CCM mnaweza kufanya haya basi 2020 mtarudi madarakani

andrews

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
1,679
152
Nchi ya Kijamaa, iliyojiandaa barabara chini ya Chama, ina nguvu za Kimaendeleo. Wazembe, wavivu na wapinzani wa nguvu hizo, hupondwa-pondwa na kusagwa-sagwa wasionekane aateeni!”

Ndugu zangu,
Baadhi yetu tumepata kuyasikia hayo yakitamkwa redioni enzi za utoto wetu. Enzi zile za Chama kimoja na redio moja. Zilikuwa ni propaganda zilizoandamana na vitisho.

Nayo ni historia yetu, na bahati mbaya, propaganda hizo zimechangia kuifanya jamii yetu iwe kama ilivyo sasa. Mwaka 2012 bado mwenye fikra tofauti anaweza kupigwa muhuri wa ’ Mpinzani wa nguvu za kimaendeleo chini ya Chama na anatakiwa apondwe-pondwe na asagwe asagwe asionekane tena!’

Ndugu zangu,
Umri wangu umenipa bahati ya kuishi kushuhudia baadhi ya matukio makubwa katika nchi yetu. Sisi ndio wale wa ’ Kizazi Cha Azimio’.

Nilikuwa sijazaliwa, siku ile ya Julai saba,1954 wakati TANU ikianzishwa rasmi ikiwa na ofisi zake pale Mtaa Lumumba, Kariakoo. Lakini, nilikuwa na miaka 10 na nilishuhudia kwa macho yangu siku ile ya Jumamosi wakati CCM ikizaliwa. Ni Februari 5, 1977.

Nakumbuka nikiwa na watoto wanzangu tulikwenda pale ofisi za TANU Ilala Boma kushuhudia tukio lile la kihistoria. Nilichoshuhudia pale Ilala Boma ni ’Kuzaliwa Kwa Chama Kipya’. Niliziona nyuso nyingi za watu wazima zilizojaa matumaini ya siku zijazo, nasi kama watoto, ujio wa Chama kipya ulitujengea matumaini ya baadae.

Lakini, kadri miaka ilivyokwenda, na kwa kusaidiwa na elimu na uzoefu wa maisha, nimekuwa nikikiona chama kisichofanya mabadiliko ya kimsingi wakati nchi na jamii ikibadilika kwa kasi. Walau, katika Awamu hii ya JK, naweza kuona jitihada za makusudi za kujaribu kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho. Hili laweza kuwa jambo la kheri kwa CCM yenyewe na nchi pia.

Maana, katika siasa, si wapiga kura tu ndio wenye kuchagua, hata chama nacho kinachagua. Na chama cha siasa kina mambo mawili tu ya kuchagua; kubadilika ( kufuatana na wakati) au kufa. Na kwa wakati tulio nao, chama cha siasa hakiwezi kudumu kwa hila, ghilba na vitisho. Katika wakati tulio nao, Chama kinachotanguliza matatu hayo kinaonyesha dalili za chama kinachoelekea kaburini. Ndio, miaka ya uhai wake itakuwa inahesabika.

Kuhofiwa haipaswi kuwa sifa ya kiongozi au chama cha siasa. Na ni ukweli, leo kuna Watanzania wenye kukihofia zaidi Chama Cha Mapinduzi kuliko Mungu wanayemwamudu. Na lipi jema kwa kiongozi na chama; kuhofiwa au kupendwa? Mwingine angependa vyote, lakini haiwezekani. Jema ni kupendwa na kuheshimiwa.

CCM itambue sasa, kuwa, mabadiliko yanakuja hata Tanzania, ni suala la wakati tu. Na vijana wa Tanzania huenda wasiingie mitaani wakafanya kama wenzao wa Misri, Tunisia na Libya. Watasubiri siku ile ya kwenda kupiga kura ifikapo 2015. Hilo la subira ya vijana ndilo tunaloliombea.

Na huku mitaani tunawasikia vijana wengi wa Kitanzania wenye kuisubiri kwa hamu 2015. Yumkini wamedhamiria kuandamana kwa wingi wakiwa na vitambulisho vyao vya kupigia kura. Wataandamana kwenda vituo vya kupigia kura kwa nia ya kuiondoa CCMmadarakani kwa nguvu za kura.

