CCM Morogoro yawatimua vigogo 9

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu
Morogoro

~Uamuzi wake watoa somo kwa upinzani

Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa Morogoro kimesema tofauti iliopo kati ya upinzani na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sera, utekelezaji majukumu ya kijamii, uaminifu katika kulinda rasilimali za nchi kwa muktadha wa kujenga Taifa linalojitegemea na kuwa na nguvu za kiuchumi.

Kimesisitiza wakati Rais Dk John Magufuli akipigania mageuzi ya mfumo, utendaji na ufanisi kuelekea uchumi wa viwanda na uchumi wa kati upinzani umekuwa ukieneza propaganda chafu ili serikali ya Chama cha Mapinduzi isiweze kutimiza matakwa ya kisera, kisheria na kikatiba.

Hayo yameelezwa jana Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa huo ambacho kimewavua uongozi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ulanga Furaha F. Lilogeri makamu Mwenyekiti Amina Seif na wajumbe saba wa kamati ya mipango na Fedha wa Halmashauri hiyo.

Shaka alisema wakati serikali ya awamu ya tano ikiweka mkazo na bidii kwa kujenga nchi, kukwepa mikingamo ya siasa chafu inayokwamisha maendeleo, kupambana na rushwa, dhulma na ubadhirifu wa mali za umma hivyo Halmashauri kuu ya mkoa Morogoro imejiridhisha kuwa viongozi waliovuliwa Uongozi wameshindwa kusimamia dhamana waliyopewa na wananchi na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla katika kusimamia majukumu yao na kukiuka maadili ya uongozi kwa kutumia vibaya dhamna waliyokabidhiwa na wananchi kwa niaba ya wananchi.

Amefahamisha kuwa mahali iliipo nchi hivi sasa mtu anayetumia akili kupima utendaji hatasita kuitaja miaka minne ya Rais Dk Magufuli imefanya mabadiliko makubwa kupata mafanikio na maboresho ya kujivunia hivyo CCM Morogoro haiko tayari kuona juhudi izo zinavizwa kwa njia moja ama ingine.

"CCM Morogoro tumemuelewa Rais Magufuli anachotaka, tumeamua kusafisha nyumba yetu lazima tuoneshe tofauti za kifikra, kimtazamo na tafsiri hasi inayotolewa na upinzani. Wakati serikali ikisimamia sera na sheria. Upinzani unapiga kelele zisio na tija. CCM hakitegemei propaganda mfu. Upinzani umeamua kueneza uongo na fitna dhidi ya Rais Magufuli na serikali anayoingoza wakati CCM inaendelea kutimiza azma na dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi" Alisema shaka

Alisema ikiwa upinzani unakataa kuunga mkono juhudi zilizopo kwa kuona hofu wakidhani wakisifu watafilisika kisiasa, waendelee kuwategemea mawakili wa propaganda na kudhani Serikali ya CCM itasalim amri au itafuata mawazo yao batili huku wakiendelea kuwa na viongozi masultani wanaolea wizi na ubadhirifu wa ruzuku na michango ya wanachama wao.

"Kuna unyang'au wa kisiasa unafanyika nchini Upinzani usipoheshimu utaifa na uzalendo tutabaki omba omba daima. Tutapuuzwa kwa kushindwa kutumia rasilimali na mali asili zetu, haiwezekani Halmashauri zinapotea billioni kadhaa alafu viongozi tunachekeana na kuleana huku wananchi wakisulubika, CCM imethubutu kuvunja mfupa mgumu kwa meno, CHADEMA nao wanaoviongozi Halmashauri ya Ulanga watanzania waone sasa tofauti yetu" Alisema Shaka.

Hata hivyo Shaka aliwataka wananchi Mkoani Morogoro kutoyumbishwa na propaganda, dhihaka au porojo za wapinzani badala yake viongozi wa serikali za CCM wa ngazi zote wasimamie utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 na kwa yoyote atakaekwenda kinyume na miiko na maadili ya uongozi hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni na Katiba ya CCM.

Mapema mwezi Septemba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara katika mkoa wa Morogoro na kubaini ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga aliondolewa na kuagiza Watumishi wote waliohusika wachukuliwe hatua za kinidhamu ambapo CCM ilimuahidi waziri mkuu kuwa haitasita kuchukua hatua kwa viongozi wake waliohusika.

"Mhe, Waziri Mkuu wakati ukikagua na kuona hali halisi, nilikuona umebadilika mpaka sura, hiki tulichokishuhudia ni uhuni na uharamia nikuhakikishie serikali mnachukua hatua na CCM tunakwenda kufanya tathmini ya kina kila aliyehusika Chama kitashughulika nae" Alisema Shaka

Hatimae yametimia kwa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro kuchukua hatua.

#T2020CCM #T2020JPM #TusikubaliKugawanyika

IMG-20191208-WA0017.jpeg


IMG_20191115_151826.jpeg
 
December 3, 2019

CCM wameingia woga kuhusu umaarufu wa CHADEMA kuelekea 2020 wilaya za Kilombero, Mikumi, Mlimba na Ifakara mkoani Morogoro, Tanzania

Mgombea wa CCM ubunge mwaka 2015 Abubakar Assenga anakumbuka machungu ya kushindwa ubunge Morogoro.

Abubakar Assenga, anaelezea pamoja na kutumia jina la Mgombea wa U-Rais 2015 kupitia CCM aliyekuwa waziri wa Ujenzi kutoa ahadi ya daraja la Kilombero, barabara ya Kidatu wilayani Ifakara, Bwawa la Umeme la Stiegler's Gorge mwaka 2015 lakini wananchi walichagua wabunge watatu wa CHADEMA Mkoani Morogoro.

Nini siri ya wananchi kuiamini CHADEMA na hivyo kupelekea majimbo matatu kwenda upinzani mkoani Morogoro .

 
Mwaka 2019
Morogoro, Tanzania

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro aelezea ugumu wa kugomboa majimbo ya Kilombero, Ifakara, Mlimba na Mikumi toka CHADEMA yote ya mkoani Morogoro. Atoa hali halisi jinsi CCM ilivyo katika hali ya unyonge mkubwa na kushindwa kuamsha ushawishi wa kisiasa kwa majimbo waliyopoteza kura 2015 na kushindwa kupata wabunge kwa tiketi ya chama kongwe CCM :
 
July 29, 2016
Tujikumbushe Hoi Hoi, Nderemo, vifijo na shangwe za wananchi Mlimba na Kilombero , Morogoro



Kesi Za CCM Kupinga Ubunge Morogoro Zatupiliwa Mbali

Mahakama kuu ya Tanzania iliyokaa Kilombero mkoani Morogoro imetupilia mbali kesi mbili ziizowasilishwa na CCM za kupinga matokeo ya ushindi ya wabunge wa CHADEMA katika majimbo ya Mlimba na Kilombero mkoani Morogoro mwaka 2015

 
Masaibu ya wananchi wa Mlimba kutoka serikali ya CCM

Mbunge wa Mlimba, Mkoani Morogoro Mh. Susan Kiwanga (CHADEMA) alikuwa mmoja wa wabunge waliosimama Bungeni leo April 19, 2017 ili kuchangia bajeti ya Wizara ya TAMISEMI na ile ya Ofisi ya Rais na utawala bora ambapo kati ya vitu alivyozungumzia ni hatua ya serikali kushindwa kushughulikia baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo

 
"Serikali Hii ni HATARI, Pesa Hamna Nyinyi, Hali Mbaya"' - KIWANGA

Mbunge wa jimbo la Mlimba (CHADEMA) Suzan Kiwanga, akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.

 
Unajipigia gitaa na unacheza mwenyewe chadema ndio mfano wa kuigwa imekua ikichukua hatua bila kumuonea haya mtu nyie igeni tu kwa chadema kumbuka ya arusha madiwani 5 kule MWANZA alikuwepo Diwani wakuitwa Adam chagulani nk. Nakushauli usirudie tena kuleta urojo Hapa.
 
Back
Top Bottom