CCM mpya siasa mpya na mustakabali wa uzalendo na demokrasia ya taifa letu

ramafosa

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
287
250
Wanajamii Forum,
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshishimiwa JPM kwa mwavuli wa chama chake CCM, watanzania tumeshuhudia mabadiliko ya uendeshaji siasa ambao ninauona ni hasi na unatishia mustakabali wa taifa letu kwa kasi kubwa.

Wapo wanaoaminishwa kuwa kuna kazi nzuri inafanyika chini ya CCM lakini kiukweli kuna ukakasi mwingi ambao usipokemewa mapema Taifa linakwenda kuangamia.

Inasikitisha kuwa ile tulichoaminishwa kuwa CCM kinabadilishwa kuwa chama cha wanyonge ni tofauti na tunachokishuhudia sasa hivi.

Inasikitisha kuwa sasa chama kinataka kurudi kule kule kilikokuwa kinakimbia ambako kilikuwa kimetekwa na matajiri wachache.

Ni wazi kuwa sasa kila anayeteka kulinda uovu na mali zake anakimbilia CCM na siyo chadema tena kama tulivyokuwa tumeaminishwa. Maana yake ni kwamba hata leo hii Lowassa akiamua kurudi CCM Polepole atapanda jukwaani kumsifia na kuwa karudi nyumbani?

Watu tulioaminishwa ni wauza madawa nao wakirudi tutaambiwa "wametubu" kwa hiyo tuwaache warudi nyumbani? Inasikitisha sana na inakatisha tamaa.

Kama Polepole na Mwenyekiti wangu Mheshimiwa Magufuli ndo siasa tumeamua kuzifanya ni hatari sana kwa mustakabali wa uzalendo na demokrasia ya Taifa letu.

Mwanga tulioanza kuuona umeanza kufifia kwa kasi ya ajabu. Kwa hiyo tumeamua kukumbatia wanachama wanaotafuta ulinzi wa mali, biashara, nyumba (hata kama hazijajengwa maeneo yanayoruhusiwa kisheria), na wala si imani au uzalendo kwa taifa letu? Hii ni aibu kubwa na ni hatari sana huko tuendako.

CCM hii ina upya gani na iliyokuwepo? Hii tu si kwamba "CCM ni ileile" bali ni CCM ambayo ni ya kuogopwa na kila Mtanzania anayelitakia mema Taifa letu awe upinzani au ndani ya CCM yenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,108
2,000
Hakuna anayeipenda CCM hata mmoja, ila wanalazimika ili kulinda matumbo yao, woga wa kuchafuliwa na pengine hata kudhuriwa. Out of kulinda maslahi yao Hakuna Mwenye mapenzi na CCM. Trust me
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom