CCM Morogoro yawajengea uwezo viongozi wake

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Ndugu Shaka Hamdu Shaka leo Juni 17, 2019 amemuwakilisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Ndugu Innocent Kalogeris kufunga mafunzo elekezi ya siku tano ya kuwajengea uwezo viongozi wa CCM na jumuiya zake Wilaya ya Morogoro Mjini.

Mafunzo elekezi ya siku 5 yanalenga kuwajengea uwezo viongozi wa kata 29, matawi 92 na mabalozi 927 yameshirikisha watendaji wa Chama na jumuiya zake, wenyeviti wa Chama na jumuiya zake, makatibu wenezi wa kata na matawi pamoja na mabalozi wote wa Wilaya ya Morogoro Mjini.

Katika mafunzo hayo viongozi wote walikabidhiwa vitendea kazi ili kurahisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

#UmojaNiUshindi2019
#MorogoroYaKijaniInawezekana #TuwePamoja
#TusikubaliKugawanyika
IMG-20190617-WA0067.jpeg
IMG-20190617-WA0078.jpeg
IMG-20190617-WA0070.jpeg
IMG-20190617-WA0079.jpeg
IMG-20190617-WA0072.jpeg
IMG-20190617-WA0076.jpeg
IMG-20190617-WA0074.jpeg
IMG-20190617-WA0083.jpeg
 
Attachments

  • IMG-20190617-WA0071.jpeg
    IMG-20190617-WA0071.jpeg
    90.3 KB · Views: 11
ALIYOYASEMA KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGORO NDG SHAKA HAMDU SHAKA WAKATI AKIMUAKILISHA MWENYEKITI WA CCM MKOA MOROGORO NDG INNOCENT KALOGERIS KUFUNGA MAFUNZO ELEKEZI YA KUWAJENGEA UWEZO, VIONGOZI WA CCM NA JUMUIYA ZAKE MOROGORO MANISPAA JUNI 17, 2019.

"Viongozi wa CCM na jumuiya zake tunawagiza kuzibadilisha kero na changamoto za wananchi kuwa fursa na kuepuka kulalamika badala yake kila mmoja ajenge ujasiri wa kupata ufumbuzi wa kila changamoto katika eneo lake" Shaka

"Mtambue na kufahamu kila ofisi ya kiongozi dhamana CCM ni lazima iwe na mpango kazi kuanzia miezi mitatu, sita, mwaka hadi miaka mitatu na utekekezaji wake uende sambamba na ilani ya uchaguzi ya CCM" Shaka

"Viongozi wa CCM mjitambue kama mmebeba amana na dhamana ya kukitumikia chama hivyo hamna budi kuchemsha bongo na kuzikabili changamoto zote badala ya kuzikimbia, kulalamika au kutelekeza majukumu" Shaka

"Dhamana ya utawala iko mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi ili kushamirisha maendeleo ya kisekta hivyo pamoja na kazi ya chama ya kuingiza wanachama wapya, kukusanya ada, kulinda rasilimali na miradi, kila kiongozi wa halmashauri kuu na kamati za siasa ngazi zote z
ajue chama kitakavyoshinda" Shaka

"Siasa ni shughuli za makundi. Kila kiongozi mwenye dhamana, atambue wajibu wa kujichanganya na makundi ndani ya jamii. Mtaji wa ushindi wa CCM ni kura za wanachama na wananchi wa makundi mengine katika jamii. Kubaki ofisini na kukimbia watu si tafsiri halisi ya utendaji bora katika CCM" Shaka

"Viongozi wa dini wangejifungia kwenye nyumba za ibada kila wakati bila kwenda kutangaza maneno ya mungu kwa watu , wasingepata waumini wa kumtumikia mungu kwenye dini zao" Shaka

"Kuna kazi za Chama ndani Chama na nje ya chama ndani ya umma. Twendeni huko kila wakati na si kusubiri kudandia ziara za viongozi. Kiongozi wa CCM asiye na mpango kazi ofisini kwake akubali kuwajibika, kazi za utendaji ni mipango ya muda mfupi na mrefu si maneno matupu" Shaka

"Ninyi ndio wasimamizi namba moja wa ilani ya uchaguzi katika maeneo yenu, kila mtendaji na viongozi wa kisiasa muwe na majukumu ya kwenda kwenye Tarafa zote zilizomo kwenye wilaya zenu , huo ndiyo utendaji huku ngazi ya kata, matawi chama na jumuiya nanyi mfike kwenye vijiji, mitaa na vitongoji vyenu" Shaka

"Ikiwa wapo viongozi hawafanyi ziara, hafanyi vikao au kukutana na viongozi wenzake na wanachama kwenye ngazi husika anakihujumu chama kwani hakitendei haki na kukitumikia ipasavyo" Shaka

"Tunapopaisha sauti zetu tukisema tunamuunga mkono Rais Magufuli kila mmoja wetu asiishie maneno tufanye kwa vitendo nendeni mkasimamie ilani na kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM kwenye kata, mitaa vijiji na vitongoji" Shaka

Mafunzo elekezi ya siku 5 ya kuwajengea uwezo viongozi wa kata 29, matawi 92 na mabalozi 927 yameshirikisha pia watendaji wa Chama na jumuiya, wenyeviti wa Chama na jumuiya, makatibu waenezi wa kata na matawi pamoja na mabalozi wote wa Wilaya ya Morogoro Mjini
 
Wakuu wenzetu kauli ya chadema ni msingi waliianzisha miaka miwili iliyopita .Leo ndio tunakuja na hii baada ya habari za chadema msingi kusambaa kwa kasi.
Bado tupo nyuma sana tujitafakari kwa kweli mtanielewa vibaya lakini tujitafakari kwani miaka mitatu tulikuwa tunazomewa sio kama ndio hivi sijui mbadala ni nini.
Kwa nini hatushawishi watu kwa hoja tumeishia kusema sijui kuna wazalendo na wasio wazalendo ndani ya taifa moja tunaloliongoza sisi Ccm.
Sasa hawa wasiowazalendo tunafanya lipi kwa njia hoja ili waelewe kauli mbiu kwani kuwa na Raia wa aina mbili sio umoja aliouacha Mwasisi Mwalimu Nyerere
 
Hawa mashetani wanachoweza ni kuiba,kuua na kuharibu.
 
Back
Top Bottom