Salama ya CCM?

Ni ukweli, kuwa CCM ina hali ngumu kuelekea 2015. Chama kimepoteza mvuto kwakundi kubwa la vijana. Anayesoma kwa makini alama za nyakati anaweza kuona, kuwaCCM ikiwa na bahati inaweza kwa tabu kutoa rais 2015, lakini, takribani nusu ya wabunge wa bunge lijalo watatoka kambi ya upinzani. Na kwa CCM inavyoenenda sasa, itakuwa miujiza kama rais wa 2020 atatoka CCM.

CCM ijiandae sasa kuwa chama cha upinzani. Na inaweza kubaki hai kwa muda mrefu kama itaipitisha nchi hii kwenye Katiba itakayoifanya Tanzania kuwa nchi ya kisasa zaidi. Yawepo mazingira ya uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Maana, kwa Katiba ya sasa, CCM ikitoka madarakani, basi, yaweza pia ikawa ndio mwisho wake, kuwa chama hicho kitakufa.

Nimepata kuandika, kuwa ili CCM isalimike na kubaki madarakani katika chaguzi zijazo, sio tu inahitaji kufanya mabadiliko makubwa, bali mabadiliko makubwa yenye kishindo.

CCM inahitaji kurudi kwenye misingi iliyoanzisha chama hicho. Huu ni wakati wa kurudisha misingi ya kimaadili ya chama na uongozi. Misingi iliyokuwapo huko nyuma. Angalia, iko wapi Miiko ya Uongozi? Imevunjwa, na ndio maana ufisadi umetamalaki.

Kwa MwanaCCM, sasa sio suala la kushinda uteuzi wa ndani ya Chama na kujihakikishia kuingia Ikulu au Bungeni, kuna umma unaotaka mabadiliko utakaomkabili mgombea wa CCM, awe mgombea Urais, Udiwani au Ubunge. Kuingia ulingoni na ‘CCM ile ile’ itakuwa ni hatari kwa wagombea wengi wa CCM siku zijazo.

Ni ukweli, kuwa ndani ya CCM imeanza kuporomoka, misingi iliyopelekea kuanzishwakwa Chama hicho tukianzia na vyama mama vya TANU na Afro- Shiraz. Hili ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, Vyama mama kwa CCM, TANU na Afro- Shiraz, vilikuwa ni kimbilio la makabwela, kimbilio la wanyonge.

Lakini, CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao. Wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi. Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!

.
Kuna wanaokimbilia ndani ya CCM kwa kuamini katika malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa chama hicho. Lakini, kuna wanaokimbilia ndani ya CCM wakiwa na malengo na madhumuni ya kwao binafsi yasiohusiana kabisa na ya CCM. Kwao wao,CCM ni sawa na daraja la miti la kuwasaidia kuvuka na kufika wanakotaka kwenda.

CCM ina nafasi ya kujisahihisha, kama kuna utashi wa kisiasa.
Maggid Mjengwa,
Sweden.
+46 736 966 032
 
[h=2]kikwete ni mnafiki no 1[/h]
Tangu tupate maraisi hatujawahi kuwa na rais mnafiki, mzembe,dhaifu na ndumila kuwili kama kikwete uendeshaji serikali yake umejaa fitina dhihaka na upuuzi mwingi anyemshabikia huyu naomba aweke haya maelezo kwa kuprint au kucopy na baa ya 2015 mtaona kwa nini tz imefika hapa ilipo ni sababu ya huyu mr dhaifu hakuna alichowahi kuongoza kikafanikiwa zaidi ya kutengeneza makundi ndani ya chama na nchini ili awe madarakani kirahisi mungu ibariki tanzania kwa haraka sana tuondokane na huyu mnafiki
 
Nchi ya Kijamaa, iliyojiandaa barabara chini ya Chama, ina nguvu za Kimaendeleo. Wazembe, wavivu na wapinzani wa nguvu hizo, hupondwa-pondwa na kusagwa-sagwa wasionekane aateeni!"

Ndugu zangu,
Baadhi yetu tumepata kuyasikia hayo yakitamkwa redioni enzi za utoto wetu. Enzi zile za Chama kimoja na redio moja. Zilikuwa ni propaganda zilizoandamana na vitisho.

