• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

CCM Mororgoro yahoji fedha ya mradi iliyoliwa, yaahidi kuwachukulia hatua kali wahusika.

T

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Messages
579
Points
225
T

the horse

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2011
579 225
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimewajia juu watendaji wanaotuhumiwa kufuja sh. milioni 11 katika halamshauri ya wilaya ya Kilosa na kusisitiza kwamba ni lazima hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

fedha hizo zinadaiwa kulipwa kwa mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga eneo la mnada wa mifugo la Dumila, wilayani humo, ambaye ametoweka kabla ya kukamilisha kazi hiyo.

Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana alipotembelea eneo la ujenzi wa mnada huo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kufuatilia kero za wananchi wilayani humo.

Alisema kuwa upotevu wa fedha hizo ulitokana na Uzembe na usimamizi mbovu wa mradi huo na kwamba CCM kamwe haitawafumbia macho watendaji waliohusika kwani hawakitakii mema Chama.

Diwani wa Kata ya Dumila Josephat Kasanga alisema kuwa Serikali ya Kijiji cha Dumila ilikataa kutoa fedha hizo ambazo zilikuwa za awamu ya pili baada ya kutoridhishwa na kazi ya awamu ya kwanza iliyogharimu shilingi milioni 8 ambapo iliishia katika kiwango cha msingi.
 

Forum statistics

Threads 1,402,920
Members 531,016
Posts 34,409,542
Top