CCM MPs kukutana hadi usiku, MOTO!!!

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
614
Wabunge wa CCM wamekutana jana kuanzia saa 11 jioni hadi saa tatu usiku chini ya Mizengo Pinda, kikao ambacho tofauti na siku za nyuma, Mwenyekiti wa kikao hicho (Pinda) anaelezwa kuwapa wabunge uhuru zaidi ya kuzungumza na kuwasilikiliza badala ya yeye kuwataka waseme anavyotaka. Wabunge waliochangia walicharuka na kusema, "Hatutaacha kujadili EPA na Richmond hadi kieleweke" maana kwa sasa hizo ni ajenda za wananchi ambao wanataka majibu sahihi na hatua kuchukuliwa..... Walisema hizo si ajenda za wapinzani kama Waziri mmoja alivyosema...... Mwingine alisema CCM ina matabaka yaani, A,B na C, wakikumbushia kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wa CCM Arusha ambao walituhumiwa kutoa rushwa ya Sh 400,000 na walizuiwa na CCM kugombea nafasi ya Uenyekiti mkoa na NEC kupitia mkoa. Wanasema wao bado ni watuhumiwa na walikubali maamuzi ya chama, leo hii wanaotuhumiwa kuhusika Richmond, EPA na Rada tena kwa maamuzi ya BUNGE na WAKAGUZI HALALI wanaendelea kuwa wajumbe wa vikao vya juu vya CCM ikiwa ni pamoja na KAmati Kuu, NEC na mmoja ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama!!!!

Kazi mwaka huu ipo....
 
Wabunge wa CCM wamekutana jana kuanzia saa 11 jioni hadi saa tatu usiku chini ya Mizengo Pinda, kikao ambacho tofauti na siku za nyuma, Mwenyekiti wa kikao hicho (Pinda) anaelezwa kuwapa wabunge uhuru zaidi ya kuzungumza na kuwasilikiliza badala ya yeye kuwataka waseme anavyotaka.

Mkuu Halisi,

Heshima mbele mkuu, tupo ukurasa mmoja, nilisema kwenye dataz huko nyuma kuwa Muungwana amewapiga marufuku viongozi wa juu wa serikali na CCM kuwatisha wabunge, angalau hii italisaidia taifa maana najua kikako kijacho cha bajeti kutakuwa na moto mkali sana, ngoja tuzifuatilie kwa karibu yaaani tha dataz!
 
... Mwingine alisema CCM ina matabaka yaani, A,B na C,

wakikumbushia kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wa CCM Arusha ambao walituhumiwa kutoa rushwa ya Sh 400,000 na walizuiwa na CCM kugombea nafasi ya Uenyekiti mkoa na NEC kupitia mkoa.

Wanasema wao bado ni watuhumiwa na walikubali maamuzi ya chama, leo hii wanaotuhumiwa kuhusika Richmond, EPA na Rada tena kwa maamuzi ya BUNGE na WAKAGUZI HALALI wanaendelea kuwa wajumbe wa vikao vya juu vya CCM ikiwa ni pamoja na KAmati Kuu, NEC na mmoja ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama!!!!

...Spot on!, inanikumbusha enzi za "usipowajibika ole wako, utakumbwa na fagio la chuma! "

na wasipofanikiwa kuwang'oa kwenye hizi kamati za Chama na zile za Bunge, tumekwisha!!!
 
Wengine sasa tunafungua macho na masikio na kuyaelekeza Dodoma, Bongo, Danganyika.
 
Hii itakuwa safi sana maana wabunge watapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao. Haya mambo ya kufuata wanachosema wakubwa yalifanya wabunge wetu waonekane ni mazezete wakati akili wanazo. Ndio nikasema unaweza ukaonyesha utii kwa wakubwa wako bila kuuza uhuru wa kufikiri. Tunataka siasa za nchi yetu ziendeshwe kwa minajiri ya kushindanisha mawazo badala ya ujanjaujanja. Right step in the right direction.
 
•Wabunge CCM: Tutakufa na mtu

Waitahadharisha Serikali kuhusu Richmond

Na John Daniel, Dodoma

WABUNGE wa CCM wamezidi kukasirishwa na vitendo vya kifisadi na kuitumia Serikali salamu za tahadhari, kwamba watakufa na mtu iwapo hawatapata taarifa ya kina kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu hatua kali dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa Richmond.

Katika hali isiyotarajiwa, wabunge hao wameonya kwamba hawatakuwa na huruma wala kulindana kichama, juu ya suala hilo zito kwa maelezo, kwamba hivi Sasa Watanzania wasio na hatia wanaumia kwa kukabiliwa na ugumu wa maisha, kutokana na mabilioni ya fedha kutumika kulipa kampuni hewa bila kuzalisha umeme kama ilivyotarajiwa.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge jana, wabunge hao walisema ili kuepuka lawama na kuhakikisha kwamba wanatekeleza azma yao ya kusafisha Serikali ya CCM dhidi ya ufisadi, walipanga kuwasilisha mapendezo yao katika kikao cha wabunge wa CCM kilichopangwa kufanyika jana jioni.

"Tunatarajia taarifa iliyokamilika na ya kina kuhusu hatua kali zilizochukuliwa dhidi ya mafisadi wote, wengine walishaachia ngazi, lakini wengine bado wapo wanaendelea na kazi zao serikalini.

"Tunataka kujua wamechukuliwa hatua gani na kwa nini wao hawajakaa pembeni, hapa hakuna kulindana wala kufichana ukweli, lazima haki itendeke," alisema Mbunge machachari wa CCM kutoka Kaskazini.

Alipoulizwa iwapo taarifa hiyo haitawagusa wanaoendelea na kazi zao serikalini na kusomwa jumla jumla kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa, Mbunge huyo alisema:

"Unajua, katika hili hakuna mchezo, kuna kitu ambacho nikisema sasa hivi wanaweza kutafuta njia ya kukwepa au ... tutakufa na mtu yeyote anayeleta mchezo, ili Serikali ijue kwamba tumeamua, mimi mwenyewe nitawasilisha mapendekezo yangu katika kikao cha wabunge wa Chama leo (jana) jioni." alisisitiza.

Naye Mbunge mwingine kutoka Tanga, alisema yeye na wabunge wengine wanatarajia kwamba Serikali itatoa majibu yanayojitosheleza na yenye kujibu maswali magumu ya Watanzania wote bila kuogopa mtu, wala kuoneana haya.

"Bunge lilifanya kazi yake, sasa tunasubiri Serikali ijibu na tunaamini majibu yatakuwa mazuri tu, hata wale ambao hakuwajibika kuacha kazi zao, lazima hatma yao itakuwa katika majibu ya Serikali katika Bunge hili, kama Serikali haitafanya hivyo, basi tutaanzia hapo, subiri tu, utaona muda ukifika, japo hatujui ni lini taarifa hiyo itawasilishwa," alisema Mbunge huyo.

Wabunge wengine waliozungumza na Majira walionesha nia ya dhati ya kutaka mabadiliko, huku wengi wao wakitaka viongozi wa Serikali waliokabidhiwa madaraka ya umma kubadilika na kutambua kwamba makosa yao madogo ni mateso kwa Watanzania zaidi ya milioni 30.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Spika Bw. Samwel Sitta, alitangaza kwamba wabunge wote wa CCM wangekutana katika kikao cha chama hicho jioni katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Kikao hicho kilitarajiwa hata hivyo kutanguliwa na kile cha uongozi wa chama hicho ambacho jana saa 5 asubuhi.

Kwa upande wao wananchi waliozungumza na Majira walidai kwamba majibu ya hatua dhidi ya watuhumiwa wa Richmond ni mtihani wa pili kwa Rais Jakaya Kikwete na ni mtihani wa kwanza kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na kwamba iwapo watashindwa kusema ukweli, itakuwa ni dosari kwao.

Katika Kikao cha 11 cha Bunge Aprili mwaka huu, Bw. Pinda, aliahidi Serikali kutoa majibu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa Richmond, huku akisisitiza kwamba suala hilo linahitaji umakini wa hali ya juu kwa kuwa linagusa maisha na maslahi ya watu moja kwa moja.

Katika mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge yaliyowasilishwa bungeni mwaka huu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Kamati hiyo ilitoa jumla ya mapendekezo 23 ikiitaka Serikali kuyatekeleza na kutoa jibu ndani ya Bunge.

Moja ya mapendekezo hayo ni kuwachukulia hatua kali wote waliohusika, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani, kuwafukuza kazi watumishi wa Serikali akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika na wote waliohusika kwa njia moja au nyingine na kashfa hiyo.

SOURCE: http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6898
 
Aliyechokoza alikua Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye badala ya kuzungumza mambo yake ya Bajeti, aliwaambia Wabunge wa CCM wajadili bajeti waache kuzungumzia mambo ya Richmond na EPA kwa kuwa hizo ni ajenda za wapinzani, na aliposema kwani wapo wabunge wa CCM wenye ajenda hizo, wakaitikia kwa sauti, "tupooooo!!!!!" na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!" akashangiliwa sana
 
Na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!"

Mwanzo mzuri! Natumai wabunge hawa watatekeleza hayo wanayosema pembeni, badala ya kuwa na nidhamu ya woga.
 
Aliyechokoza alikua Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye badala ya kuzungumza mambo yake ya Bajeti, aliwaambia Wabunge wa CCM wajadili bajeti waache kuzungumzia mambo ya Richmond na EPA kwa kuwa hizo ni ajenda za wapinzani, na aliposema kwani wapo wabunge wa CCM wenye ajenda hizo, wakaitikia kwa sauti, "tupooooo!!!!!" na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!" akashangiliwa sana
Inasikitisha sana waziri badala ya kutetea maslahi ya taifa anasema EPA na richmond ni za wapinzani!kwa hiyo kumbe wapinzani ndo wanatetea maslahi ya taifa!Bora wabunge wa CCM wameamka sasa!
 
Aliyechokoza alikua Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye badala ya kuzungumza mambo yake ya Bajeti, aliwaambia Wabunge wa CCM wajadili bajeti waache kuzungumzia mambo ya Richmond na EPA kwa kuwa hizo ni ajenda za wapinzani, na aliposema kwani wapo wabunge wa CCM wenye ajenda hizo, wakaitikia kwa sauti, "tupooooo!!!!!" na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!" akashangiliwa sana

Good boy! Ole Sendeka.
Huo ndio utetezi wa wananchi tunaohitaji kuusikia,siyo kuwaziba watu midomo na kuwatisha wasiseme klichowapeleka Dodoma na kuwafanya mithili ya wanafunzi wa chekechea.
 
waziri badala ya kutetea maslahi ya taifa anasema EPA na richmond ni za wapinzani!kwa hiyo kumbe wapinzani ndo wanatetea maslahi ya taifa!Bora wabunge wa CCM wameamka sasa!

Huyu waziri ndiye wa kukamata vizuri ana kaufisadi ndani ya moyo wake. Ongera sendeka najua huyu jamaa hana mchezo
 
hivi mmemsahau mustapha mkulo mapema namna hii? ufisadi wake alipokuwa NSSF ulikuwa wa kizenji. nendeni pale mkawaulize waliokuwa naye pale. ,nadhani pesa za kampeni ya ubunge angezipata wapi?
bado safari nin ndefu. na msitegemee mengi toka bunge la dodoma, mafisadi wamejizatiti sana kuliko tunavyodhani.
 
Aliyechokoza alikua Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye badala ya kuzungumza mambo yake ya Bajeti, aliwaambia Wabunge wa CCM wajadili bajeti waache kuzungumzia mambo ya Richmond na EPA kwa kuwa hizo ni ajenda za wapinzani, na aliposema kwani wapo wabunge wa CCM wenye ajenda hizo, wakaitikia kwa sauti, "tupooooo!!!!!" na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!" akashangiliwa sana

Halafu mtu kama huyu ndo ameteuliwa kuwa waziri wa fedha ambako kuna BOT.

Si ndo atazidi kuzichota? maana wapinzani ndo wamezusha kuwa kuna hela zimechotwa...

Muungwa nakupa pole una kazi sana na hao mawaziri wako. Labda uwapeleke tena Ngurdoto.

Kaazi kwelikweli
 
hivi mmemsahau mustapha mkulo mapema namna hii? ufisadi wake alipokuwa NSSF ulikuwa wa kizenji. nendeni pale mkawaulize waliokuwa naye pale. ,nadhani pesa za kampeni ya ubunge angezipata wapi?
bado safari nin ndefu. na msitegemee mengi toka bunge la dodoma, mafisadi wamejizatiti sana kuliko tunavyodhani.

bwana weye hebu tueleze ndio upi ufisadi wa kizenji?
 