Nayo ni historia yetu, na bahati mbaya, propaganda hizo zimechangia kuifanya jamii yetu iwe kama ilivyo sasa. Mwaka 2012 bado mwenye fikra tofauti anaweza kupigwa muhuri wa ' Mpinzani wa nguvu za kimaendeleo chini ya Chama na anatakiwa apondwe-pondwe na asagwe asagwe asionekane tena!'

Ndugu zangu,
Umri wangu umenipa bahati ya kuishi kushuhudia baadhi ya matukio makubwa katika nchi yetu. Sisi ndio wale wa ' Kizazi Cha Azimio'.

Nilikuwa sijazaliwa, siku ile ya Julai saba,1954 wakati TANU ikianzishwa rasmi ikiwa na ofisi zake pale Mtaa Lumumba, Kariakoo. Lakini, nilikuwa na miaka 10 na nilishuhudia kwa macho yangu siku ile ya Jumamosi wakati CCM ikizaliwa. Ni Februari 5, 1977.

Nakumbuka nikiwa na watoto wanzangu tulikwenda pale ofisi za TANU Ilala Boma kushuhudia tukio lile la kihistoria. Nilichoshuhudia pale Ilala Boma ni 'Kuzaliwa Kwa Chama Kipya'. Niliziona nyuso nyingi za watu wazima zilizojaa matumaini ya siku zijazo, nasi kama watoto, ujio wa Chama kipya ulitujengea matumaini ya baadae.

Lakini, kadri miaka ilivyokwenda, na kwa kusaidiwa na elimu na uzoefu wa maisha, nimekuwa nikikiona chama kisichofanya mabadiliko ya kimsingi wakati nchi na jamii ikibadilika kwa kasi. Walau, katika Awamu hii ya JK, naweza kuona jitihada za makusudi za kujaribu kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho. Hili laweza kuwa jambo la kheri kwa CCM yenyewe na nchi pia.

Maana, katika siasa, si wapiga kura tu ndio wenye kuchagua, hata chama nacho kinachagua. Na chama cha siasa kina mambo mawili tu ya kuchagua; kubadilika ( kufuatana na wakati) au kufa. Na kwa wakati tulio nao, chama cha siasa hakiwezi kudumu kwa hila, ghilba na vitisho. Katika wakati tulio nao, Chama kinachotanguliza matatu hayo kinaonyesha dalili za chama kinachoelekea kaburini. Ndio, miaka ya uhai wake itakuwa inahesabika.

Kuhofiwa haipaswi kuwa sifa ya kiongozi au chama cha siasa. Na ni ukweli, leo kuna Watanzania wenye kukihofia zaidi Chama Cha Mapinduzi kuliko Mungu wanayemwamudu. Na lipi jema kwa kiongozi na chama; kuhofiwa au kupendwa? Mwingine angependa vyote, lakini haiwezekani. Jema ni kupendwa na kuheshimiwa.

CCM itambue sasa, kuwa, mabadiliko yanakuja hata Tanzania, ni suala la wakati tu. Na vijana wa Tanzania huenda wasiingie mitaani wakafanya kama wenzao wa Misri, Tunisia na Libya. Watasubiri siku ile ya kwenda kupiga kura ifikapo 2015. Hilo la subira ya vijana ndilo tunaloliombea.

Na huku mitaani tunawasikia vijana wengi wa Kitanzania wenye kuisubiri kwa hamu 2015. Yumkini wamedhamiria kuandamana kwa wingi wakiwa na vitambulisho vyao vya kupigia kura. Wataandamana kwenda vituo vya kupigia kura kwa nia ya kuiondoa CCMmadarakani kwa nguvu za kura.

Salama ya CCM?

Ni ukweli, kuwa CCM ina hali ngumu kuelekea 2015. Chama kimepoteza mvuto kwakundi kubwa la vijana. Anayesoma kwa makini alama za nyakati anaweza kuona, kuwaCCM ikiwa na bahati inaweza kwa tabu kutoa rais 2015, lakini, takribani nusu ya wabunge wa bunge lijalo watatoka kambi ya upinzani. Na kwa CCM inavyoenenda sasa, itakuwa miujiza kama rais wa 2020 atatoka CCM.

