CCM mnaomtetea SABAYA oneni aibu, tazameni rafu za tuhuma za Rushwa kati ya MNYETI na OLE MILLYA.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
CCM kutetea wala rushwa wanyang'anyi mjaanza leo, kuna watu mmetokwa mapovu kuhusu Ole Sabaya kudai rushwa kwa nguvu kwa mfanyabiashara wa hoteli Kilimanjaro, hamna hata haya mnafunika madhambi msoyajua kutetea Rushwa? CCM gani hii? Bora JK alikua akisikia mambo haya anaagiza uchunguzi haraka na anachukua hatua.

Kwasababu ya ubishi usiokua na tija kwa taifa, Sasa tazameni ya mbunge wa Simanjiro(CCM)James Ole Millya anavyomtuhumu mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kupokea Rushwa kwa Mwekezaji wa mgodi wa Tanzanite1-Mererani, Mnyeti naye anadai kua anao ushahidi wa James Ole Millya kutishia watu Bastola ili apewe Rushwa kwa nguvu. Hivi hii ni kweli awamu ya 5 inayojipsmbanua kupinga rushwa au ni utawala wa aina gani huu? Hii aibu ya viongozi wakubwa makada wa CCM kutuhumiana rushwa mbele ya wananchi bila huruma mchana kweupe,mtawaambia nini wananchi? Hii aibu mnaificha wapi?

Hivi hawa kina Dr Bashir Ally wanaozunguka nchi nzima kuwaambia wananchi kua awamu ya 5 imejipambanua kwa kukomesha vitendo vya rushwa hamuogopi Mungu? Haya malumbano ya Rushwa dhidi ya viongozi wakubwa kabisa makada wa CCM hamuoni kua yanawavua nguo mchana kweupe? Mnawadanganyia nini wananchi? Mteteeni Sabaya kwa kisingizio kua ni propaganda za kisiasa za Mbowe dhidi yake ili aondolewe Hai lakini Mungu hua sio wa kukebehiws.
 
Upuuzi mtupu, leta evidence ndo tunayongojea, kwa hizo mambo za CCTV cameras zinazidi kumpaisha kwa kuonesha ni jinsi gani jamaa ni mchapa kazi, halali anapambana.
 
Kwa haya yote yanayotokea sasa, naweza kusema serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete ilikuwa serikali sikivu kwelikweli.

Awamu hii ni mwendo wa kuchukua hatua pale nitakapojisikia na kupendezwa mimi, sipangiwi!
 
JK alikua akisikia malalamiko anafanya uchunguzi na kuchukua hatua za haraka, Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpenzi. Enzi za JK wananchi wakikulalamikia huna kazi
 
Usishangae siku bwana mkubwa akimpiga chini(baada ya kusoma upepo),ni CCM hawa hawa watakuwa wa kwanza kumpongeza.
 
Upuuzi mtupu, leta evidence ndo tunayongojea, kwa hizo mambo za CCTV cameras zinazidi kumpaisha kwa kuonesha ni jinsi gani jamaa ni mchapa kazi, halali anapambana.
Kiongozi wa Umma anapotuhumiwa waziwazi vile bila kificho anapoteza uhalali wa kuendelea kukalia kiti. Ni ama ajiuzulu kupisha uchunguzi au asimamishwa kazi na mamlaka mpaka uchunguzi ukamilike. Uchunguzi ukionyesha tuhuma sio za kweli anaweza kurudi pale au akapanda zaidi.

Sidhani kama yule mfanyabiashara ni kichaa hadi aweze kumzushia kiongozi wa serikali tuhuma nzito kama zile.
 
JK alikua akisikia malalamiko anafanya uchunguzi na kuchukua hatua za haraka, Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpenzi. Enzi za JK wananchi wakikulalamikia huna kazi
Kuna wanaotaka kutuaminisha hii ni serikali sikivu kuliko ile ya awamu ya nne. Hapana, hii ni serikali sikivu ndio, ila ni kwa yale inayopenda kusikia.
 
Nazani hao ma RC na DC wapo kwenye operation maalimu ya kukusanya hela ya uchaguzi za ccm, zamani walikuwa na utaratibu wa kuwandikia barua ya michango uchaguzi unapokaribia, sasa kwa vile inaonekana makampuni hawataki kutoa, imebidi waje na mbinu mbadala.
 
mwacheni mkuu wa wilaya apige kazi hizo nituhuma ambazo hazina ukweli wowote uli ni njama za wapinzn wakiongozw na mbowe kumkwamisha mkuu wawilaya
 
CCM kutetea wala rushwa wanyang'anyi mjaanza leo, kuna watu mmetokwa mapovu kuhusu Ole Sabaya kudai rushwa kwa nguvu kwa mfanyabiashara wa hoteli Kilimanjaro, hamna hata haya mnafunika madhambi msoyajua kutetea Rushwa? CCM gani hii? Bora JK alikua akisikia mambo haya anaagiza uchunguzi haraka na anachukua hatua.

Kwasababu ya ubishi usiokua na tija kwa taifa, Sasa tazameni ya mbunge wa Simanjiro(CCM)James Ole Millya anavyomtuhumu mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kupokea Rushwa kwa Mwekezaji wa mgodi wa Tanzanite1-Mererani, Mnyeti naye anadai kua anao ushahidi wa James Ole Millya kutishia watu Bastola ili apewe Rushwa kwa nguvu. Hivi hii ni kweli awamu ya 5 inayojipsmbanua kupinga rushwa au ni utawala wa aina gani huu? Hii aibu ya viongozi wakubwa makada wa CCM kutuhumiana rushwa mbele ya wananchi bila huruma mchana kweupe,mtawaambia nini wananchi? Hii aibu mnaificha wapi?

Hivi hawa kina Dr Bashir Ally wanaozunguka nchi nzima kuwaambia wananchi kua awamu ya 5 imejipambanua kwa kukomesha vitendo vya rushwa hamuogopi Mungu? Haya malumbano ya Rushwa dhidi ya viongozi wakubwa kabisa makada wa CCM hamuoni kua yanawavua nguo mchana kweupe? Mnawadanganyia nini wananchi? Mteteeni Sabaya kwa kisingizio kua ni propaganda za kisiasa za Mbowe dhidi yake ili aondolewe Hai lakini Mungu hua sio wa kukebehiws.
Nilishaandika na kuandika kuwa tumebadilisha wadolozi kwa wakwapuaji wanaotumia bunduki yaani majambazi. Kiongozi wao ni jambazi mkuu
 
Rushwa imetamalaki sana wakati huu, tena kwa sasa ni kwa nguvu kabisa. Bashite style
 
mwacheni mkuu wa wilaya apige kazi hizo nituhuma ambazo hazina ukweli wowote uli ni njama za wapinzn wakiongozw na mbowe kumkwamisha mkuu wawilaya
Upuuzi kabisa huu, hakuna Mtanzania mijinga ninyi mnakula rushwa mnasumbua sana wafanyabiashara. Eti unasingizia Shamba, mambo ya kodi na shamba wapi na wapi?
 
Hata mm ningefurahi sana Mh. Rais JPM awachukulie hatua kali kabisa RC Mnyeti na DC Sabaya, sbb dalili zote za rushwa ziko wazi..
 
Back
Top Bottom