Hii itakuwa safi sana maana wabunge watapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao. Haya mambo ya kufuata wanachosema wakubwa yalifanya wabunge wetu waonekane ni mazezete wakati akili wanazo. Ndio nikasema unaweza ukaonyesha utii kwa wakubwa wako bila kuuza uhuru wa kufikiri. Tunataka siasa za nchi yetu ziendeshwe kwa minajiri ya kushindanisha mawazo badala ya ujanjaujanja. Right step in the right direction.

Tusubiri tuone kama wabunge wa CCM watafanya kweli na kuacha kufuata mstari wa chama, maana kikao kilichopita pia tuliambiwa Bunge litawaka moto, na hatukuona moto wowote bali zilikuwa ni cheche tu za hapa na pale.

Si ajabu wameshafundwa kwamba pamoja na kuikosoa serikali, lakini msivuke mipaka na kuiharibu kabisa serikali. Tuwape siku 10 za kwanza tuone kama watakuwa na uhuru wa kweli wa kujadili kero mbali mbali za Watanzania.

Pia tunataka wajadili Kiwira na kuishinikiza serikali irudishe umiliki wa mgodi huu kwa Watanzania na pia ripoti ya madini waijadili na kuishinikiza serikali iyafanyie kazi mapendekezo yaliyotolewa haraka iwezekanavyo.
 
Sasa hivi wataamka kwa sababu tatu kubwa:

i) hakuna anayetarajia uwaziri tena

ii) ule mzuka wa umaarufu wa JK uliokuwa unatisha kila mtu umekwisha. Kwa hiyo sasa kila mtu yupo huru kusema na kumsema JK sio dhambi tena kama ilivyokuwa mwanzoni

iii) wabunge wa CCM wameona wenzao wa upinzani wanavyohusudiwa na wananchi. Hakuna mwanasiasa anayetaka kujenga uadui na wananchi. Ilifika mahala ilikuwa ni aibu kusema mimi ni mbunge wa CCM.

Nasikia pia hata mawaziri wana wakati mgumu sana huku mitaani na hasa mikoani, wananchi wanawadharau sana. Sasa yote haya yanawafanya wabunge waanze kujirudi hasa ukizingatia 2010 ipo karibu.
 
Courtesy of competitively contrasting and combative contesting courtesants.
 
Aliyechokoza alikua Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye badala ya kuzungumza mambo yake ya Bajeti, aliwaambia Wabunge wa CCM wajadili bajeti waache kuzungumzia mambo ya Richmond na EPA kwa kuwa hizo ni ajenda za wapinzani, na aliposema kwani wapo wabunge wa CCM wenye ajenda hizo, wakaitikia kwa sauti, "tupooooo!!!!!" na ndipo akasimama Ole Sendeka akasema, "mimi nimetumwa na watu wa Simanjiro, kuwatetea, kuna matatizo ya zahanati, shule na kadhalika, serikali haina fedha, leo kuna fedha bilioni 133 watu wamegawana kama zawadi ya birthday munasema tusizungumze!!. nitasema tu!!!" akashangiliwa sana

Mimi bado sijawa na imani sana na hii hatua. Maana kadiri hali ninavyoiona ni kwamba chama tawala kiko juu kabisa katika mfumo wa utawala; ikifuatiwa na serikali. Bunge na mahakama vinaburutwa tu.

Labda yawezekana katika kundi la mafisadi elfu, kunaweza kutokea wenye nia njema wawili. Huwezi kujua.
 
CCM ni moja na msitegemee chochote kutoka kwenye hiyo Caucus yao. Kinachofanyika hapo ni kuwekana sawa tu na in the process kutakuwa na wapayukaji kama Sendeka et al but, mwisho wa siku business as usual mwendo mdundo....

By the way its good to see "tamaa ya fisi kumfuata mwanadamu kwa kudhani mikono yake itaanguka" keep good work na endeleeni kuishi in fantasy!
 
CCM ni moja na msitegemee chochote kutoka kwenye hiyo Caucus yao. Kinachofanyika hapo ni kuwekana sawa tu na in the process kutakuwa na wapayukaji kama Sendeka et al but, mwisho wa siku business as usual mwendo mdundo.
jamani hata kwenye maslahi ya taifa?CCM kama chama hakina kosa!ila kuna watu
ndani ya CCM wanatumia huo mwanya kufisadi!sasa waziri kweli anasema EPA ni ya wapinzani jamani!
halafu unasema Sendeka ni mpayukaji!hivi kweli wewe unaesema hivi ni mtanzania au?
 
Back
Top Bottom