za nchi jirani zinavyo m-describe Mzee Baba, kama mtu MKAIDI.

Je, mkaidi ni mtu wa aina gani? Huyo kwa kiingereza ni Stubborn na huwa hafai kwenye jamii kwani aweza kuleta madhara makubwa.

Kwa vile hayo yamesemwa sana hapa ndani na wapinzani wake na kitengo cha propaganda cha CCM kulivalia njuga jambo hili, ni wakati sasa Polepole na timu yake kupambana na majirani zetu wanaomwita Mzee Mkaidi kwa nguvu ileile wanayoitumia humu ndani.

Ila jambo moja la kujiuliza ni kuwa kwa nini kila mtu na akili zake anapata picha kuwa Mzee ni Mkaidi?

View attachment 1396496

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unasemaje? Hilo nalo ni jambo la kuwaalika CCM! Naona akili ziko tenge. Tangu lini Kenya ikasema la maana juu ya majirani zake? Tufikie wakati tusidandie kila habari na kuileta JF kwa majadiliano. Tujadili nini sasa!
 
Back
Top Bottom