Ccm Msipochunga Mtaiteketeza Nchi Yetu

May 19, 2008
7
0
Hivyo viongozi waliopo madarakani wanachokifikilia ni kipi juu ya amani ya nchi yetu. Wanafikili kutumia mabavu na khofu ndio nguvu ya kuweka amani. Sivyo kabisa. Yote ni kuendelea kujenga uhasama na kuchukiana baina ya watanzania. Na ni hatali zaidi kwa kizazi kijacho. Hivyo ni pesa au madaraka yanayomfanya mtu hata asahau kuheshimu maamuzi ya laia. Kwa upande wa CUF na CCM zanzibar ndio imeshindikana. Yote ni sababu za ukiritimba wa wenye kushika mpini. Viongozi wa CCM tumikieni watu na sio wafuasi. Watu ndio taifa na wafuasi ndio chama. Mnapowekwa madalakani sio ni kuwatumikia waliowapa kula. Mutende yapasayo kwa jamii yote ya watanzania.

Fanyeni suluhu kwa halaka sana kwa wazanzibar CCM na CUF. Jeuri isiwapeleke huko. Sio vibaya kuangalia mifano iliyopita. Rais mstaafu Salmini Amour amekua hana thamani kwasasa na inafahamika ununda wake na kujipakazia kuwa yeye ni Comandoo. Sasa anashindwa kumtolea dhamana mtoto wake Amini Salimini aliefanya ubadhirifu.

Pia mambo haya yatatokea kwa Karume na watoto wake katika miaka michache ijayo Mungu akipenda. Viongozi musiwe mbali na kumbukumbu. Tendeni haki kwa watu wote. Wazanzibar wanahitaji amani, upendo na masikizano. Msisubili kuona michilizi ya damu katika vichocholo vya mitaa ya Zanzibari.

Watch
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom