figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Katika muundo mpya wa CCM ya awamu ya tano, tumeamua tuwe na CCM mpya ambayo ni CCM mabadiliko sio yale mabadiliko ya kuzungusha Mikono ya waru fulani.
CCM hii tunataka mtu mmoja awe na cheo kimoja. Na hilo tumefanikiwa kuanza ngazi za chini kwenye uchaguzi ulioisha wa ndani ya chama.
Sifa ya Sheria ni msumeno hukata hukata huku na huku, sasa ni zamu ya ngazi ya Kitaifa, tunataka kuona Kofia moja.
Sisi wananchi tunaomba Viongozi wetu wawe mfano wa kuonesha kwa vitendo dhana ya Kofia moja.
CCM tunaongea kwa Vitendo na rais wetu ni mtu sikivu
Naomba kila Mwanaccm ulipo, tukazanie hili swala la haki ndani ya chama
Namshukiru sana Mzee wetu M/mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, yeye kashauri kuangaliwa upya kwa utaratibu wa kupokezana vijiti katika uongozi wa juu wa CCM.
Hii Kampeni iwe ya nyumba kwa nyumba.
Mheshimiwa Bulembo kashatimiza kauli yetu ya Kofia moja. Kaonesha njia.
Uwenyekiti wa chama apewe Mangula au Kinana. Hii itasaidia kumbana mwenyekiti wetu wa chama tofauti na sasa. Ukimuuliza swali la chama anajificha kwenye kivuli cha Urais.
Kuondoka kwa Nyalandu itufumbue Macho umuhimu wa Kofia moja.
Nyalandu katuachia pengo japo tunajitutumua kwamba aende tu. Mwanaccm mwenzetu B. Membe alilizungumzia hili na kusema "Lazaro Nyalandu anaweza kubezwa, kutukanwa na kudharauliwa. Lakini ametuachia ujumbe mzito. Busara inataka tutafakari hoja zake.Tusipuuze!"
Ni wakati wa Kofia moja. Hii ya kufukuza watu bila kuwahoji wala kuwapa barua sio desturi ya chama chetu pendwa CCM.
Kumbukeni pale dodoma tulifanyia mabadiliko Katiba yetu na kuamua kupitisha mabadiliko makubwa ya katiba, ambayo yanapunguza idadi ya wajumbe katika vikao vya juu na pia kupunguza kofia za uongozi mwanachama mwenye cheo ndani ya chama, ubunge au serikalini.
Mabadiliko hayo yalipendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 13 mwaka jana.
Mabadiliko hayo yalitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliyemaliza muda wake, Nape Nnauye kwamba muundo wa chama umebadilika na mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa CCM, Toleo la 2012, Kifungu cha 22 na 23.
Tunaomba Daktari, Profesa, Mheshimiwa, Mwenyekiti wa CCM Rais John Pombe Magufuli ajiweke pembeni kama katiba inavyotaka.
Si rahisi kutumikia mabwana wawili. Tumekaa kimya sana lakini tunaona hakuna kinachoendelea kuhusu Kofia moja. Kuendelea kuwa na Kofia tatu ni kuvunja katiba.
Tutailinda katiba ya CCM kwa nguvu zote. Na hili wanaccm tunaungana.