CCM Msiseme Hamkujua Mambo Haya Ni Hatari Kwa Amani Ya Taifa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Msiseme Hamkujua Mambo Haya Ni Hatari Kwa Amani Ya Taifa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Jun 17, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nina hofu kubwa kwamba huko tuendako (si miaka mingi) Tanzania, hasa huku Tanganyika, amani itatoweka kabisa na watu wengi zaidi watapoteza maisha kwa sababu tu ama CCM haina uongozi au viongozi wake wanaongozwa na wasiojua uongozi. Sitaweza kurejea kila kitendo kinachofanywa na viongozi wa CCM (Chamani na Serikalini) kuashiria matatizo zaidi siku za usoni.
  1. Viongozi wa serikali wanazidi kupoteza trust ya wananchi kadri siku zinavyokwenda. Pinda huyu anayetetea posho za vikao kwa kauli za kimipasho kama ilivyoandikwa na Mwananchi 16 Juni, 2011 (".....Ni kwa bahati mbaya kwamba jambo hili limekuwa likikuzwa sana, mimi naamini kuwa ni jambo dogo, lakini kwa jinsi linavyokuzwa linaleta sura tofauti kabisa," alisema Pinda na kuongeza:
   "Hata Chadema, wabunge wake watakuwa wanamezea mezea mate, lakini sasa wafanyeje"...
   ) amepoteza sana umaarufu miongoni mwa wananchi ukilinganisha na ilivyokuwa miaka kama mitatu hivi iliyopita. Kwa nini.. wakati watu wanalalamikia shida halisi na ambazo wananchi tusiopenda siasa tumeanza kuzijua Wana-Chukua Chako Mapema bado wanajibu kama vile nchi nzima ni mazuzu watupu. Kwani si Pinda huyu huyu aliyelalamikia ununuzi wa VX V8 (Mashangingi) miaka michache iliyopita kwamba ni matumizi makubwa yasiyo sababu? Tofauti yake na matumizi ya mabilioni kulipa posho za vikao ni nini? Mungu anisamehe!...Huyu Pinda mpya ananichefua.
  2. Viongozi wa chama kama Nape nao utumbo mtupu! Baadhi yetu tumewachoka mno, japo najua wapo wanaowaunga mkono kwa sababu wamedanganywa na kuamini kuwa sisi tusiokubaliana nao ni wadini na eti tumetumwa na makanisa kuwaondoa madarakani. Wengine tayari wanafaidika kwa kuwa ni zamu yao (UVCCM-Pwani) hivyo wapo tayari kutetea uozo wa serikali na chama kwa gharama zozote pasipo kujali ni njia gani inatumika. Hawa viongozi wanachoweza kujitetea dhidi ya ufisadi ulioenea sana nchini ni kwamba mbona hata Slaa anapata mshahara mkubwa. Hili ndilo jibu. Kwa hiyo ufisadi hauna tatizo kwa kuwa CDM nao wanakula?
  3. Vituko vya Spika wa Kwanza Mwanamke katika Afrika Mashariki (na ...... wapi sijui) mnaviona pia. Ushabiki wa kijinga unaoendelea Jengoni ni hatari sana maana watu wanaotetea mambo ya msingi wanadhalilishwa na wajinga kushangiliwa. Wananchi hata wale wa level ya chini kabisa ya uelewa wameanza kumshitukia Bibi huyu na kilichomweka hapo kitini. Nao pia wanazidi kuchoka na "Chukua Chako Mapema"
  >>>>>>>>>Ninachokiona hapa na kuomba wanajamvi tukitazame kwa umakini unaostahili ni kwamba (hata nyie mnaona) wananchi wanazidi kuichoka CCM na viongozi wake. Wananchi wanazidi kuujua ukweli kwamba pamoja na kutumia fedha na mbinu nyingi, safi kwa chafu, kupata madaraka CCM, JK na Bosi wao RA hawawezi lolote zaidi ya kujitajirisha kwa ufisadi tena uliokosa haya. Sasa hivi pesa ngumu na ndiyo inaendelea kucontrol kila kitu; huduma, haki, upendeleo vyote hivi havipatikani bila kutoa hongo karibu katika kila sekta. Watu waliopaswa kubadili mwelekeo wa nchi juu ya rushwa/ufisadi aibu imewajaa sasa hata hawawezi kuwakemea wasaidizi wao. Kwa kuwa waliyofanya wao yanatisha ukilinganisha na wasaidizi wao hivyo wameamua kila mtu ale mahala pake ili walau kuwe na amani miongoni mwa walaji. Lakini bado amani haijapatikana hata huko ndani ya magamba.

  >>>>>>>>>Wananchi wakiendelea kuwachoka kina JK, Pinda na wenzake ni wazi uchaguzi ujao watawanyima kura CCM na inawezekana chama cha upinzani kupata ushindi hata katika nafasi ya rais kitu ambacho naamini (kwa kuwa JK atakuwa bado rais) madaraka hayatatolewa kwa mshindi na kwa kuwa wananchi watamjua mshindi huenda wengi wakaamua kuingia mtaani kudai ushindi apewe aliyeshinda na si anayeungwa mkono na dola. Matokeo yake mnayajua. Watu watauawa na hali haitaishia hapo kwa kuwa mambo ya visasi yataanza. CCM mnawajua! Usishangae akiibuka kiongozi mkubwa tu (ili kuungwa mkono na watu) akataja udini na upuuzi mwingine wowote kama sababu na baadhi yetu akili ya kuchuja "0" hivyo watafuata uzushi huo na mwishowe tutakuwa na machafuko mabaya sana.

  >>>>>>>>>Ushauri wangu kwa CCM na viongozi wake: Fanyeni lililo jema, msikilize malalamiko halisi ya wananchi na kutumia mbinu sahihi kuyatatua. Msijibu hoja za msingi kwa mipasho na badala yake zitafakarini kwa kushirikiana na waliotumwa kuzileta nchi iepuke shari zisizokuwa za lazima. Utajiri aliokwishapata mwajiri wenu RA na rafiki zake unawatosha kuishi kama wapo peponi hata baada ya mauti kuwafika kwa hiyo waambieni kuliibia taifa basi. Achani imani za mwaka 47 kudhani mtatuzuga kwa chumvi na kanga siku zote badala yake aminini kwamba mkitutendea mema tutawashukuru kwa kuwaamini na hivyo mnaweza kupata nafasi nyingine lakini si kwa nia za kujitajirisha na kupeana zamu za kutufilisi.

  Msiseme hamkujua kwamba upuuzi huu mnaofanya kupitia Spika, Pinda, Nape na wenzao unahatarisha uvumilivu wa wananchi ambao nyie hupenda kuuita Amani. Tangu mmeanza tamaa za utajiri mkubwa mkubwa hakuna amani Tz japo uvumilivu bado upo.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kaka hawa jamaa wanasoma wana elewa vyema wakisha mailiza wanawaza mkakati mchau zaidi ni wapuuzi zaidi hawa watu .
   
 3. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyo mizengwe msanii mtupu hakuna cha mtoto wa mkulima wala nini, ni fisadi asiye na huruma
   
Loading...