CCM Msimdhalilishe Mama Maria Nyerere, Msilazimishe Ugomvi katika Familia ya Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Msimdhalilishe Mama Maria Nyerere, Msilazimishe Ugomvi katika Familia ya Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Mar 20, 2012.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Leo Nimesoma kwenye Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba Mama Maria Nyerere ametaka Vicent akemewe na Vile vile lazima Vicent Amheshimu Benjamin Mkapa.

  Sina Tatizo na Kauli ya Mama Maria bali nina Tatizo na HILA za CCM ( Shame on you CCM)

  CCM Muache Mama Maria Apumzike.

  1. Mama Maria Nyerere si Mwanasiasa ni kitendo cha Aibu kumuingiza Mkenge Mama huyu katika Malumbano ya Kisiasa yaliyoanzishwa na Mkapa.

  2. Mkapa ni Mtu Mzima Propaganda haziwezi kumsafisha Dhidi ya Kauli zake Dhidi ya Vicent

  3. Naiomba Familia ya Mwalimu Nyerere ( Madaraka, Makongoro na wengine) Kuweni Makini na CCM maana msipokuwa Makini Mama yenu anaweza kugeuzwa Kichaka cha Propaganda na Akaoneka si Mama wa Taifa bali Kituko katika Jamii. Hilo liko ndani ya Uwezo wenu, waambieni CCM kwamba Mkapa ni Mtu Mzima amerusha Shambulizi amejibiwa basi alimalize na si Kumtuma Mama Maria kwenye Vyombo vya Habari.

  4. Kwako Jakaya, Mwacheni Mama wa Taifa Apumzike. Mkapa ni Mtu Mzima na anaweza kujitetea


  Ni Ujumbe ambao ningependa kumfikishia Mama Maria Mwenyewe lakini niemshindwa naamini Watoto wake huwa wanapita hapa.
   
 2. T

  Thesi JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Well said
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wassira, Mkapa, Ole Sendeka na wengine wana haki ya kumnadi mgombea wa chama chao popote pale, lakini hawana haki (nasisitiza) ya kuleta ugomvi ndani ya familia ya mtu. Mwl Nyerere pamoja na kuwa baba wa Taifa lakini anayo familia yake huko Butiama. Kitendo wanachofanya Wassira na Mkapa sio tu kumchafua mmoja wa wanafamalia ya Mwl Nyerere lakini wanaelekea kuzua kutoelewana ndani ya hii familia. Waliona shida gani kumnadi mgombea wanayemtaka bila ya kuingilia familia ya watu?
   
 4. B

  BMT JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  jana tumejadili ili,au we mgeni humu,TUMECHOKA NA MAMBO HAYO,MOD ONDOA HII BWANA
   
 5. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,959
  Likes Received: 20,296
  Trophy Points: 280
  Huyu Mama Maria naye inabidi achanganye na zake, kina Mgeja wametumwa kumchota na mwisho wake ni kwa yeye kujivua, huu ndo ukweli, Mkapa ka-bipu' wamwache apigiwe kwani VN kajiunga na xtreme.
  Atulie, ni Mama tunayempenda na kumthamini sana, ukimya wake kwa mambo taka ya kina BWM utamfanya awe na manufaa kwa taifa lakini akichukua upande basi ajue bongo ya sasa hatuhitaji kukuona na mvi ndo tujue una busara
   
 6. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  wana jf naomba huyu ape tusimjadili kwenye jukwaa kwan mwaka 1995 akiwa nccr aliahidi akirudi ccm awe maiti sasa tunajadili msukule wanini?. ole sendeka hana usafi wowote kwani mwaka 2005 alipewa na makaburu wa samakis au tanzanite one mchanga na baadhi ya wana apolo wakateka hayo malori na kwenda nayo hivyo huyu nae fisadi tu:mullet:
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jamani tokea mwalimu atutoke ccm imekosa sifa ya kuwa chama cha siasa.
  Kwa sasa ukiwa mwanachama wa ccm akili zako zinaparaganyika mazima unabaki unawaza upumbavu tu!
  CCM hovyoooo!!!!!
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huwa napata wasiwasi sana fikra zako ndogo kama punje ya mchanga ulizo nazo

