CCM-MPYA chama kipya tawala Tanzania

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,531
8,615
Sasa hivi ni wazi kuwa Tanzania inatawaliwa na chama kipya kiitwacho ,CCM-MPYA, hii ni baada ya kuwa wazi kuwa chama kiliitawala nchi hiyo hadi mwaka 2017 kilipoondolewa baada ya mapinduzi baridi yaliohusisha kuwaondoa wale viongozi wajulikanao kama "CCM ina wenyewe" kwenye mkutano mkuu wa chama uliofanyika Dodoma
Mwenyekiti wa CCM alimkabidhi rasmi mwenyekiti wa CCM.MPYA ,JPM
BADO HAIJAJULIKANA KIREFU CHA JINA CCM MPYA

kuna kila dalili uongozi wa ccm mpya unaendelea kujiimarusha ambayo hasa itaongozwa na makada wageni ,na kazi ya kupanga safu iko chini ya mwenyekiti akisaidiwa na kijana wale aliyemsajili aliyekua na mrengo wa upinzani na uwanaharakati akishauriwa kwa karibu na wazeee kama Butiku na wengine

Bado haijajulikana hatima ya viongozi wa kundi lilokuwa linatawala la CCM,itakuwa ipi na watachukua hatua gani kujibu mapigo.

Vyama vya upinzani.vinafuatilia kwa karibu maendeleo ya mgawanyiko huoo uliozaa CCM MPYA.
 
Umenichekesha sana kwenye hitimisho lako hili'

''Vyama vya upinzani.vinafuatilia kwa karibu maendeleo...ya mgawanyiko huoo uliozaa CCM MPYA''

Kwa hiyo upinzani wanasubiri makada wa CCM wakatwe ili wawachukue kama walivyofanya kwa Lowassa na genge lake.

Halafu eti ndio tunaaminishwa kuwa hivyo ni vyama mbadala wa CCM! Have mercy upon us, O LORD!
 
Umenichekesha sana kwenye hitimisho lako hili'''Vyama vya upinzani.vinafuatilia kwa karibu maendeleo...ya mgawanyiko huoo uliozaa CCM MPYA''Kwa hiyo upinzani wanasubiri makada wa CCM wakatwe ili wawachukue kama walivyofanya kwa Lowassa na genge lake.Halafu eti ndio tunaaminishwa kuwa hivyo ni vyama mbadala wa CCM! Have mercy upon us, O LORD!

Hoja mfu kabisa hii. Kwa hivo Madabida na Sophia Simba wako CHADEMA tayari baada ya kufukuzwa CCM?
 
Hoja mfu kabisa hii. Kwa hivo Madabida na Sophia Simba wako CHADEMA tayari baada ya kufukuzwa CCM?

Lowassa-na-Sumaye-walipokuwa-CCM.jpg
 
Ccm mpya ni kitu kiingine kabisa na ccm hii ya kawaida, waatanza kuneemeka na uwaziri kuanzia uchaguzi wa 2020
 
Itawezekana kama baada ya utawala wa Magufuli apatikane mtawala mwingine mwenye mtazamo wake...

La sivyo CCM ni ile ile tu, na ukitaka kujua CCM ipo vipi fuatilia mijadala ya bunge...
 
Itawezekana kama baada ya utawala wa Magufuli apatikane mtawala mwingine mwenye mtazamo wake...

La sivyo CCM ni ile ile tu, na ukitaka kujua CCM ipo vipi fuatilia mijadala ya bunge...
Ccm bungeni inabidi..ujitoe ufahamu ,wapo.wabunge rafiki...zangu ukikutana nao.nje ..wana akili sana lakini wakiwa ndani ya bunge unashangaaa akili zimeenda wapi
Yaaani ukitaka kusurvive ccm.jitoe ufahamu,cheza music wa boss,unga mkono tuuuuuuu
 
Tumu ombee tu rais wetu akaze mwendo
kweli kabisa namuomba mungu amjalie heri na afya njema........ila nawaswas na dhamira maana badala ya kukiri ccm ndio imetuangamiza anaagiza kupambana na upinzani ambao kupitia upinzani huo ndio tumegundua haya madudu


kwan manager hakuwemo ktk kundi la ndiooooooooooooooooooo ???kwa hati ya dharula na maigizo yenu .....siku ubongo wenu ukijifungua kutoka gizani walah mtataman kujifiagia ...miili yenu na roho vitashindana kwa aibu kali...iam sure facts will prevail na usanii utaonekana tu. ni siasa tupu ya kuhuisha chama cha makanikia badala ya uzalendo.
 
Umenichekesha sana kwenye hitimisho lako hili'

''Vyama vya upinzani.vinafuatilia kwa karibu maendeleo...ya mgawanyiko huoo uliozaa CCM MPYA''

Kwa hiyo upinzani wanasubiri makada wa CCM wakatwe ili wawachukue kama walivyofanya kwa Lowassa na genge lake.

Halafu eti ndio tunaaminishwa kuwa hivyo ni vyama mbadala wa CCM! Have mercy upon us, O LORD!
Kama hukuelewa uliza, sisi kazi yetu ni kuongeza kuni na kusubiri mtokoto.
 
CCM sio dude la kuamini kabisa, CCM ni wasanii ambao hawakuwahi kutokea duniani, Singeli yao wanaijua wenyewe..

Uwepo wa CCM na watu wake ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi hii..........
 
Kama akili za upinzani za mwaka 1995 ndo akili za ccm 2017 tusiulizane tena nani aliyetuloga?
 
Kama CCM-MPYA haijapitia taratibu za usajiri wa vyama vya siasa basi ni hatari sana. Lakini kama CCM-MPYA haijafanyiwa usajiri wa vyama vya siasa basi hiyo bado ni CCM tu, ila toka kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 mgombea Urais wa CCM, Rais Dr Magufuli alikuwa ni mgombea binafsi (independent candidate) na slogan kubwa ilikuwa 'Magufuli for change' (M4C) na nembo pamoja na jina la CCM vilikuwa na font ndogo.

mc4.jpg

tmp_9158-m706153208-jpg.337351

Magufuli-620x308.jpg


Sources: Via Google
 
Back
Top Bottom