CCM MP's are simply Selfish, Incompetent, Insecure and fearful. Simply Pathetic! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM MP's are simply Selfish, Incompetent, Insecure and fearful. Simply Pathetic!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nitasemaukweli, Jun 16, 2011.

 1. n

  nitasemaukweli Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia kwa kirefu jinsi ya experiences za MP's wa ccm. CCM is really full of selfish people and we definately can call the so. Most of them sit in parliament just to receive 'posho' and those 'allowances' then head home. We see them all the time when they show knowledge deficiency with their votes, failed policies and they can't even ask questions neither useful dialog. Sometime you can't imagine what kind of people are these and more so where they came from. You might come to the conclusion that these MP's maybe they don't live within Tanzania society or just foreigners.

  Several past sessions tell us these MPs are insecure either weak or just wait for orders. CCM MP's you see them always wait for orders and match to vote while their mouth shut, dress like important people in society. One thing we know is this, they constant worry for their jobs and more so if they will get nominations next election. How do we change them? Here are some of the solutions, let's stop ccm for paying them bribes in exchange for their votes and numbness. Also, once we get our constitution we will forget these kinds of people for good.

  "Just simply pathetic to say"

  Wewe unafikiriaje kuhusu ajira ya wabunge wa ccm? Wanamfanyia kazi nani? Tumia wakati huu kupeleka ujumbe maalumu kwa ccm na wabunge wao, tunajua wanashinda humu na simu za serikali kusoma JF ... ajabu hawajifunzi lolote kama walivyokuwa mashuleni.

  Tanzanian Affairs » REPORT ON RICHMOND SCANDALHome » Insight » PoliticsPreconditions for an Effective Constitution for Tanzania
  allAfrica.com: Tanzania: Needed in 2011 - a Radical Budget
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Maliza shule kwanza bwana mudogo, your presentation is full of grammatical mistakes and misspellings.
  Maliza shule , mpango ulioassisiwa na serikali ya CCM!
  Sisi tuliosoma sana miaka ya TANU na CCM tuasikitishwa sana kwa kijana kushindwa kabisa kujieleza.
  To make it worse, inaelekea "msomi" huyu ni kijana wa chuo kikuu-kwa reference yake.Reference ambayo haina direct relevance na alichoandika.
  Tatizo ni lako kijana
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Endelea kijana, wasikukatishe tamaa, hao ni magamba tu. wako selfish sana, hwanauzalendo kabisa (2015)
   
 4. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Kuwa makini unapomrekebisha mtu tafadhali
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  aisee umeandika vizuri sana wao wabunge wa sisiemu wanafanya kwa maslahi ya chama chao na si kwa masilahi ya wananchi
   
 6. n

  nitasemaukweli Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe kuna walimu wa shule za vidudu humu JF. Umeelewa kila kitu na wazazi wako ndio tatizo na kikwete si alisoma chuo mbona wanamaliza Taifa letu. Umaskini wa mawazo ni ndio chanzo cha kutuletea 'richmond na dowans' angalia hizo posho zilivyowasomesha na kununua hayo magari, hio ni shule sio.

   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mhhhhhh Bora mleta mada na grammatical error zake but sematicaly nimeemuelewa. Wewe na maelezo yako mazuri ni kama wabunge wa CCM anaowasema mleta hoja. Maneno matamuau kisomo kiferu but hawafanyi lolote...... Si unajua hata A .Chenge ni Havard graduate. kwake presentation na sheria haijawaisaidia watanzania

  Naona na wewe siiku za karibuni michango yako inakosa substance. mpaka unaanza kungalia sarufi. MAy be unahitaji kupekua pekua vitabu.

  Eti mliosoma miaka ya TANU.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wabunge wa CCM hawapo kwa ajili ya wananchi, wapo kwa ajili ya chama chao cha Magamba. Wa TZ tunaumia bure na huu mzigo wa watu wanaotumia kodi zetu bure bila ya huruma yeyote hawatutetei hata kidogo
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  toa boriti kwenye jicho lako kwanza
   
 10. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa ni ccm kwanza nchi baadae
   
 11. n

  nitasemaukweli Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Chadema again excellent respond to kikwete's budget. Wananchi wanaopenda nchi yao utawajua kwa matunda yao sio, let's see Mkullo if you can top that.

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Bajeti ya upinzani yalitikisa Bunge
  • MASHANGINGI YOTE KUUZWA

  na Martin Malera, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  KAMBI ya Upinzani Bungeni, imesoma bajeti mbadala ambayo imefuta ada za shule, misamaha mikubwa ya kodi, mfumo wa kulipana posho za vikao (sitting allowances) kwa watumishi wa umma na kulipa pensheni kwa wazee wote nchini.
  Eneo jingine iliyoligusa ni kutaka kuyauza magari yote ya kifahari (mashangingi) na serikali ianzishe utaratibu wa kukopesha magari ya kawaida kwa mawaziri na watendaji wote serikalini.
  Bajeti hiyo pia imependekeza kupunguzwa kodi watozwayo wafanyakazi wote nchini na tatizo la umeme litangazwe kuwa janga la kitaifa.
  Akisoma bajeti mbadala ya kambi ya upinzani jana bungeni, Waziri Kivuli wa Uchumi na Fedha, Zitto Kabwe, alipendekeza kufuta kodi zote za uanzishaji wa biashara ndogondogo ili kuchochea ujasiriamali nchini.
  Akifafanua mpango wa ulipaji posho za wabunge na watumishi wote nchini, Zitto alisema kambi ya upinzani inapendekeza mfumo mzima wa kulipana posho za vikao (sitting allowances) uondoke katika utumishi wa umma.
  "Ninaomba ieleweke kuwa hatupingi posho za kujikimu ambazo viongozi au maofisa wa umma hulipwa wanaposafiri nje ya vituo vyao vya kazi.
  "Posho hizi zirekebishwe kuendana na gharama za maisha za sasa. Lakini posho za vikao zifutwe mara moja," alisema Zitto.
  Mbunge huyo ambaye kwa takriban wiki moja sasa amejikuta kwenye mzozo na Spika wa Bunge, Anne Makinda na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuhusu posho za wabunge, alisema wabunge wanapaswa kuwa mfano wa kufyeka posho zao.
  "Waheshimiwa wabunge, iwapo sisi tukiendelea kujilipa posho za kukaa humu ndani na kwenye kamati zetu, tunakuwa tunatoa ruhusa kwa watumishi wa serikali kulipana posho hizi na hatutakuwa na mamlaka ya kuwahoji na kuwawajibisha," alisema Zitto na kushangiliwa na wabunge wa upinzani.
  Huku akitibua nyongo za wabunge wa CCM, Zitto alisema mfumo wa posho za vikao ni rushwa ya kitaasisi wanayojipa watu wenye mamlaka.
  Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema wakati kiongozi wa umma anapolipwa posho kwa kikao cha kufanya maamuzi yanayohusiana na majukumu yake ya kazi ambayo analipwa mshahara, polisi halipwi posho kwa kulinda, mwalimu halipwi posho kwa kuingia darasani wala muuguzi halipwi posho kwa kusafisha vidonda vya wagonjwa.
  "Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inashauri kufanya marejeo ya mfumo wa posho na mfumo wa mishahara kwa watumishi wa umma. Suala hili ni lazima tulianze sasa na katika bajeti hii tunayoijadili.
  "Lazima tuwaonyeshe Watanzania kuwa tunajali hali zao ili kurejesha imani ya umma kwa wanasiasa na viongozi wao," alisema.
  Zitto, alirejea hotuba ya bajeti ya Waziri Mkulo wakati akiahidi kupunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kudhibiti matumizi, lakini alisema bajeti ya serikali ya mwaka huu wa fedha imetenga sh trilioni 0.987, sawa na asilimia 13 % ya matumizi ya kawaida ya serikali na asilimia 6% ya bajeti yote kwa ajili ya kulipa posho.
  "Kambi ya Upinzani inahoji, je, waziri atapunguza posho zipi na kwa kiasi gani wakati tayari ametenga kiasi cha sh trilioni 0.987 kwa ajili ya posho?" alihoji.
  Dondoo za Bajeti Mbadala
  Zitto aliahidi kuongeza mapato hadi kufikia sh trilioni 14.160 kutoka trilioni 13.525 za serikali.
  "Tumeongeza mapato ya ndani hadi sh trilioni 8.68 kutoka sh trilioni 6.7 za serikali, tumeondoa kukopa mikopo ya kibiashara, hii inatokana na ukweli kwamba kufanya hivyo ni kuliongezea taifa gharama za kulipa madeni yenye riba kubwa na pia hili linafanya uchumi kuathirika, kwani serikali inakuwa ikishindana na sekta binafsi katika kuchukua mikopo kwenye taasisi za fedha, hivyo kuathiri uchumi," alisema.
  Zitto aliendelea kusema kuwa wameondoa posho mbalimbali ambazo ni sh trilioni 0.987 na kuzipeleka kwenye kuboresha mishahara ya watumishi wa umma na katika bajeti ya maendeleo.
  Nyingine ni kupunguza matumizi ya kawaida ya serikali kutoka sh trilioni 8.6 na kuwa 7.9.
  Alisema pia kuwa Kambi ya Upinzani inapendekeza kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya umeme na gesi ili kumaliza kabisa tatizo la nishati ya umeme na kuchochea matumizi ya gesi majumbani.
  "Pia tutakusanya mapato ya ndani kwa 22.84% ya Pato la Taifa ukilinganisha na serikali ambayo watakusanya 17%, tumepunguza misaada na mikopo kutoka nje na kuwa 27.54 % ya bajeti wakati ya serikali ni 29%.," alisema.
  Kwa mujibu wa Zitto, Kambi ya Upinzani imetoa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaongeza sh trilioni 1.905.
  Alitaja muhtasari wa vyanzo vipya vya mapato na kiasi kitakachoingizwa kuwa ni pamoja kodi ya misitu sh bilioni 100.
  Chanzo kingine ni kurekebisha misamaha ya kodi (sh bilioni 658), mauzo ya hisa za serikali (sh bil. 550), kurekebisha kodi sekta ya madini (sh bil. 240), kuimarisha usimamizi wa mapato ya wanyamapori (sh bil. 81), kuondoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwa kampuni za madini (sh bil. 59).
  Kwa mujibu wa Zitto, chanzo kingine cha mapato kitatokana na usimamizi wa mapato katika utalii (sh bil. 68) na kuimarika kwa biashara na EAC (sh bil. 150). Vyanzo hivyo vyote vitaingiza sh bil. 1905.
  Alisisitiza kuwa vyanzo hivyo ni vipya na ambavyo havikusanywi na serikali na kupanua wigo wa kodi.
  Pia alipendekeza kurekebisha sheria za kuzuia ukwepaji wa kodi (anti tax avoidance measures) na kuboresha mfumo wa kodi.
  Alisema Kambi ya Upinzani wamependekeza kurahisisha mfumo wa Kodi ya Mapato (Personal Income Tax) na kwamba sasa kila Mtanzania ajaze fomu za kodi (tax returns) kwa mujibu wa sheria hata kama hana kipato.
  Alitoa mfano wa watu wenye nyumba za kupangisha mijini, alisema wanapata fedha nyingi na wengine hutoza kodi ya pango kwa kutumia dola za Marekani lakini hawalipi kodi ya mapato.
  "Kambi ya Upinzani inapendekeza kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority na kwamba kila mwenye nyumba ya kupangisha lazima atambuliwe na kulipa kodi inavyostahili," alisema.
  Misamaha ya kodi
  Kuhusu kiwango cha kodi, Zitto alisema misamaha ya kodi inayotolewa Tanzania ni kikubwa mno.
  "Hii inaonekana wazi kwa kulinganisha kiwango cha misamaha ya kodi kinachotolewa Tanzania na kile kinachotolewa katika nchi za Uganda na Kenya.
  Nchini Tanzania kati ya miaka ya 2005/06 na 2007/08 misamaha ya kodi ilikadiriwa kuwa wastani wa asilimia 3.9 ya Pato la Taifa. Mwaka 2008/09 misamaha ya kodi ilikuwa asilimia 2.8 ya Pato la Taifa na mwaka 2009/10 asilimia 2.3.
  Ukilinganisha na Kenya na Uganda misamaha ilifikia asilimia 1 na 0.4 ya Pato la Taifa la kila nchi husika kwa mtiririko huo," alisema.
  Alisema kama Tanzania ingerekebisha viwango vya misamaha ya kodi ili kulingana na kiwango kilichofikiwa na Kenya, zaidi ya sh bilioni 600 zingeokolewa kwa mwaka 2007/08 peke yake.
  Kwa mujibu wa Zitto, ukubwa wa kiwango cha misamaha inayotolewa nchini unaweza kuelezewa kwa kukilinganisha na malengo ya ukusanyaji wa mapato ya kodi ambayo Tanzania inashindwa kuyafikia.
  Mfano katika mwaka 2008/09 na 2009/10, Zitto, alisema serikali haikutimiza lengo lake la mapato kwa wastani wa sh bilioni 453 kila mwaka.
  Alisema katika kipindi hicho hicho, misamaha ya kodi iliyotolewa ilifikia wastani wa sh bilioni 724 kwa mwaka Juni 2011, msamaha wa kodi unakadiriwa kuwa sh bilioni 930.
  Umeme janga la taifa
  Katika hotuba hiyo ya Bajeti Mbadala, kambi ya upinzani imependekeza tatizo la umeme litangazwe kuwa janga la kitaifa.
  Zitto alisema katika moja ya vipaumbele vya serikali mwaka huu Waziri Mkulo alitaja umeme.
  Alisema Waziri Mkulo, alipendekeza kumaliza tatizo la umeme na kwamba ametenga sh bilioni 537 kwa ajili hiyo.
  Hata hivyo alisema upembuzi uliofanywa na Kambi ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti vilivyotolewa na serikali, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa sh bilioni 402.4.
  Alisema fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi ya kawaida sh bilioni 76.95 na kwa upande wa Bajeti ya Maendeleo zimetengwa sh bilioni 325.4.
  Kwa mujibu wa Zitto, sh bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160 MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza.
  Alisema hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti hii.
  "Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo ya mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano, katika uzalishaji umeme ambapo kama taifa tumepanga kuzalisha megawati 1788 za ziada kutoka MW 1034 (installed capacity) zilizopo sasa, tunahitaji kuzalisha wastani wa MW 358 kila mwaka kwa miaka mitano.
  Hivyo basi, ukiondoa mradi wa MW 160 ambao tayari umeanza na umetengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu, tunahitaji mradi mwingine wa angalau MW 200 ndani ya mwaka huu wa fedha. Mradi ambao unaweza ukatekelezwa kwa haraka ni mradi wa Kiwira awamu ya kwanza MW 200," alisema.
  Alisema miradi iliyosalia ya Mchuchuma na Ngaka (makaa ya mawe), Mtwara - Somanga Fungu na Kinyerezi ( gesi asilia) na Ruhudji (maji), ielekezwe kwa taasisi zilizoainishwa kwa ajili ya utekelezaji na serikali kuingia makubaliano na taasisi hizo ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati.
  "Mheshimiwa Spika, madhara ya ukosefu wa umeme kwenye uchumi wa taifa ni makubwa sana. Mamlaka ya Mapato Tanzania ilinukuliwa ikisema kuwa mgawo wa umeme uliotokea mwanzoni mwa mwaka huu unaweza kuikosesha mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 840.
  Tumeona juhudi za Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la umeme lakini juhudi hizi hazionekani upande wa serikali na hasa Wizara ya Nishati na Madini.
  "Mheshimiwa Spika, imefikia wakati sasa kutangaza kuwa umeme ni janga la taifa na kwamba Bunge lipitishe azimio la uzalishaji wa umeme kwa viwango vya mpango wa maendeleo na kuweka adhabu ya kumfukuza kazi waziri iwapo miradi hiyo haitakuwa imekamilika kila mwaka," alisema Zitto.
  Pamoja na kukosoa, Zitto alimpongeza Waziri Mkulo, kwa kusikiliza na kuyaingiza kwenye bajeti ya serikali baadhi ya mapendekezo yao.
  "Ninachukua fursa hii kumpongeza waziri mwenzangu kwa kusikiliza maoni yetu kwenye baadhi ya mambo hayo na hivyo kuonyesha kwa umma moja ya faida ya mfumo wa vyama vingi.
  " Tunatarajia kuwa serikali itaendelea kusikiliza maoni yetu na kuyafanyia kazi. Changamoto hii na kwa uzito ule ule pia ipo kwetu sisi wa Kambi ya Upinzani kusikiliza pia maoni ya serikali.
  "Ni kwa namna hii ndiyo tutajenga taifa la watu walio huru, lenye demokrasia, usawa na haki, na lenye kutoa fursa kwa wananchi wake," alisema.
  Akitangaza sura ya Bajeti Mbadala kwa mwaka huu wa fedha, Zitto alisema mapato ya ndani (sh trilioni 8.681), mapato ya halmashauri (sh trilioni 3.51), mikopo na misaada kutoka nje (sh trilioni 3.924), mikopo ya ndani (sh trilioni 1.204) jumla mapato yote ni sh trilioni 14,160.
  Kwa upande wa matumizi, Zitto alisema matumizi ya kawaida ni sh trilioni 7.913 wakati matumizi ya maendeleo ni sh trilioni 6.247.
  Zitto alimalizia kwa kusema: "Kila mtu akitimiza wajibu wake, tunaweza. Tukiacha kuwa taifa la walalamikaji, tunaweza. Tukiendeleza umoja wa kitaifa, mshikamano na kulinda haki za raia, tunaweza. Ninaamini, tunaweza!"

  Bajeti ya upinzani yalitikisa Bunge

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 12. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Sio wote wana tatizo hili na kwa wale walio namna hiyo, kinachochangia selfishness and incompetency on their part ni kwamba wapo more ona defensive mode, kwahiyo wabunge wa opposition ambao wapo on the offensive mode ndio wanaonekana kuwa contrary to them. Upinzani ukija jaaliwa kuchukua uongozi wa nchi itafikia hatua kama hiyo ambapo wananchi watakuja taka mabadiliko na hivyo baadhi ya wabunge ambao sasa watakuwa ni wa chama tawala wataanza kuonekana selfish and incompetent. Otherwise sidhani kama kuna tofauti kati ya ole sendeka, mwakyembe, selelii, kilango na wabunge wa upinzani wanaoibua hoja nzito za kuichangamsha serikali. Being selfish and incompentent ni mbunge-specific, not party - specific.
   
 13. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi sina tatizo na lugha yako maana ni lugha ya kigeni kwahiyo hata ujasiri wa kuandika hapa unastahili hongera. Weakness kubwa saana kwenye point yako ni generalisation. Ukitazama kwa ujumla, pale kuna watu wapo vizuri saana sasa kuna tatizo la mtu, chama na mfumo. Kuna watu wameoza CCM na CDM pia. CCM inamatatizo na inafahamika. Lakini mfumo nao upo ICU. Labda nikutolee mfano, pale Bungeni ukihama chama tu umepoteza nafasi yako ya ubunge. Haya ni matatizo. Lakini kuna kina Magufuli, Mwakyembe, Sitta nk hawa ni bora saana huwezi kulinganisha na wengi CDM. Wao yapo wanayoamini ambao kwao tafsiri ya ubinafsi, kutojiweza, kutojiamini na wasiwasi si sahihi.
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Point noted!
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu naona unataka wale wanaotaka "zidumu fikra za Mbowe" ndio uatelewa?
  It takes two to tango ,sema substance isiyo na mantiki na bado nitakuelewesha my point of view.
  Usipende kuamini tu in the sense of mob psychology,toa facts and logical arguments.
  Zidumu fikra iliisha na wenyewe.
  And mind you presentation and clarity is something for thinkers to ponder, sio kariakoo hapa as someone said.
   
Loading...