   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Bangi za usiku zinakusumbuwa wewe, ni nani aliyekwambia hapa kuna limit ya mijadala? kwa taarifa yako/yenu this is just a beginning huyu Mmakonde wenu wa Msumbiji ni lazima anyongwe tu kwa kosa la mauwaji ya Baba wa Taifa.
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  Kwa taratibu za boma, mwanaume ndo msemaji wa familia.
  Kauli ya Madaraka ndo kauli ya Boma la Nyerere,Huyu mama maria kachomekewa juu juu hajui chochote juu ya malumbano haya yaliyoanzia arumeru.
  Otherwise, mzimu wa Mwalimu Nyerere utawaandama wauaji wake milele.
   
 11. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka mama huyu alilia sana haswa pale ubinafsishaji ulipotia hodi msasani jirani na kwake,bibi wa watu alipiga ukugwi weeeeeeeeeeee kuhus kiwanja jirani na kwake kubinafishwa na project ya matofari kiwanja cha wajukuu zake kuchezea kikawa kiwanja cha biashra,hakuna aliyemsikia Bibi wa watu zaidi watu walimuona anabwatuka tu na uzee.

  Mungu saidia alikuwa Jakaya Kikwete aliyeingia madarakani kaingia leo kesho yake cha kwanza tunaona greda linabonda matofari ya Kiwanja jirani na kwa bibi huyu.Hivyo Bibi huyu na hakika Jakaya ana huruma nae hivyo basi awaambie wana CCM na dola wamuaache Bibi huyo vinginevyo bidiii zake zote alizofanya juu ya bibi huyu kupewa heshima na kuonekana tunu ya mke wa kiongozi mwenye heshima itavunjwa sasa hivi na kuleta kituko kwa jamii.Hakika ni Jakaya pekee mwenye uwezo wa kuwazuia CCM na Dola kumuacha mama huyu asiingizwe kwenye mchezo wa waliochafuka ili awasafishe wawe weupe kama dheruji wakati walipoyaanzisha bibi huyo alikuwa nyumbani akiendesha kwaresima yake na maombi ya kumuomba Mungu mumewe nae apate heshima anayostahiki kwa matendo yake ndani ya kanisa na hakuwa nao.

  Kwa kuwa JK ndiye aliweza kutatua kilio chake wakati ule na ndiye mwenye jukumu la kumtunza kwa sasa awakanye wale wote wanaotaka kufumua yaliyo lala,yasije yakampaka tope bibi huyu ambae watanzania tulio wengi hasa kizazi kipya tunamuona kama taswira ya mtu aliyeishi na Baba wa Taifa kwa ukaribu zaidi kuliko mtu yoyote yule chini ya uso wa dunia hii.Hivyo kuchafuka au kumsogezea maneno ya kumletea mama huyu aina yoyote ile ya mazungumzo ya mambo ya kampeni ya Arumeru ni kufumua historia isiyopendezwa kuwekwa kumbukumbu yaliyopita.

  Chonde chonde Rais Kikwete waaaonye wanaccm na dola inayomnyemelea mama huyo eti aweke sawa mambo!!!!!!!!!!!
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu Albedo umeleta hoja muhimu kwa heshima ya mama yetu Mama Maria Nyerere. Mkapa alienda Arumeru akauwasha moto,wamuache umuunguze aliyeanzisha. Tafadhari sana akina mzee Butiku, Salim, Warioba na wengineo naomba mwingilie kati kabla mama yetu kudhalilishwa kwasababu ya kutetea watu welevi,wazushi na mafisadi!
   
Loading...