CCM ijiandae sasa kuwa chama cha upinzani. Na inaweza kubaki hai kwa muda mrefu kama itaipitisha nchi hii kwenye Katiba itakayoifanya Tanzania kuwa nchi ya kisasa zaidi. Yawepo mazingira ya uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Maana, kwa Katiba ya sasa, CCM ikitoka madarakani, basi, yaweza pia ikawa ndio mwisho wake, kuwa chama hicho kitakufa.

Nimepata kuandika, kuwa ili CCM isalimike na kubaki madarakani katika chaguzi zijazo, sio tu inahitaji kufanya mabadiliko makubwa, bali mabadiliko makubwa yenye kishindo.

CCM inahitaji kurudi kwenye misingi iliyoanzisha chama hicho. Huu ni wakati wa kurudisha misingi ya kimaadili ya chama na uongozi. Misingi iliyokuwapo huko nyuma. Angalia, iko wapi Miiko ya Uongozi? Imevunjwa, na ndio maana ufisadi umetamalaki.

Kwa MwanaCCM, sasa sio suala la kushinda uteuzi wa ndani ya Chama na kujihakikishia kuingia Ikulu au Bungeni, kuna umma unaotaka mabadiliko utakaomkabili mgombea wa CCM, awe mgombea Urais, Udiwani au Ubunge. Kuingia ulingoni na ‘CCM ile ile' itakuwa ni hatari kwa wagombea wengi wa CCM siku zijazo.

Ni ukweli, kuwa ndani ya CCM imeanza kuporomoka, misingi iliyopelekea kuanzishwakwa Chama hicho tukianzia na vyama mama vya TANU na Afro- Shiraz. Hili ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, Vyama mama kwa CCM, TANU na Afro- Shiraz, vilikuwa ni kimbilio la makabwela, kimbilio la wanyonge.

Lakini, CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao. Wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi. Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!

.
Kuna wanaokimbilia ndani ya CCM kwa kuamini katika malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa chama hicho. Lakini, kuna wanaokimbilia ndani ya CCM wakiwa na malengo na madhumuni ya kwao binafsi yasiohusiana kabisa na ya CCM. Kwao wao,CCM ni sawa na daraja la miti la kuwasaidia kuvuka na kufika wanakotaka kwenda.

CCM ina nafasi ya kujisahihisha, kama kuna utashi wa kisiasa.
Maggid Mjengwa,
Sweden.
+46 736 966 032

Mbona Umesahau kusema kuna GAP kubwa kati ya Walio Nacho na Wasio Nacho?

Na Hiyo GAP kubwa imeanzia Ndani ya CHAMA kitukufu cha CCM wengi ya Viongozi ndani ya CCM hawafuati

Nguzo za Chama Cha Mapinduzi Angalau zile za Marekebisho za AZIMIO LA ZANZIBAR.

- Kuna baadhi ya Viongozi wa CCM au Wastaafu wa CCM wana fedha nje ya NCHI kwenye BENKI USWISI

Hauoni itakuwa bora kama watakuja na kusema Ukweli walipataje hizo PESA?

- Yeah labda 2020 hizo 10% za Madini watakuwa wameziachia? kama kweli watashindwa uchaguzi 2015

- CCM sio tena Chama Cha Kijamaa, kama wanasema hivyo ni kuwadanganya Wananchi CCM ni Chama cha Wachache

Mabeberu, Wanaona ni Bora kuuza Ardhi kwa Capitalist America na Madini kwa Communist CHINA; Wote wanajua

jinsi ya kumu-exploit Mwafrika as a Cheap Labor; Migogoro ya Capitalist Owning Land in Rukwa Matatizo yameshaanza

Kwa wananchi; na Pia Huko Huko Rukwa Wachina Wanawatumikisha Waafrika na kutowalipa pesa zinazotakiwa

- Rukwa - Mkuu wa Mkoa ni Kipenzi cha CCM; Eng. Manyanya aliyefananisha Dr. Ulimboka na madai yao na Hitler

Lakini ana Matatizo ya U-Capitalist na U-Communist exploiting local Africans hasemi chochote.

- CCM Sidhani kama IKIANGUKA itajikusanya na kurudi--- INANIKUMBUSHA YA KANU...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom