CCM MPs kukutana hadi usiku, MOTO!!!

Safi kabisa wanaccm. Tukiwaambia watu hapa kuwa Kikwete na wanaccm wanafanya kazi ya kuendeleza nchi, wapinzani wanapinga. Sasa wataona vitendo.
 
Safi kabisa wanaccm. Tukiwaambia watu hapa kuwa Kikwete na wanaccm wanafanya kazi ya kuendeleza nchi, wapinzani wanapinga. Sasa wataona vitendo.

Ongera Mkuu lakini umeisha sikia tena leo bungeni? peruzi peruzi utapata kinachoendelea Serengeti. nafikiri pia umepata kinachoendelea kwenye madini. Nafikiri unatakiwa kuedit ujumbe wako sehemu fulani.
 
Ongera Mkuu lakini umeisha sikia tena leo bungeni? peruzi peruzi utapata kinachoendelea Serengeti. nafikiri pia umepata kinachoendelea kwenye madini. Nafikiri unatakiwa kuedit ujumbe wako sehemu fulani.


Masaka anakurupuka kimawazo hata kimatendo .Hajui analo lisema .Yeye na CCM tu na CCM na yeye .hajiulizi wala hawazi .

JK anafanya jema huku na kule anafanya maajabu .Kitendo cha Serengeti na kwenye madini kinammaliza kabisa huyu JK na CCM yenu .Pale waziri akisimama na kutetea mwekezaji na mafisadi sasa sijui JK hapo anakuwa sehemu gani .Mke wangu hawezi kutetea jambo bila ya maekezo the same applis to JK .Asema haya na kumbe anawatuma mawaziri kutetea uozo.Kazi anayo sasa .
 
Ongera Mkuu lakini umeisha sikia tena leo bungeni? peruzi peruzi utapata kinachoendelea Serengeti. nafikiri pia umepata kinachoendelea kwenye madini. Nafikiri unatakiwa kuedit ujumbe wako sehemu fulani.

kakindomaster,

haya yote ni mambo ya uzushi tu kwa Kikwete. Kuna wabunge bado wana kambi za uchaguzi wa 2005 na hawataki kuziacha. Kikwete amekuwa Rais kwa hiyo wakubali tu matokeo na kujenga nchi.
 
kakindomaster,

haya yote ni mambo ya uzushi tu kwa Kikwete. Kuna wabunge bado wana kambi za uchaguzi wa 2005 na hawataki kuziacha. Kikwete amekuwa Rais kwa hiyo wakubali tu matokeo na kujenga nchi.

Na hii ya Ripoti ya Madini ni Chuki Mkuu?

Tunategemea Rais JK ataitolea maelezo ya kutosha

Mkuu Lunyungu

Nina wasiwasi mawaziri wanaweza kufanya kama South Korea, mnamkabidhi kila kilicho chake tu na kuondoka. Kumbe huyu JK ndio maana safari za USA haziishi anakwenda kuuza nchi huko. Watu amekuja Bush acha washangilie, safari ya watu kama bush itatutokea puani.
 
...ufisadi wake alipokuwa NSSF ulikuwa wa kizenji.
bwana weye hebu tueleze ndio upi ufisadi wa kizenji?

Kama ambavyo tunawabana Mkullo, Pinda, na Simba, the State House Minister of Propaganda, wanavyo toa public gaffes kila siku, na hapa pia tukichemsha, tutawajibishana kwa misingi ile ile

Mtu wa Pwani, kazi nzuri. Mwikimbi, tunasubiri majibu.
 
Mnanifurahisha sana ,yaani wengine wanasema vita vya panzi fulaha ya kungulu ,ila kuna waliozidi ambao wao husema vita vya tembo kifo kwa nyasi au ziumiazo ni nyasi.
Hao wakutane hadi asubuhi ni kwa ajili ya kusutana tu na si kwa maendeleo wanayotaraji wananchi ,yaani wakiondoka hapo itakuwa kila mmoja anajisifu na kusifiwa upande wake ,kama wengine mlivyoanza kusifu wakati siku zinapita na hali inarudi kama kawaida na kwa sasa ukiangalia hata pima joto ya upinzani imepungua ,mikiki na makeke ya akina Zitto na Slaa yanaonekana kuyeyuka kama mvuke wa turbine za steam ,umetoka kwa kasi na kuwanguza akina Lowasa na wenzake na sasa unaendelea kupowa. Nothing will be done to make them kukoma and others kuogopa au kuwa warning ,nothing.
Upinzani unaelekea kupoteza muelekeo na CCM wanachokifanya hivi sasa ,kukutana na mara unamsikia huyu kasema hivi yule kawambia msiogope ,hawa wanajaribu kujenga hoja ambayo mavuno yake ni kuweza kuwateka tena wananchi kwa kuwaaminisha kuwa CCM ndio chama pekee kinachoweza kusimamia nchi hii hasa pale inapoyumba.
Ukiangalia utaona upinzani umekosa kuitumia nafasi hii ya ufisadi kuisakama serikali kikweli kweli na badala yake imewaachia CCM kuyamaliza wenyewe kwa wenyewe na wakipeana hukumu wenyewe kwa wenyewe ,kwa kadiri wanavyohisi hapa panaweza kupunguza makali,wapinzani wameshindwa kuitumia nafasi ya kukosekana umeme kwa Unguja kwa kiasi ya mwezi sasa ,hizi ni oputunity ambazo zinaweza kutumika na kuiangusha na kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa haraka zaidi na ndizo chances zinazotumika sehemu nyengine duniani zenye vyama vingi vya siasa na sio kukaa blah blah na kusema ,fulani na fulani wanahusika na hili na lile ,kitu ambacho wanakitumia CCM ni kupangua na kuweka mwengine wakihesabu wameshaondoa udhia na upinzani utaanza kutafuta hekalu lingine kuiandama serikali ndio ukaona Upinzani mara unaibua hili mara lile ,huu upinzani umekuwa kama machine ambayo ni computarised kuirekebisha CCM bila ya kuiathiri.
CCM kwa jinsi walivyojipanga ni kuwa mmoja wao akishindwa kuvumiliwa basi wanamuondoa na utawasikia wakisema alilolifanya ni lake binafsi Chama wala serikali haihusiki , hivi kwa kweli sivyo inavyotakiwa ionekane ni lazima kwa hali yeyote lawama na madai yabebeshwe serikali iliyopo madarakani sio mnaibua maovu halafu CCM kwa hila zao wanambebesha mtu mmoja ,mfano wa Balali utaona kila mtu amemsakama Balali wakati jambo linahusu wizara nzima na serikali yake ,kwa nini awe balali peke yake ,au kwa nini awe Lowasa peke yake na wenziwe watatu ,ule mtiririko wote ulikuwa ukwapuliwe kwa wizara nzima.
Kubadilisha mawaziri sivyo inavyotakiwa ,umebadilisha mawaziri basi mambo yamekwisha,hakuna kesi hakuna sababu ,just tunaambiwa utendanji wao haukufikia kiwango ,watu wameshachukua mishahara kibao ,halafu wanaondolewa hivi hivi tu , hizi zitakuwa ndio mbio za vijiti ,wakti watu hawa sababu za kuondolewa zipo ,ubadhirifu wa mali ya taifa ,kama ni kwenye mbuga ,kama ni kwenye misitu kama ni kwenye fedha ,uchunguzi unaendela ,watachunguzwa wangapi ?
Vyama vya upinzani inaonekana navyo vinawapiga chenga wananchi kwani havieleweki msimamo wao upo wapi kama ni kuibua hoja au ni kuibua hoja na kuona sheria inafuata mkondo wake ,na sheria sio mtu kujiuzulu , mtu amejiuzulu kwa nini amejiuzulu ni lazima ijulikane kwa undani na wananchi wajue amejiuzulu kwa kuwa mambo aliyotuhumiwa nayo si kweli au ni kweli ,kama si kweli ni nani mhusika na kama ni kweli sheria zipi zimefuatwa ,mbona watu hawa tunapigana nao vikumbo mitaani .
Kuna kiongozi mmoja alisema kuwa kama serikali haitachukua sheria dhidi ya waliohusika atawashawishi wananchi waingie mabarabarani ,kudai hatima ya ufusadi .
Niliposema pima joto ya upinzani imeanza kushuka nilikuwa na ushahidi wa huyu Mheshimiwa Zitto ambae baada ya kuibua sakata lake alikuwa kama lulu kila sehemu akifika na akihitajiwa angalau watu wamuone na kumpongeza na kumshangilia kuwa ni shujaa lakini leo hii ,hata akipita karibu mpaka uambiwe ndio yule ,kwa maana ile kasi yake imeyeyuka na ule mvuto na hisia za watu kwamba wamepata shujaa zimeanza kudidimia.
Nasema nguvu ambayo aliipata Mheshimiwa Zitto asitarajie kama itaweza kuibuka au ataweza kuipata tena ,it is gone forgood,kwa wakati ule angeweza kuushawishi umma na kuuamrisha vile atakavyo yeye na kama angekazania kuziendeleza nguvu zile basi leo Tanzania tungekuwa pengine hawa vigogo na vigome vyote vingelikuwa vinahariana kwani umma umeamshwa na hautaki kusikia habari za tunaunda kamati.
 
...................mwanahalisi la leo limeuhusisha moja kwa moja MTANDAWO wa kikwete 2005..moja kwa moja na wizi wote uliotokea kwenye EPA....hata wosia wa ballali...unatuhumu watu ambao ni wana mtandao na tayari unaaza kusambaa ...
 
Mkuu Wangu Halisi,

I love it, saafi sana, sasa mkuu kuna jamaa yangu amekuona hapo Dodoma, nishitue kama bado upo hapo ili nikupe mikoba zaidi pa kwenda kuchota more dataz,

Tanzania, tumetoka mbali sana kisiasa, kuna ambao hawakuyaona ambayo wengi tuliyapitia huko nyuma ya jinsi tulivyokuwa tumebanwa, mimi Town yaani Dar, zamani niliwahi kuishi na mkali wangu anayeitwa Bob Bayona, yaani wing moja kwenye gorofa moja Down Town, ambalo ndani lina hoteli ya Son-Afrique Hotel, next to Business College,

Bayona, the man alikuwa msomi sana na mtu mweye kichwa hasa, lakini the guy alikuwa mlevi sijawahi kuona, akishalewa alikuwa na tabia ya kusema hovyo sana kuhusu ubovu wa serikali kama tunavyosema hapa JF yaani kukosoa, man! siku moja saa kumi na moja za asubuhi watu tunarudi kutoka mangomani, ilikuwa Jumapili unajua enzi zile mambo yote yalikuwa Msasani Beach kwa JPP na Choggy, tukakuta jengo zima limezingirwa na watu hivi design design, duh tukaambiwa hatuwezi kuingia ndani mpaka wamalize shughuli zao, kuja kushitukia eti jamaa ni maajenti wa Serikali wamekuja kumchukua Bayona kwamba anataka kupindua serikali ya Mchonga, daaamn!

Hata wafagiaji wa lile jengo na Hotel could not believe it, I mean the man was so loved in the building and so harmless kwamba hata watoto wadogo mle jengoni wasingeweza kuamini, halafu jamaa all the time kama hayuko kazini ameutwika ugimbi, sasa atapindua vipi serikali? Tulipaoiifutailia zaidi ile ishu huko kwa wakubwa tukaambiwa, hivi huwa hamumsikii akisema sema hovyo kuhusu serikali, Bayona, na kwamba alikuwa akishirikiana na Ngaiza na wengine kina MCgheee, alipelekwa somewhere kisiwani for the next at least three to four years, siku alipotoka hatukuamini jinsi mkulu aliyekuwa na afya njema na jitu miraba minne halafu unajua jamaa alikuwa lightskinned hivi mweupee ukim-cheki kwa wasi wasi utadhani mtishi, wote tuliomuona tulilia machozi!

Sasa my point ni kwamba ni rahisi kwetu sisi hapa kusema na kudharau, baadhi ya wabunge na wananchi wengine kwa ujumla, kama kina Kubenea, wanaojaribu kwa kila hali kwa kujitoa mhanga, kuikoromea serikali kwa faida ya sisi wananchi, sasa hivi kuna njama kubwa sana inapikwa ya kumtoa Spika, sawa kuna some ishus ambapo wanaonekana kuwa hawako na sisi, lakini wakuu ninaomba kusema kuwa sometimes sisi wananchi tunahitaji ku-appreciate madogo yanayotafutwa na viongozi wetu, regardless ya vyama vyao kinachofanyika sasa hivi bungeni ni hatua kubwa sana, wakuu ukilinganisha na tulikotoka as a nation hasa kwa wale tulioona na kuishi angalau kidogo on zile enzi za noma, leo tuna wabunge ambao wako radhi kufanya anything ili ishu nzito za wananchi zisisemwe kabisa, tena wengine ni vijana kama sisi!


Naomba kutoa Hongera kwa wabunge wetu wote wanaotupigania sisi wananchi bungeni, kwa kazi nzito wanayoifanya huko bungeni, kuna wananchi ambao tuko nyuma yenu, na mtalipwa na Mungu tu!

Mungu Aibariki Tanzania.
 
Mkuu Wangu Halisi,

Hata wafagiaji wa lile jengo na Hotel could not believe it, I mean the man was so loved in the building and so harmless kwamba hata watoto wadogo mle jengoni wasingeweza kuamini, halafu jamaa all the time kama hayuko kazini ameutwika ugimbi, sasa atapindua vipi serikali? Tulipaoiifutailia zaidi ile ishu huko kwa wakubwa tukaambiwa, hivi huwa hamumsikii akisema sema hovyo kuhusu serikali, Bayona, alipelekwa somewhere kisiwani for the next at least three to four years, siku alipotoka hatukuamini jinsi mkulu aliyekuwa na afya njema na jitu miraba minne halafu unajua jamaa alikuwa lightskinned hivi mweupee ukim-cheki kwa wasi wasi utadhani mtishi, wote tuliomuona tulilia machozi!


Mungu Aibariki Tanzania.

....hiyo ndio Legacy ya Nyerere na tukisema alikuwa Dikteta Mwanakijiji anatuita wazushi.
 
...................mwanahalisi la leo limeuhusisha moja kwa moja MTANDAWO wa kikwete 2005..moja kwa moja na wizi wote uliotokea kwenye EPA....hata wosia wa ballali...unatuhumu watu ambao ni wana mtandao na tayari unaaza kusambaa ...

Katika miaka kadhaa iliyopita, JF tumekuwa wa kwanza mara zote kutoa habari sensitive humu jamvini wakati bado ziko moto kabisaaa kabla hazijaonekana popote pale. Chale zangu zinanielekeza nisitoke kabisa mtandaoni kwani dakika chache zimebaki kuja kuona lazi za Balali zikimwagwa humu...

Invisible, fanya vitu vyako................. Embu mwaga huo wosia mzee. All eyes on JF!!!
 
Back
Top Bottom